Mauaji ya Kimbari ya Yugoslavia yaliyosahaulika

mcTobby

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2018
Posts
4,072
Reaction score
12,119
Wadau , wakubwa kwa wadogo natangauliza salamu zangu kwenu, natumai mu buheri wa afya .

Nadhani wengi wenu mliopita shuleni hususani advanced level mnamkumbuka mwamba mmoja aliyejulikana kama Josip brozi Tito, rais wa yugoslavia. Ingawaje historia inamsema vizuri kutokana na ujasiri wake wa kukataa kuwa chawa wa kiongozi wa umoja wa kisoviet wakati huo bwana stalin , lakini chini ya kapeti utawala wake uligubikwa na unyanyasaji wa makundi kadhaa yaliyokuwepo ndani ya yugoslavia,mauaji ya koholela pamoja na utekaji na vifungo kwa wapinzani wake wa kisiasa.


Tito kwenye historia huonyeshwa kama kielelezo na mfano wa kuigwa kama kiongozi aliyeiunganisha yugoslavia iliyosaidia kudhibiti vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini mwake.
Lakini kwa wengi wa raia , wengi waliona nchi yao kama gereza kubwa

Kivipi? Twende kazi. Baada ya vita kuu ya pili ya dunia kuisha mwaka 1945, makundi kadhaa ndani ya yugoslavia ambao walikuwa wakiupinga utawala wa wa Brozi Tito walijisalimisha kwa jeshi la ukombozi la uingereza ( British expeditiary Force), lakini waingereza wakawakabidhi hawa walio salimu amri kwa utawala wa brozi Tito. Makundi haya yaliyopigana na utwala wa Tito ilikuwa ni jamii za watu wa Croatia, waserbia na wa Slovenia ndani ya yugoslavia.



Kilichofuata baada ya hapo ni jambo lililoisikitisha dunia japo jambo hili lilifichwafichwa.
Inakadiriwa raia wapatao 50,000 waliuliwa pasipo kufunguliwa mashtaka ( summary execution).
Raia ,hususani wanawake na watoto ndio waliokuwa waathirika wakubwa.

Ndani ya yugoslavia kulianzishwa death marches , ambapo raia waliokuwa wanampinga josep brozi tito walilazimishwa kujipanga kwenye mistari na kisha kutembea hadi sehemu maalumu ambapo wangeuliwa. Hii ilijulikana kama " way of the cross " au njia ya msalaba. Ndugu zangu wakatoliki wanaelewa hapa vizuri.
Ujumbe wa rais huyu wa Yugoslavia ulikuwa clear " No mercy to those who oppose him.

Pia jeshi la josep brozi tito liliwalenga makundi ya waitaliano waliokuwa kwenye miji midogo ya istria na dalmatia,(kwa sasa miji hii ni sehemu ya nchi za Slovenia na croatia). Lengo la kuwakamata waitaliano pamoja na kuzichukua Mali zao ni kisasi dhidi ya utawala wa Mussolini Dikteta wa Italia aliyekuwa amekalia kimabavu maeneo ya yugoslavia.
Inakadiriwa zaidi ya waitaliano 10,000+ waliluliwa kwa kutumbukizwa kwenye shimo moja lililojulikana kama FOIBE. Wengine wakanyang'anywa Mali zao na kufukuzwa .
Kwa kifupi tito alikuwa anafanya kitu kinachojulikana kama ethnic cleansing .




Kwa sasa nchi ya italia huadhimisha siku ya mauaji haya kama " Foibe remembrance day" kila ifikapo tarehe 10 February. Kwa ajili ya kuwakumbuka wale wote waliouliwa kwa kutumbukizwa ndani ya shimo la foibe na utawala wa tito


Na pia kabla hata ya vita ya pili ya dunia zaidi ya raia laki tano jamii za wajerumani ambao ni swabian Danube ,walikuwa wakiishi ndani ya yugoslavia lakini tito alitaka kuwafuta wote kabisa. Wengi waliuliwa ikikadiriwa idadi ni wajerumani laki moja. Wengine walifungwa kwenye kambi za mateso ili wafie huko na njaa huku wengine zaidi ya wajerumani laki mbili na nusu wakifukuzwa kwenda kwao Ujerumani. Vijiji vyote walimokuwa wanakaa jamii hizi vikafutwa kwenye ramani.


Vilevile jamii za waserbi wa chetniks waliokuwa wakiendesha vuguvugu wakipinga unazi na ukomunisti waliitwa maadui wa taifa la yugoslavia. Na kweli , kati ya mwaka 1945 hadi 1946 wengi wao waliuliwa huku familia zao zikifungwa jela au kupelekwa uhamishoni. Na pia makanisa ya wa Serbia ya orthodox yalivunjwa na kuharibiwa.


