Mauaji ya Mzee Karume: Acha sasa tuhoji yasiyohojika!

Mauaji ya Mzee Karume: Acha sasa tuhoji yasiyohojika!

labda niseme tu kuwa wewe ni mdogo sana na hukuyakuta mapinduzi
na ni wale kindakindai mnayoyakataa mapinduzi mkimtaka Jamsheed arudi
View attachment 993073
Field Marshal Okelo mwenye kofia na wanamapinduzi wa kweli sio Karume aliyejificha Dar es salaam
nimekutafutia tafsiri ya Kiswahili iliyoandikwa na Joseph Mihangwa aliyekuwepo Zanzibar kipindi hicho na alikuwa akitoa Makala zake RAI Tanzania sijaipata
Atrocities of Amin: John Okello (Field Marshall)

GuDume naona umeshamjua huyu mtu kaliba zake na ni wale walioyapinga mapinduzi na kubadili kabisa historia ya nguvu za Okello
mm nimeachana naye kwa vile tu Mada ni ya kifo cha Mh Karume na muuaji wake ni Kanali Humud Humud
acha mada iendelee

Acheni kuishi kwa misingi ya Propaganda
 
Mauaji ya Sheikh Karume ni halali kwa kiasi kikubwa sababu hakutaka kuimarisha umoja ndani ya taifa lake na badala yake alijenga jamii yenye mifarakano hasa kwa wafuasi wa ZPPP na Hizbu. Kuwafukuza kazi na wengine kuwataka watoke warudi kwao mwaka 1964 waarabu walioingia Zanzibari karne ya 11 yaani mwaka 1100's. Baada ya mapinduzi watu wenye asili ya kiarabu walinyang'anywa mali na vitu vyao walivyokuwanavyo kwa zaidi ya miaka 500. HUU ULIKUWA NI UKATIRI WA HALI YA JUU hata kama kweli au kwa kiasi fulani walipata vitu hivyo kwa unyonyaji Zanzibari ni nyumbani kwao hawana sehemu nyingine.

Hujuma ndani ya ASP dhidi ya viongozi aliowaona kuwa na ushawishi kuweza kuhatarisha utawala wake kuwaua, kuwatesa, kuwafunga jela, kuwafukuza Zanzibari kwa kuwateua kuwa Mabalozi, Mawaziri serikali ya Muungano. Hiyo ilijenga chuki kubwa baina yake na mavamizi wenzake, TAYARI AMEJENGA MAADUI WAWILI.

MUUNGANO wa Tanganyika na Zanzibari, kupitia historia na miaka niliyosoma hapa na sehemu nyingine ni wazi Sheikh Karume alijiunga katika muungano kutokana na wasiwasi wa serikali aliyoipindua kuweza kurejea tena Zanzibari na kumshambulia, vilevile hakuwaamini Umma Party. Njia pekee ya kuimarisha usalama ni kujiunga Muungano na majeshi ya Tanganyika yalienda Zanzibari kuimarisha ulinzi.

Mwl.Nyerere alijitoa sana katika Muungano kwa lengo wazi ambalo daima Afrika na Dunia ilijua dhamira yake ya kutaka umoja na mtengamano Barani Afrika. Lakini Sheikh Karume alikuwa na malengo tofauti na dhamira kisasi dhulma, hujuma kwa waarabu utumwa wa ndoa na kutawala bila kufanya uchaguzi kwa miaka 50. yaani 1964 hadi 2014, nani anaweza tabiri huenda Mungu angembakiza yangetokea machafuko makubwa.

NANI ALIMUUA SHEIKH KARUME?
Nikirejea mipango ya kuuawa kwa Sheikh Karume, hasa majukumu waliyopewa kundi lililokuwa Zanzibari kujipanga kwa kuiba silaha na baadae kuwa katika wakati mgumu baada kundi lililokuwa Dar es Salaam kushindwa kutimiza majukumu yao.
Kwa mipango iliyokuwepo awali ni dhairi lengo kuu ilikuwa kuipindua serikali ya Sheikh Karume na sio kumuua, ikiwa mpango wa kupindua ulishindikana kwa nini mauaji ya Sheikh Karume?
Ndio kusema wengi wao hasa waliokuwa na jukumu la kutekeleza upinduaji wa serikali ya Sheikh Karume walikuwa na kisasi mioyoni mwao (kutbarek bin kisasi). Kwa sababu waliamini uhai wao upo kulipiza kisasi hawakujali lile litakalowakuta hata baada ya kutekeleza hazma yao.

