Mauaji ya Kimbari ya Yugoslavia yaliyosahaulika

Nchi za Ulaya zlipita kipindi kigumu lakini huko hoja yao ilikuwa ni ya kisiasa zaidi i.e. kuwanyamazisha wapinzani kwa kuwaua na hakuna vilivyokuwa mali zilizokuwa zinachukuliwa (kama ilikuwepo ni kidogo), uporaji wa ardhi au mali za Jamii fulani. Hapakuwa na Taifa kutoka nje lililoingia kwa uwazi kuunga mkono yaliyokuwa yakitokea.
Lakini huko Congo DRC hoja ni pamoja na Ukabila, Utawala, Uchukuaji wa madini (Rasilmali ), watu raia kuuawa na utekaji /uporaji wa maeneo makubwa ya nchi. Halafu kuna Taifa la nje limejiingiza kwa uwazi kuunga mkono wapinzani wa Serikali ikiwa ni pamoja na kutoa misaada ya kijeshi kwa wapinzani.
Ukiangalia hizo scenario mbili utaona ni tofauti kabisa. Kwa hiyo Congo haiwezi ikaja kuwa kama Ulaya bali Congo DRC itasambaratika , itamegeka kuwa ni nchi 2 au 3 na bado kutakuwa na mwendelezo wa mauaji ya kuvizia ya kikabila Watutsi vs Wahutu.
 
Uingereza hii ya malkia ilipitia kichapo cha Hitler sema tu ndio hivyo historia kubwa zinaandikwa na wao pamoja na wale wanahistoria wasiokuwa neutral🤣
Wanaficha aibu ndogondogo zinazozuilika kiwepesi 😂😂, mshindi ndio huratibu historia yote hata kama huko nyuma uliwahi kumtwanga ushindi wake ndio utakua maarufu.
 
Ni wazalendo haswa . Popote wawapo duniani wana feel ile pride ya utaifa wao
Kwasababu babu zao waliipambania, sisi tumechelewa sana kujitambua mpaka kutawaliwa. Nchi imejikusanya kwa uzuri baada ya ukoloni.
 
Ni kweli kabisa. Halafu inashangaza waliopo madarakani wanasahau kwamba hapa duniani hawataishi milele - iko siku watake wasitake watayaacha madaraka yao aidha kwa kifo cha kawaida au kuuliwa au kutokana na uzee. Wanajilimbikizia mali za damu na umwamba wa siku chache.
 
Huenda wakongo wakajifunza uzalendo kupitia hayo machafuko, akipatikana kiongozi awaunganishe hata kwa mkono wa chuma.
 
Huenda wakongo wakajifunza uzalendo kupitia hayo machafuko, akipatikana kiongozi awaunganishe hata kwa mkono wa chuma.
Chuki ya Kikabila (Ukabila) ni MBAYA sana tena pale inapokuwa ni chuki ya kulipiza kisasi kwa mtindo wa kuuana. watu wa Kabila fulani wanaua watu wenzao wa kabila lingine tofauti na wanajisikia kujivunia jambo hilo.
Hiyo ni laana; haitokaa iishe. Wanasema inadumu hadi kizazi cha NNE.
 
Wachanganye damu kama hapa bongo, mchaga kaoa/kuolewa na mnyakyusa na mtoto wao kaoa/kuolewa na mngoni na mjukuu kaenda kulowea Tanga kaoa/kuolewa na mbondei.

Huko hizi mambo hakuna, kwamba mhutu hawezi kuoa mtutsi??
 
Wachanganye damu kama hapa bongo, mchaga kaoa/kuolewa na mnyakyusa na mtoto wao kaoa/kuolewa na mngoni na mjukuu kaenda kulowea Tanga kaoa/kuolewa na mbondei.

Huko hizi mambo hakuna, kwamba mhutu hawezi kuoa mtutsi??
Excellent. Hiyo njia ndo Mujarab sana. e.g Wamasai huku Kiteto wameoa Warangi na Wagogo; japokuwa mwanamke wa Kimasai pure kuolewa na kabila lingine kuna changamoto zake. Sasa Wamasai wanaitana na Warangi ni Watani (waliwahi kupigana vita) tena ni mashemeji Ke waKirangi wameolewa Umasaini. Hapo sio rahisi tena Mmasai amuue Mtani wake na Shemeji yake. Ugomvi ukitokea baina yao (Mrangi vs Mmasai au Mgogo vs Mmasai) huwa unamalizwa na wazee kirahisi sana.
Umewaza mbali sana mkuu.
 
Kwenye ukabila kidogo na sisi tumejitahidi.

Nakumbuka mwaka fulani nuko advance nyanda za juu kusini huko. Ile shule walikua wanaletwa wanafunzi toka kaskazini kwa asilimia zaidi ya 85 na wanafunzi wengine wanatokea maeneo ya kaeibu hapo.

Hiyo mbinu nayo ilisaidia kuua hilo pepo la ukabila na ukanda.
 
Asante kwa Mwaliko.
Binafsi nimesoma hii historia kwa namna mbili darasani na mtandaoni.

Nilipata kujifunza mambo mawili muhimu hasa katika mauaji ya kimbali .

Ukabila - swala la ukabila sio tu linaweza kuigawa nchi ikabaki vipande vipande.

Jambo la pili nilijifunza kuhusu Haki-ukiwanyima haki , utaliza makundi na katika hayo makundi ndo yataibuka makabila , wanachama Kama NETO n.k


Ila kwakuwa Africa ni sikio la kufa bado kuna viongozi wanasiasa ambao wanacheza na haki za raia wao mfano Tanzania miaka ya nyuma iliwahi kupata kiongozi aliyekuwa anaubiri Amani Ila anaogopa kuhubiri haki.



 
Inashangaza sana...tumepungukiwa maarifa...
 
Wanaficha aibu ndogondogo zinazozuilika kiwepesi 😂😂, mshindi ndio huratibu historia yote hata kama huko nyuma uliwahi kumtwanga ushindi wake ndio utakua maarufu.
🤣🤣 kabisa. Nikipata wasaha nitaleta kisa chake hapa. Alichapika yeye na beshte yake mfaransa kichapo kitakatifu.
Karibu sana. Haki ni natural basic need kwa kila kiumbe haswa mwanadamu. Ukimnyima mtu haki yake ndio hapo anapoitafuta in a hard way hapo ndipo yanaibuka machafuko katika jamii. Historia haidanganyi
 
Ni vizuri tukawa watu wa kujifunza kutokana na makosa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…