Mauaji ya Mzee Karume: Acha sasa tuhoji yasiyohojika!


Mkuu hapo naona unajichanganya. Vita vya dakika 20 unavifahamu vizuri source yake?
 
Jamii ya kibantu ilikuwepo mwanzo, ikaja ikatawaliwa na mreno, wareno wakaja kuondolewa na waarabu wa oman (hawa waliitwa na wenyeji).

Kumbe hata wale waliofanya Mapinduzi ya 1964 walikuwa wakuja tu!
Wale Wabantu waliokutwa na Mwarabu sijui hata waliishia wapi!

Mkuu kabla ya huyo muarabu mnaemsema Hakukua na jamii ya kibantu tu kama mnavozungmza au mnavoamani.

Mumewahi isikia Sultanate of Kilwa au Kilwa Empire? mumewah kumsikia mtu alieitwa Ali ibn al-Hassan Shirazi, ambaye ndie alikua founder wa Kilwa Empire?

Wakuu historia ya kweli sio hii tunayosomeshwa tuliotengenezewa na Tanu.
 
Yote nimeyasikia na ya kwako naongezea katika Elimu ya mapinduzi ila jazia jazia Mkuu

Mkuu mapinduzi sio kitu cha misahira kama tunavoaminishwa, Kwa mujibu wa tunavoaminishwa au kusomeshwa basi mapinduzi ya Zanzibar yalikua ni kitu chepesi sana, Eti wakwezi na wakulima. Suala la Mamlaka ya nchi inayotambulikana Duniani mpaka ndani ya UN watoke wakwezi wafanye mapinduzi halafu wachukue serekali hivi linaingia akilini hilo katika hali ya kawaida?

Mbona Jeshi la Tanganyika lilishindwa kufanya mapinduzi 64? tena wakati tayari kila kitu walishakaribia kukieka under-control mjini? na nyerere aliashakimbia na kujificha kabisa waweze wakwezi?

Baada ya vita Vya kwanza na Baadae vita vya pili vya Dunia, dunia nzima tayari ilikwishakua chini ya under control ya mzungu. (US/UK/Russia). Hakuna utawala wowote Duniani unaosimama bila ya kukosa support ya either U.S/U.K au Russia lakwanza fahamu hilo mkuu. Wazungu walipoondoka Afrika walihakikisha nchi zote zipo chini ya mikono ya watu wanaowataka wao. na kama mazingira ya harakati za uhuru hayakawapa nafasi yakuwaachia wanaowataka basi Uhuru haukudumu lazima kulitokea mapinduzi yakuondoshwa serekali.
Mkuu yaliotokea Zanzibar pia yametokea D.R.C kisa cha lumumba unakifahamu naamini, Pia Yametokea Burundi, Nasehemu nyengine Barani Afrika fatilia historia ya Bara La Afrika utaona vizuri sana. Hata Iddi Amini aliekwa madarakani na Muengereza na Pia akaondoshwa na Muengereza baada ya kukosana nao. Hizo nyengine zote hua ni vijisababu vya kutengenezwa tu nyuma ya pazia.
Wengi wetu tunaamini aliyofanyiwa Lumumba ni ukatili na tunawanyooshea vidole wazungu kwa Ubaya wao. Lakini kwa suala la Zanzibar tunyafumbia macho huku sababu tu kuwa tumejaza propaganda za kutengenezewa ndani ya vifua vyetu.

Mpako hapo tunakwenda vizuri mkuu?
sorry nipo too tight kwahiyo nakosa nafasi ya kutosha ya kuchangia hii mada nzuri, hata ninapost nakua ninaharaka sana.
 

Umeuliza vizuri sana mkuu. Swali lakwanza linaanzia hapa. Kuna Uthibitisho wa uwepo wa Waarabu Zanzibar hata zaidi ya miaka elfu moja nyuma. kwa mujibu wa maelezo ya historia mbalimbali pamoja na vitabu vya historia.