Kwa kifupi baada ya josep brozi tito kutwaa madaraka alihakikisha hakuna upinzani dhidi yake ndani ya yugoslavia.
Na kweli wengi wafungwa wa kisiasa waliishia kwenye kambi za mateso na wengine walifungwa kwenye gereza la Goli Otok ,moja ya gereza baya zaidi huko yugoslavia wakati huo.
Gereza hili ambalo lilikuwa kisiwani ndilo lililokuwa likiwafunga wakisindikizwa na mateso makali kwa wale wote walio mpinga tito.

gereza la Goli Otok


Josep brozi tito hakuishia hapo. Wale wote waliokuwa wanampinga wakiwa nje ya Yugoslavia hususani marekani, Argentina na hata Ujerumani aliwatumia " kikosi kazi" na kuuliwa na Wasiojulikana . Hii ina maana yugoslavia ilikuwa ni police state .

Sera ya huyu bwana tito ya "brotherhood and unity" yaani undugu na umoja ilikuwa ni sera ya kulazimisha makundi au jamii tofauti tofauti( waserbia ,wa Slovakia,wa Slovenia na jamii zingine) ziishi kwa pamoja ndani ya serikali kuu "central government " lakini minyukano iliendelea chini kwa chini. Kwa sera yake hii ilisaidia kudhibiti vita vya wenyewe kwa wenyewe visitokee mpaka ilipofika miaka ile ya 1990 moto wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipolipuka.
Huyu mwamba alipokufa mwaka 1980 nchi ya yugoslavia ikatumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyopelekea umwagaji mkubwa wa damu. Kitu ambacho hakutaka kitokee ndani ya nchi yake ya yugoslavia .

Yote kwa yote wanahistoria wanafunika uovu wake kutokana na ukweli ya kwamba alimpinga stalin waziwazi hadharani. Ila Ukweli ni alikuwa mhusika mkuu wa mauaji ya kimbari ndani ya yugoslavia.
 

Attachments

  • 20250226_182757.jpg
    69.8 KB · Views: 2

Hii ni katuni iliyochapishwa kwenye magazeti ya ki soviet ikimkosoa josep brozi tito kiongozi huyu wa Yugoslavia kama ndumi la kuwili . Hapa akijifanya kupokea misaada kutoka west kwa siri huku yeye akijifanya kuwa ni neutral 😐.
All in all huyu mwamba alikuwa kipenzi cha mchonga. Picha chini Hapa wakisalimiana baada ya kutembelea Tz miaka ya 1970.
 
Muelezee pia huyu mwamba aliesumbua sana enzi hizo kwenye Jimbo la Kosovo adi kuzaliwa kwa nchi ya Kosovo- bwana Slobodan Milošević
 
Vitu kama hivi ndio inapoteza maana ya maisha... Ila tatizo raia nao ni wabishi sana hivyo ukiwa kama kiongozi kuna wakati inabidi uvae koti refu la ibilisi
 
Nchi za Ulaya zilipitia kipindi kigumu sana cha vita za wao kwa wao, waasi, madikteta, mapinduzi mpaka leo wengi wao wako imara na wanalinda nchi zao yasijirudie yaliyopita.

Au ni lazima nchi zipate hizo tabu ndio ziwe imara na zenye maendeleo, si ajabu Congo ikaja kua kama ulaya 😂😂
 
Vitu kama hivi ndio inapoteza maana ya maisha... Ila tatizo raia nao ni wabishi sana hivyo ukiwa kama kiongozi kuna wakati inabidi uvae koti refu la ibilisi
Shida ni kua ukizikwa unazikwa na falsafa zako labda uandae mrithi, na mrithi aandae mrithi iwe hivyo kwa miongo kadhaa.
 
Muelezee pia huyu mwamba aliesumbua sana enzi hizo kwenye Jimbo la Kosovo adi kuzaliwa kwa nchi ya Kosovo- bwana Slobodan Miloševićun
Umenikumbusha filamu ya Behind the enemy line.
 
Ni wazalendo haswa . Popote wawapo duniani wana feel ile pride ya utaifa wao
 
Uingereza hii ya malkia ilipitia kichapo cha Hitler sema tu ndio hivyo historia kubwa zinaandikwa na wao pamoja na wale wanahistoria wasiokuwa neutral🤣
 
Kuna muda watawala wanagubikwa na kitu kinaitwa inferiority complex inawapelekea kugeuka wauaji...kisa tuu hawataki kupingwa..na mtawala ikimuingia hii akili ya kukataa kupingwa walai watu watateseka sana...ni kuombea tuu huyo kiongozi afe..tumshukuru Mungu tunaishi zama ambazo kuna utandawazi taarifa zinafika kwa wakati..kuna taasisi za kutetea haki za binadamu..mashirika ya kimataifa n.k..otherwise I feel sorry...very sorry kwa walioishi miaka hyo kabla ya world war 2..walipitia mateso makali...hasa kwa nchi za ukomunist..
Japo kuna majirani zetu na sehemu zingine za Africa yani wao ndo wameona fasheni sasa kupigana na kuuana..kujimilikisha mimali huku wananchi wao wana umaskini wa kutupwa...

Picha inasikitisha sana hii ya watoto...hawana makosa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…