Mauaji ya halaiki ya Watanzania MO 29 yaingizwe kwenye syllabus ya somo la history

Mauaji ya halaiki ya Watanzania MO 29 yaingizwe kwenye syllabus ya somo la history

Makongodcrue

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2025
Posts
1,864
Reaction score
2,591
Wanajamvi
Mo 29 na kuendelea ni kipindi ambacho nchi yetu iliingia katika kiza kinene, anga lake likiwa limefunikwa na damu, huku ardhi yake ikilalamika kuelemewa na miili ya Tanganyika ikiomba msaada wa kuhifadhiwa na ndugu zao.

Ni kipindi ambacho nchi yetu imeingia katika historia mbaya zaidi ya mauaji ya halaiki ya Watanzania kwa manufaa ya wachache kukalia dola.

Watoto wetu na wajukuu zetu na vizazi vijavyo vinatakiwa kufahamu haya, vinatakiwa kufahamu ni kwa namna gani wazazi wao waliuwawa ili watu fulani wafaidi mema ya nchi kwa kigezo cha kulinda amani.

Ni muda muafaka sasa hili tukio kuingia kwenye somo la historia ili vizazi vijavyo wajifunze kilichotokea katika nchi yao.
 
Kuingizwa inawezekana na hata isipokuwa hivyo historia itaandikwa kuhusu hili tukio.

Sema mpaka sasa hakuna idadi rasmi ya watu waliokufa,nani alitoa amri ya kuuliwa kwa watu(hapa speculations kibao japo kiongozi mkuu ndio anabeba huu mzigo).

Ni kitu gani kilifanya wauaji wafanye yale mauaji?(Mfano yale ya Rwanda ilikuwa ni kati ya kabila mbili.Je,hii ya kwetu wauaji walikusudia nini kufanya vile)

Ukishapata majibu ya maswali kama hayo unaweza kurahisisha uandishi wa hili tukio katika historia
 
Back
Top Bottom