Kumbuka kundi lililokuwepo Zanzibar walianza kuchunguzwa na kutafutwa hasa baada ya kugundulika upotevu wa silaha hivyo basi wangeacha kufanya lolote wangeuawa au wangejaribu kutoroka wangekamatwa na baadae kuuawa kama kina Abdallah Kassim Hanga. Hivyo mauaji ya Sheikh Karume yalifanywa na watu waliokuwa na msukumo, wasiwasi wa dhahama baada ya jaribio lao kushindwa. Na mwenye hasira dhidi ya Sheikh Karume ni dhairi alijitolea KUFA kulipiza kisasi cha kifo cha BABA YAKE.

Hitimisho, Abdulraham Babu alikuwa na nia ya kupindua lakini alishindwa na kukatisha safari yake ya Zanzibari. Katika mazingira haya Mwl.Nyerere hakuhusika na mipango yoyote ya kumuua Sheikh Karume lakini kwa kero na usumbufu wake hata kama aliambiwa MZEE kuna hili jambo linaendelea huendwa alijibu SAWA. Kuona jambo linaelekea kutendeka pasina ushiriki wako ukalinyamazia ni sawa na kulibariki au kuridhia"asukumalatu ridhaa".
Kwahiyo Sheikh Karume aliuawa na watu waliokuwa na chuki naye, kwa kuwa aliwaudhi watu wengi ni dhairi kifo chake kilikuwa ni furaha, au kilitoa ahueni na kubadilisha upepo wa kisiasa.

hapa kama kuna aina ya ukweli japo sina hakika sana
 
Acheni kuishi kwa misingi ya Propaganda
wewe ni kupinga kila kitu na kuficha hoja zako
ziweke hapa bayana tuzichambue
wengine tumeishi na hao waarabu, tumetembelea Museum za hapo Zanzibar na tunajua chuki za Hizbu, Shiraz na wakulima & wakwezi\leta hoja zako usipinge mara tunaropoka mara propaganda
ni vizuri Historia iandikwe upya
 
Tatizo la kwanza mkuu unaleta mambo ya waarabu. Hivi kuna sehemu mimi nilimtaja muarabu? mbona unachngaya mambo? mada ni Okello sasa mnatoka mnaleta story za Sultan na Muarabu. Tumzungumze huyo Okello ili tufahamiane.
 
Na mkuu story za zakuahadithiwa museum ndio hizo nilizosema propaganda zenyewe. Mnadanganywa tu mule.
 
Tatizo la kwanza mkuu unaleta mambo ya waarabu. Hivi kuna sehemu mimi nilimtaja muarabu? mbona unachngaya mambo? mada ni Okello sasa mnatoka mnaleta story za Sultan na Muarabu. Tumzungumze huyo Okello ili tufahamiane.
Ok hii Mada ni ya Karume na si Okello
Okello aliyeongoza mapinduzi aliuawa na Idd Amini
kwa vile una habari nzuri ya kuirekebisha hii Historia ya Karume na Okello ungetuwekea
maana nijuavyo waarabu wote hawayakubali Mapinduzi wanaona km Kisiwa ni cha Sultan Sayyid
ndio maana tukiwaeleza chimbuko la Kifo cha Karume wanahemuka
Tunakusikiliza Mkuu maana toka mwanzo hujatanabaisha chochote
 
Sheria ya siri ni miaka 50, hivyo subiri 2021 zitafunguliwa. Kuanzi baada ya Desember 9 mwaka huu, siri za uhuru na serikali ya Tanganyika zitamwagwa hadharani.
Sifikiri kama siri kwenye suala hili zitatolewa. Wakizitoa si ndio itakuja kuwa aibu na uhasama baina ya pande mbili?

Lisemwalo lipo....

Nasikia Mzee Karume alipoanza kusema Muungano mwisho chumbe/muungano ni kama koti basi ndio ikawa sababu ya kumshuhulikia....
 
maana nijuavyo waarabu wote hawayakubali Mapinduzi wanaona km Kisiwa ni cha Sultan Sayyid
ndio maana tukiwaeleza chimbuko la Kifo cha Karume wanahemuka
Sio waarabu, majority ya wazanzibari baada ya kuijua historia ya kweli mapinduzi hawayakubali, na hakuna anaesema kuwa kisiwa ni cha sultan. Uhuru wa Zanzibar ulipatikana 1963 kutoka kwa mkoloni muingereza.

