Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Haya tuliyajua.Ndio maana serikali inasita kuchukua hatua kukomesha tatizo hili,kwa vile wanaohusika ni vigogo wenyewe.Aibu sana.
 
Wakazi wanane wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya akiwemo mfanyabiashara maarufu wa kuuza vipuri vya magari, wametiwa mbaroni kwa tuhuma za kutaka kumteka na kumuua albino.

Mfanyabiashara huyo, Benedicto Mwachembe (45) na wenzake walikamatwa Desemba 16, mwaka huu asubuhi baada ya jaribio lao hilo kushindikana.

...mtoto huyo aliwataja watuhumiwa wawili kati ya hao kuwa ni Thomas Lugoma (26) na Aizeck Lugoma (32) ambao ni wanafamilia wa Power ambaye ni baba mzazi wa albino huyo.

source; Mfanyabiashara amtaka albino akiwa yu hai

...attention wakubwa, this is not a laughing matter anymore, hasa inapoanza kuhusisha wanafamilia, dalili za ethnic cleansing zinanukia...!!!
 
Japo swala la ndugu zetu, wadogo zetu wenye ulemavu wa ngozi linatusikitisha sana hasa pale unaposikia upumbavu wa binadamu wa karne ya 21 eti atakuwa tajiri akifanya hivyo. Kwa kweli naungana na wote wanaolaani upumbavu huu.

Lakini, bado najiuliza siku ile mzee mzima Pinda, alipokuwa akijibu swali ambalo alipewa shinikizo la kujiuzuru kama hataweza kutosheleza maelezo, "on that particular time what really was ringing in his mind"? Was it the emotional sadness of albino killings or a great fear that he might ending up resigining? I guess the later could be mostly true.
 
- emotional sadness of albino killings (like any other good and responsible citizen)? = T

- great fear that he might ending up resigining (like any other politician)? = T

- therefore alitosheleza maelezo

- 🙄
 
Mimi kwa maoni yangu yalikuwa ni machozi ya kinafiki tu kwa kuhofia kwamba kauli aliyoitoa ilikuwa haikubaliki na Watanzania wengi na hivyo kuhofia kupoteza wadhifa wake.
 
As we re great thinkers, Nadhani tuna wataalamu for doing research kweli tujiulize all albinos wamezaliwa awamu ya nne???? y now?? Kwani awamu ya tatu walisurvive vipi?? ya pili je?? Na ya kwanza??
Then let be wise kuna other place huwezi kukuta mlemavu wa aina yoyote y?? Ukweli ni kwamba nikiwa mdogo i heard that people huwa ni wa ajabu wanapoteaga tu??? Let start from there then we can get real solution, i think walikuwa wanauawa kimya kimya!
The situation is boring WaTZ ,kwani slogan ya hari mpya nguvu mpya ikitumika unadhani yataendelea haya???
 
You are right mazee ! Why now?
 
Kwenye gazeti la The Express leo kuna habari kuwa waganga wawili waliotuhumiwa kumuua albino mkazi wa kijiji cha Kiwira wameachiliwa huru kwa amri ya DPP.
Waganga hao ni Asangalwise Katite na Gererde Kalonga na walikamatwa Feb 27 2008 baada ya kukutwa na viungo vya albino.
 
Mchungaji ‘akutwa’ na vipande vya albino
Merali Chawe, Mbeya
Daily News; Tuesday,February 17, 2009 @19:17

Mchungaji wa Kanisa la Pentecoste lililopo Idiwili Kata ya Iyula, wilayani Mbozi anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kukutwa na mabaki ya mwili wa binadamu yaliyokuwa yakiuzwa Sh milioni 30.

Cosmas Mwasenga (39) alikamatwa Februari 13 mwaka huu akiwa na Luseshelo Mwashilindi ambaye inadaiwa alikuwa ameyahifadhi nyumbani kwake mabaki hayo. Mabaki hayo ambayo Polisi inahisi kuwa ni ya albino, ni vipande vinne vinavyosadikiwa kuwa sehemu ya mikono.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Zelothe Stephen alisema leo kuwa watuhumiwa hao walikamatwa katika eneo la Mlowo, Mbozi. Akizungumzia tukio hilo, Kamanda Zelothe alisema Februari 12 mwaka huu, polisi walipata taarifa kuwa kuna kikundi cha watu Mlowo, wana vipande vya mabaki ya mwili wa mwanadamu vinavyosadikiwa kuwa ni mabaki ya mwili wa albino.

Alisema taarifa hizo zilidai kuwa kikundi hicho kilikuwa kinatafuta wateja ili kuwauzia vipande hivyo na kwamba watu waliokuwa wanatafuta wateja waligawanyika katika Wilaya ya Mbozi na baadhi ya mitaa ya Jiji la Mbeya.

“Tuliweka mtego na kukutana na watu hao ambao walisema wanauza viungo vya ‘kunguru mweupe’ wakimaanisha albino, ambapo walikubaliana na kukutana na Mwashilindi ambaye alikuwa anahifadhi viungo na kufikia makubaliano ya kuvinunua kwa Sh milioni 30,” alisema.

