Mauaji ya Bodaboda Kongwa

Mauaji ya Bodaboda Kongwa

The Eye

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2020
Posts
278
Reaction score
393
Kumekuwa na wimbi la wizi wa pikipiki na hata mauaji kwa vijana wanaofanya kazi ya kusafirisha abiria kwa pikipiki wilayani Kongwa-Dodoma.

Wiki tatu zilizopita Kijana mmoja aliyekuwa akifanya kazi hiyo Kongwa mjini alipotea kwa kipindi cha wiki mbili na baadae kukutwa akiwa amefariki na mwili wake ulikuwa umeharibika na kubaki mifupa.Mwili wake uliokotwa kijiji cha Suguta wilayani humo umbali wa takribani kilomita 40 kutoka Kongwa mjini.

Usiku wa kuamkia jana yaani tarehe 7 May. Kijana mwingine kutoka Pandambili "alichinjwa" na kuporwa pikipiki yake.

Matukio mengine yamekuwa yakifanyika kwa kuporwa pikipiki bila wenye nazo kuuawa matukio ya namna hii yakemewe haraka kwani yanaleta taharuki kwa watu.

©TanzaLand
Kongwa-Dodoma
 
Dah,Siyo poa kabisa. Wapumzike kwa Amani Bodaboda.
 
Changamoto za jimboni kwake Ndugai huwa anazifuatilia kweli? Maana akikalia kile kiti anachojua ni wanawake waliofukuzwa Chadema.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom