Mauaji ya Sheikh Karume ni halali kwa kiasi kikubwa sababu hakutaka kuimarisha umoja ndani ya taifa lake na badala yake alijenga jamii yenye mifarakano hasa kwa wafuasi wa ZPPP na Hizbu. Kuwafukuza kazi na wengine kuwataka watoke warudi kwao mwaka 1964 waarabu walioingia Zanzibari karne ya 11 yaani mwaka 1100's. Baada ya mapinduzi watu wenye asili ya kiarabu walinyang'anywa mali na vitu vyao walivyokuwanavyo kwa zaidi ya miaka 500. HUU ULIKUWA NI UKATIRI WA HALI YA JUU hata kama kweli au kwa kiasi fulani walipata vitu hivyo kwa unyonyaji Zanzibari ni nyumbani kwao hawana sehemu nyingine.
Hujuma ndani ya ASP dhidi ya viongozi aliowaona kuwa na ushawishi kuweza kuhatarisha utawala wake kuwaua, kuwatesa, kuwafunga jela, kuwafukuza Zanzibari kwa kuwateua kuwa Mabalozi, Mawaziri serikali ya Muungano. Hiyo ilijenga chuki kubwa baina yake na mavamizi wenzake, TAYARI AMEJENGA MAADUI WAWILI.
MUUNGANO wa Tanganyika na Zanzibari, kupitia historia na miaka niliyosoma hapa na sehemu nyingine ni wazi Sheikh Karume alijiunga katika muungano kutokana na wasiwasi wa serikali aliyoipindua kuweza kurejea tena Zanzibari na kumshambulia, vilevile hakuwaamini Umma Party. Njia pekee ya kuimarisha usalama ni kujiunga Muungano na majeshi ya Tanganyika yalienda Zanzibari kuimarisha ulinzi.
Mwl.Nyerere alijitoa sana katika Muungano kwa lengo wazi ambalo daima Afrika na Dunia ilijua dhamira yake ya kutaka umoja na mtengamano Barani Afrika. Lakini Sheikh Karume alikuwa na malengo tofauti na dhamira kisasi dhulma, hujuma kwa waarabu utumwa wa ndoa na kutawala bila kufanya uchaguzi kwa miaka 50. yaani 1964 hadi 2014, nani anaweza tabiri huenda Mungu angembakiza yangetokea machafuko makubwa.
NANI ALIMUUA SHEIKH KARUME?
Nikirejea mipango ya kuuawa kwa Sheikh Karume, hasa majukumu waliyopewa kundi lililokuwa Zanzibari kujipanga kwa kuiba silaha na baadae kuwa katika wakati mgumu baada kundi lililokuwa Dar es Salaam kushindwa kutimiza majukumu yao.
Kwa mipango iliyokuwepo awali ni dhairi lengo kuu ilikuwa kuipindua serikali ya Sheikh Karume na sio kumuua, ikiwa mpango wa kupindua ulishindikana kwa nini mauaji ya Sheikh Karume?
Ndio kusema wengi wao hasa waliokuwa na jukumu la kutekeleza upinduaji wa serikali ya Sheikh Karume walikuwa na kisasi mioyoni mwao (kutbarek bin kisasi). Kwa sababu waliamini uhai wao upo kulipiza kisasi hawakujali lile litakalowakuta hata baada ya kutekeleza hazma yao.
Kumbuka kundi lililokuwepo Zanzibar walianza kuchunguzwa na kutafutwa hasa baada ya kugundulika upotevu wa silaha hivyo basi wangeacha kufanya lolote wangeuawa au wangejaribu kutoroka wangekamatwa na baadae kuuawa kama kina Abdallah Kassim Hanga. Hivyo mauaji ya Sheikh Karume yalifanywa na watu waliokuwa na msukumo, wasiwasi wa dhahama baada ya jaribio lao kushindwa. Na mwenye hasira dhidi ya Sheikh Karume ni dhairi alijitolea KUFA kulipiza kisasi cha kifo cha BABA YAKE.
Hitimisho, Abdulraham Babu alikuwa na nia ya kupindua lakini alishindwa na kukatisha safari yake ya Zanzibari. Katika mazingira haya Mwl.Nyerere hakuhusika na mipango yoyote ya kumuua Sheikh Karume lakini kwa kero na usumbufu wake hata kama aliambiwa MZEE kuna hili jambo linaendelea huendwa alijibu SAWA. Kuona jambo linaelekea kutendeka pasina ushiriki wako ukalinyamazia ni sawa na kulibariki au kuridhia"asukumalatu ridhaa".
Kwahiyo Sheikh Karume aliuawa na watu waliokuwa na chuki naye, kwa kuwa aliwaudhi watu wengi ni dhairi kifo chake kilikuwa ni furaha, au kilitoa ahueni na kubadilisha upepo wa kisiasa.