Alisema Februari 13, taratibu za kupata kiasi hicho cha fedha zilikamilika na walipofika kwa Mwashilindi alitoka akiwa na vipande vinne vya mabaki ya binadamu vikiwa vimefungwa katika karatasi, na Polisi wakamkamata. “Baada ya kupekua katika nyumba ya Mwashilindi tulifanikiwa kupata dawa za binadamu, maji ya kuchanganya na dawa na koti jeusi mali ya Mchungaji Mwasenga,” alisema.

Aliongeza kuwa watuhumiwa wote wawili wanashikiliwa na watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika. Kamanda Zelothe alisisitiza umuhimu wa wananchi kutoa taarifa Polisi na kusema kwa kufanya hivyo, ndipo vitendo vya mauaji ya albino vitapungua. “Tunapenda kuwaomba wananchi waendelee kutoa taarifa za siri kwa viongozi wa juu, ili ziweze kufanyiwa kazi haraka,” alisema.
 
Hii ni aibu na kweli,

Pentekoste sii Walokole???

Vipi tena??

Tuamini dini/thehebu gani?
 
la maana ni kuwa endapo wana kesi nzuri na ushahidi usio shaka na jamaa wakakutwa na hatia, wananchi waliotoa taarifa hiyo wazadiwe kutoka zile milioni kadhaa!! This is how we gonna defeat them! Sasa kama wale wananchi wangefuata agizo la Waziri Mkuu la kuwaua papo hapo ingekuwaje?
 
Hivi viungo vya ma-Albino vinawasaidiaje watu? Maana hata ukiangalia maisha wanayoishi ni ya kifukara kweli kweli. Wanafaidikaje hawa watu? Sisi Miafrika tuna imani za ajabu sana aisee
 
Hii habari si ndio ilichapishwa katika gazeti la wiki zilizopita na ilipata kujadiliwa humu humu.
Si ndie huyu mchungaji aliekataa kula kiapo kwa kutumia Biblia na si ndio watu hawa walioachiwa na mahakama kwa kuonekana hawana hatia au hii ni watu wengine ?
 
Mchungaji ‘akutwa’ na vipande vya albino
Merali Chawe, Mbeya
Daily News; Tuesday,February 17, 2009 @19:17

Mchungaji wa Kanisa la Pentecoste lililopo Idiwili Kata ya Iyula, wilayani Mbozi anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kukutwa na mabaki ya mwili wa binadamu yaliyokuwa yakiuzwa Sh milioni 30.

Cosmas Mwasenga (39) alikamatwa Februari 13 mwaka huu akiwa na Luseshelo Mwashilindi ambaye inadaiwa alikuwa ameyahifadhi nyumbani kwake mabaki hayo. Mabaki hayo ambayo Polisi inahisi kuwa ni ya albino, ni vipande vinne vinavyosadikiwa kuwa sehemu ya mikono.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Zelothe Stephen alisema leo kuwa watuhumiwa hao walikamatwa katika eneo la Mlowo, Mbozi. Akizungumzia tukio hilo, Kamanda Zelothe alisema Februari 12 mwaka huu, polisi walipata taarifa kuwa kuna kikundi cha watu Mlowo, wana vipande vya mabaki ya mwili wa mwanadamu vinavyosadikiwa kuwa ni mabaki ya mwili wa albino.

Alisema taarifa hizo zilidai kuwa kikundi hicho kilikuwa kinatafuta wateja ili kuwauzia vipande hivyo na kwamba watu waliokuwa wanatafuta wateja waligawanyika katika Wilaya ya Mbozi na baadhi ya mitaa ya Jiji la Mbeya.

“Tuliweka mtego na kukutana na watu hao ambao walisema wanauza viungo vya ‘kunguru mweupe’ wakimaanisha albino, ambapo walikubaliana na kukutana na Mwashilindi ambaye alikuwa anahifadhi viungo na kufikia makubaliano ya kuvinunua kwa Sh milioni 30,” alisema.

Alisema Februari 13, taratibu za kupata kiasi hicho cha fedha zilikamilika na walipofika kwa Mwashilindi alitoka akiwa na vipande vinne vya mabaki ya binadamu vikiwa vimefungwa katika karatasi, na Polisi wakamkamata. “Baada ya kupekua katika nyumba ya Mwashilindi tulifanikiwa kupata dawa za binadamu, maji ya kuchanganya na dawa na koti jeusi mali ya Mchungaji Mwasenga,” alisema.

Aliongeza kuwa watuhumiwa wote wawili wanashikiliwa na watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika. Kamanda Zelothe alisisitiza umuhimu wa wananchi kutoa taarifa Polisi na kusema kwa kufanya hivyo, ndipo vitendo vya mauaji ya albino vitapungua. “Tunapenda kuwaomba wananchi waendelee kutoa taarifa za siri kwa viongozi wa juu, ili ziweze kufanyiwa kazi haraka,” alisema.

