Mauaji ya Bodaboda Kongwa

Mauaji ya Bodaboda Kongwa

Kumekuwa na wimbi la wizi wa pikipiki na hata mauaji kwa vijana wanaofanya kazi ya kusafirisha abiria kwa pikipiki wilayani Kongwa-Dodoma.

Wiki tatu zilizopita Kijana mmoja aliyekuwa akifanya kazi hiyo Kongwa mjini alipotea kwa kipindi cha wiki mbili na baadae kukutwa akiwa amefariki na mwili wake ulikuwa umeharibika na kubaki mifupa.Mwili wake uliokotwa kijiji cha Suguta wilayani humo umbali wa takribani kilomita 40 kutoka Kongwa mjini.

Usiku wa kuamkia jana yaani tarehe 7 May....Kijana mwingine kutoka Pandambili "alichinjwa" na kuporwa pikipiki yake.

Matukio mengine yamekuwa yakifanyika kwa kuporwa pikipiki bila wenye nazo kuuawa....matukio ya namna hii yakemewe haraka kwani yanaleta taharuki kwa watu.



©TanzaLand
Kongwa-Dodoma
Ndugai yupo hapo dodoma mjini akimnanga jjm kwa mipasho yake iliyokosa vina! Hebu aende jimboni kwake kuthibiti huu ujambazi!
 
Tatizo lako una akili za kichawi sana.

Tunaongelea masuala ya mauaji wewe unaleta habari za punda.
Ndio nimekuambia hongereni hapo Kongwa kwa kupata bodaboda!

Wakati nakuja hapo Kongwa na basi pekee la Shabiny tulikuwa tunaikuta mikokoteni ya punda hapo stendi!
 
Back
Top Bottom