Halafu ndio kwanza nikusikie weye kuwa waarabu wanahemuka wakisikia habari za kifo cha Karume, habari hawana mkuu. Wameyasahau tayari. Kabla ya kupinduliwa Zanzibar iliheshimika, baada ya mapinduzi zanzibar imedharaulika. Sasa wahemuka kwanini zaid ya kutucheka tu?
 
Hivi wenyeji hasa wa Zanzibar ni watu wa jamii/kabila gani?

Mkuu Zanzibar wote kiasili ni wahamiaji, Kama ilivo kwa Tanzania Bara pia. Anapotokea mtu kujinasibu kuwa yeye mwneyeji wa asili wa Tanzania ni muongo tu. Kila kabila ukilipekua halina hata miaka mia 500 katika eneo la Tanzania Bara.
 
Sio waarabu, majority ya wazanzibari baada ya kuijua historia ya kweli mapinduzi hawayakubali, na hakuna anaesema kuwa kisiwa ni cha sultan. Uhuru wa Zanzibar ulipatikana 1963 kutoka kwa mkoloni muingereza.

Halafu ndio kwanza nikusikie weye kuwa waarabu wanahemuka wakisikia habari za kifo cha Karume, habari hawana mkuu. Wameyasahau tayari. Kabla ya kupinduliwa Zanzibar iliheshimika, baada ya mapinduzi zanzibar imedharaulika. Sasa wahemuka kwanini zaid ya kutucheka tu?

Mkuu hawa hakifahamu hata wanachokizungumza. Tatizo kubwa la kubeba propaganda bila kuufahamu ukweli kiuhalisia.
 
Ok hii Mada ni ya Karume na si Okello
Okello aliyeongoza mapinduzi aliuawa na Idd Amini
kwa vile una habari nzuri ya kuirekebisha hii Historia ya Karume na Okello ungetuwekea
maana nijuavyo waarabu wote hawayakubali Mapinduzi wanaona km Kisiwa ni cha Sultan Sayyid
ndio maana tukiwaeleza chimbuko la Kifo cha Karume wanahemuka
Tunakusikiliza Mkuu maana toka mwanzo hujatanabaisha chochote

Kuna baadhi ya watu wanajaribu kuwaaminisha watu kuwa Mapinduzi ya Zanzibar yalifanywa na Okello. huku wakitumia kitabu alichokiandika yeye mwenyewe okello na hizo picha chache zilizopo juu hapo kama ndio reference kuu.
Na kuna na wengine wanaamisha watu kuwa mapinduzi ya Zanzibar yalifanywa na Karume. Hawa wao wanakosa mashiko ya aina yoyote kabisa. Hawana refrence zozote bali tu watulazimisha tuamini wanavosema. (Nahuo ndio msimamo wa Serekali zote mbili za SMZ na SMT)
Wapo wengine wanaosema kuwa mapinduzi ya Zanzibar yalifanywa na Umma Party. (Kama umeptia historia vizuri utakuwa unawafahamu)
Na kuna na wengine wanasema mapinduzi yamefanywa na Nyerere.

Mkuu yote haya umeshayasikia au kuna geni?
 
Nashukuru kwa elimu hiyo.
Lengo langu lilikuwa kujua kati ya jamii za kibantu na kiarabu ipi ilianza kuingia Zanzibar?

Jamii ya kibantu ilikuwepo mwanzo, ikaja ikatawaliwa na mreno, wareno wakaja kuondolewa na waarabu wa oman (hawa waliitwa na wenyeji).
 
Kuna baadhi ya watu wanajaribu kuwaaminisha watu kuwa Mapinduzi ya Zanzibar yalifanywa na Okello. huku wakitumia kitabu alichokiandika yeye mwenyewe okello na hizo picha chache zilizopo juu hapo kama ndio reference kuu.
Na kuna na wengine wanaamisha watu kuwa mapinduzi ya Zanzibar yalifanywa na Karume. Hawa wao wanakosa mashiko ya aina yoyote kabisa. Hawana refrence zozote bali tu watulazimisha tuamini wanavosema. (Nahuo ndio msimamo wa Serekali zote mbili za SMZ na SMT)
Wapo wengine wanaosema kuwa mapinduzi ya Zanzibar yalifanywa na Umma Party. (Kama umeptia historia vizuri utakuwa unawafahamu)
Na kuna na wengine wanasema mapinduzi yamefanywa na Nyerere.