Disgusting... Jamani alikuwa anaviombea...! Si mnajuwa tena wenzetu wapindwa katika maombi na kuombeana...! Labda ivyo viungo vinatumika katika yale mambo ya kugusana kwenye kipaji na kuangushana... ili kuonyesha kuwa jamaa katembelewa na roho mtakasifa...! Dah! Sasa Hizi dini na imani zingine ni balaa...! Very disgusting!
 
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,Bw.Zelothe Stephen aliwataja watuhumiwa wawili kuwa ni Mchungaji wa kanisa la Pentekoste Idiwili,Cosmas Mwasenga (39) na Luseshelo Mwashilindi (38) ambao walikutwa na viungo vinavyodhaniwa vya maeneo ya mikono wakipita kutafuta wateja huku wakiviita kwa jina la ¡viungo vya Kunguru mweupe¢.

Kamanda Stephen alisema kuwapolisi walipokea taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu kuwepo watu waliokuwa wanatafuta wateja wa viungo hivyo vya albino katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya Makunguru na Mwanjelwa wakitamka jina la kunguru mweupe.

Alisema kuwa polisi baada ya kupata taarifa hiyo waliweka mtego kwa kujifanya wanunuzi ambapo baada ya kupata bei hiyo walikwenda kuchukua viungo hivyo kwa mtuhumiwa Mwashilindi na kuvikuta huku vikiwa vimefungwa kwa mafungu mawili yaliyokuwa na vipande vinne vya viungo hivyo vikiwa vimewekwa katika karatasi.

Aidha Kamanda Stephen alisema kuwa baada ya kuwakamata watuhumiwa wote wawili walikwenda kufanya upekuzi katika nyumba ya Mchungaji Mwasenga na kufanikiwa kukuta chupa ya dawa ya sindano ya kutibu binadamu aina ya Penicilline na maji yake sanjari na koti jeusi.

Kamanda Stephen alisema watuhumiwa wamekamatwa na watafikishwa mahakamani muda wowote baada ya uchunguzi kukamilika na kwamba viungo hivyo vinatarajiwa kufikishwa kwa mkemia mkuu kwa uchunguzi zaidi.

Katika tukio jingine Kamanda Stephen alisema Bw.Saimon Masawe (42),mkazi wa Ivumwe (Baba mzazi wa kijana mwenye ulemavu wa ngozi) pamoja na balozi wa mtaa wa Ivumwe wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuhusika kumnyoa nywele kijana huyo sanajri na kutowajibika kumlinda mlemavu huyo wa ngozi.

Kamanda Stephen alisema kuwa mnamo februari,5 mwaka huu majira ya saa 12.45 asubuhi kijana huyo aliamka na kwenda shuleni lakini baada ya kufika umbali wa mita 400 na kubakisha mita takribani 600 alivamiwa na kukamatwa na watu watatu wakiwemo wanaume wawili na mwanamke mmoja na kumficha karibu na tanuri la matofari.

Alibainisha kuwa kijana huyo alidai kuwa alikalishwa katika kaaratasi la nailoni na kuanza kunyolewa nywele zake za katikati na kubakishwa nywele za pembeni mithili ya mtu mwenye upara ambapo wakati zoezi hilo linaendelea alipita mtu akiwa katika baiskeli akiendelea na safari zake bila kujuwa kilichokuwa kinatendeka na ndipo watu hao waliingiwa na hofu na kukimbia.

Kamanda huyo alifafanua kuwa kabla ya kukimbia watu hao walimchanja kwa wembe chale mbili ndogo katika mkono wake wa kushoto na kumtelekeza kijana huyo ambaye baadaye aliondoka kuelekea shuleni akiwa ameficha kichwa chake kwa kofia bila kumweleza mtu yeyote hadi aliporejea nyumbani na kumweleza mama yake mzazi aliyetajwa kwa jina la Upendo masawe (40).

Alisema kuwa baada ya kupokea taarifa hiyo Mama huyo aliwaita majirani pamoja na balozi kuwasimulia mkasa huo na ndipo walipochukua hatua ya kutoa taarifa polisi ambapo baada ya kumhoji baba yake mzazi alidai aliondoka mapema alfajiri kuelekea shambani na kurudi usiku na kukuta taarifa hiyo.

Kamanda Stephen alisema kuwa baada ya mahojiano hayo polisi wanamshikilia baba wa kijana huyo kwa uzembe wa kutomfuatilia kijana wao huku wakijuwa kuwa maisha yao yapo hatarini ambapo balozi ametiwa mbaroni kwa kutowajibika ipasavyo kuhakikisha mlemavu huyo analindwa muda wote kuanzia nyumbani hadi shuleni mpaka anarudi nyubani.

Hata hivyo kamanda Stephen alifafanua kuwa kama ilivyoamua serikali kupania kuwalinda kwa nguvu zote watu wenye ulemavu wa ngozi na ndivyo viongozi wengine na wananchi kwa ujumla wakiwemo wazazi wanavyotakiwa kuwajibika.

source:Dullonet Tanzania | Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste akamatwa na viungo vya Albino.
 
Mmh..I can imagine kazi bado kubwa

Ina maana hawa ndugu zetu inabidi wawe na mabody guards 25/7?
 
Back
Top Bottom