Mkuu yote haya umeshayasikia au kuna geni?
Yote nimeyasikia na ya kwako naongezea katika Elimu ya mapinduzi ila jazia jazia Mkuu
 
Jamii ya kibantu ilikuwepo mwanzo, ikaja ikatawaliwa na mreno, wareno wakaja kuondolewa na waarabu wa oman (hawa waliitwa na wenyeji).
upo sahihi lakini wenyeji walipotaka kumuondoa muarabu wa Oman wakashindwa, kwa nini walimuita Muingereza akaja kupiga vita ya dk 20 na kumuweka mtu wake toka Oman
na kwanini wenyeji waliamua wenyewe Jamuari 12 kujichukulia hatua mkononi kufanya mapinduzi wengine hawakuyakubali?
Je una habari hata ya Marehemu Karume yalikuwa yawe Mapinduzi? na mpaka leo kuna ombwe mbili bado ?
 
Napata kitu hapa.
Hayo maneno uliyo_bold ulimaanisha nini?
Hao wakazi Wa visiwa, waliwaita waje kuwasaidia kuwaondoa wareno, kwa vile wao (walioitwa) walifanikiwa kuwaondoa wareno kwao.
 
upo sahihi lakini wenyeji walipotaka kumuondoa muarabu wa Oman wakashindwa, kwa nini walimuita Muingereza akaja kupiga vita ya dk 20 na kumuweka mtu wake toka Oman

Mimi nakushauri tu, rudia tena kusoma historia ndugu yangu mana ili ulichoandika ni dhahir shahir kuwa kumbe huijui hii habari au wamekulisha uongo waliokufundisha.

Wenyeji wametaka kumuondoa muarabu wa oman, halafu wakamwita muingereza akaja akapiga vita halafu wakamueka tena mu Oman? hujaona contradiction kweli katika ulichoandika? Wametaka kumuondoa mu oman ili awekwe mu oman?

Anyways, hii incident iko well known and it is very clear. Hii haikuwa vita baina ya Wazanzibar na waoman, hii ilikuwa vita baina ya ndugu wenyewe katika ufalme wakitaka kupinduana.

na kwanini wenyeji waliamua wenyewe Jamuari 12 kujichukulia hatua mkononi kufanya mapinduzi wengine hawakuyakubali?
Wenyeji kama wapi? Utawala wa kisultan unajua umetawala miaka mingapi Zanzibar? hao unaowasikia kuwa ndio wanajisifia mapinduzi wao wenyewe wakuja tu. ni vugvugu la watu wachache tu na hata wenyeji hawakutegemea. Mapinduzi yalobarikiwa na wenyeji huwezi kutumia nguvu kuwatuliza watu na wala huwezi kuwa na khofu juu ya unaowaongoza.

By the way, ulishawahi kuisikia story jamaa alisema kuwa zanzibar hakuna ata chumvi akapelkwa kwa Karume akalishwa polo zima la chumvi? Zanzibar kulikua na njaa kisawasawa, ulikuwa utawala wa kidikteta.

Je una habari hata ya Marehemu Karume yalikuwa yawe Mapinduzi? na mpaka leo kuna ombwe mbili bado ?

Hapa, correct me if i am wrong, umemaanisha kuwa mauaji ya karume ni mapinduzi, kama sivo nlivofahamu utanielewesha.

Mapinduzi yaliofanywa na Nyerere baada ya Karume kuanza kuhoji Muungano. Connect the dots, Mzee Jumbe nae alipoanza harakati za kujitoa kwenye Muungano, Maalim Seif akenda kwa Nyerere, Nyerere kusikia, Jumbe kaekwa pembeni na akamfungia Kigamboni!
 
Mambo mengi ya kihistoria yamefichwa sana hadi leo imebaki kuwa ni siri
 
Hapa, correct me if i am wrong, umemaanisha kuwa mauaji ya karume ni mapinduzi, kama sivo nlivofahamu utanielewesha.

Mapinduzi yaliofanywa na Nyerere baada ya Karume kuanza kuhoji Muungano. Connect the dots, Mzee Jumbe nae alipoanza harakati za kujitoa kwenye Muungano, Maalim Seif akenda kwa Nyerere, Nyerere kusikia, Jumbe kaekwa pembeni na akamfungia Kigamboni!

Mkuu hapo kidogo, mbona statement yako imekaa vibaya ? Kwanini umtaje Maalim Seif tu? kwani alikua peke yake? Mbona humtaji na Salmin Amour? kwanini humtaji Salim Ahmed Sailm? Ilikua ni team iliofanya hivyo simtu mmoja. Ni kundi la wanasiasa wasomi vijana. Kwanini siku zote mnakua mnamzungumza Maalim Seif tu kwenye hili?
 
Back
Top Bottom