Lakini je uthibitisho wa uwepo au ujiowa Wabantu Zanzibar una ushahidi gani? Je unaweza leta data zozote au umewahi kusikia zinazoonesha kama kulikua na Wabantu Zanzibar miaka 1200 nyuma?
Je pia umewahi sikua au kujua ni makabila gani ya kibantu ambayo yalikuawepo asili Zanzibar?

haya maswali yanakosa majibu mkuu.
hao wanoitwa wao ndio wenyeji wa Zanzibar wao wanajiita ni washirazi. Washirazi mkuu ni Wapersia+ Arabs na historia yao ipo wazi kabisa.
Wengine wanasema Kuna jamii ya Watu wanaitwa Wahadimu ndio wenyeji. Hao wahadimu mkuu kiasili ni watumishi au Watumwa walioletwa Zanzibar kutoka Bara. Na wanapatikanwa mkoa wa kusini Unguja. Historia yao ipo wazi kabisa wala haina chenga kabisa. hawa hawafiki hata miaka mia 3 ndani ya Zanzibar. Na mimi nimeshakutana nao achilia mbali kuwasoma vitabuni asili zao wanazifahamu kabisa.
Na kuna wanosema Asili ya Watu wazanzibar ni wahamizi kutoka Tanzania Bara huku wakinasibishwa na Makabila ya Kitanga na Pwani kua ndio wenyeji. Lakushangaza ni kuwa Historia ipo wazi kabisa kuwa Zanzibar kuna watu wanaishi tokea hata hayo makabila wanayoyataja kina Wazaramu na wenzao hayapo kabisa kwenye eneo la Tanzania.

Mkuu tunakwenda sawa mpaka hapo?
 
labda nikueleze kwa kifupi tu kuwa Zanzibar ilivamiwa na wageni, wakiwemo Wachina, washiraz na wengineo na walikuja kufanya biashara za shanga viungo vya chakula, vyombo vya udongo nk kwa kubadilishana na
vitu kutoka hapo visiawani na Bara hadi Congo
Hawa wageni walikuwepo miaka zaidi ya 2000 (yaani kabla ya Kristo) sasa walipokuwa wanaabiri huo Pwani kuanzia Mogadishu Kilwa hadi Sofala ndipo wakasema wamevumbua na akafuata Mreno
ni kutokana na Wikipedia yako hawa watu wakinunua wanajifanya ni kwao wakati wamewakuta wenyeji
N a kwa Zanzibar ni hivyo hivyo waliwakuta wabantu
Labda kabla sijaenda mbali hawa waarabu walipokuwa wakizaa na watumwa wa kike waliwakataa watoto wao na mpaka leo hawaruhusiwi kurithi au kutambulia huko Oman
Na pili hii ndio ikaleta tabaka kubwa na hadi watu kuitana Waarabu koko na waarabu safi wa Oman ambao walileta msemo usemao Punda hapandi Muscat
 

Mkuu wikipedia sio source yakuaminika kwenye kupata taarifa sahihi zakitu. Mimi mwenyewe nimmoja katika wanao add vitu vingi sana kwenye hizo makala zao nafahamu vizuri mazingira yake kichohitajika ni souce tu ya addition yako nasio uhalali wa kiandikwacho. Nimeweka hiyo source link ya huyo mtu alau kwa wasiopata aidia waweza kupata picha kiasi.
Jengine unaweza kutwambia ni wa Bantu wa makabila gani ambao waliokutwa? hilo halisa source mkuu ndio mana nikaeleza kuwa kinachozungumzwa hakina dalili yoyote. Na jengine la kujalizia hao Wapersi walipofika hapa afrika mashariki waliwakuta wa Yemen wakiwa ndio watawala wa ukanda huu nasio wabantu. ingia nadani zaidi mkuu utayaona.
Na mkuu utawanyikaji wa wabantu kutoka Afrika magharibi mpaka kufika kusini na mashariki unajua ulianza kipindi gani? hiyo 2000 years nyuma mkuu maeneo ya Tanzania hakuna mbantu kabisa.
 


Mkuu unarudi kwenye matango pori. Stori za kukaririshwa za Tanu. Ficha chuki zako mkuu, haya mambo hayataki chuki.

Nakuhusu uarabu koko na uarabu safi mkuu tatizo liko wapi? Kwani hakuna Mbantu koko na safi? Hakuna mzungu koko na safi? Hivi Chotara ni nani?

Na kuhusu iyo kesi ya kuzaa. Hata kama tuseme ipo hivo unavosema wewe. Hivi hufahamu taratibu za kiislamu kama mtoto wa nje ya ndoa Hamrithi baba? Hufahamu kama taratibu za kiislamu mtoto wa nje ndoa si mwanao na unaweza kumuo kabisa? masuala ya Imani zao waachie wenyewe. AU na weye nikatika hao Waarabu koko wanaobaguliwa?
 
Ndugu yangu usilishwe Matango pori, na huwezi nifundisha historia ya mwarabu wa Oman mpaka wanagawana utawala mmoja atawale Oman na mwingine Zanzibar
Mpaka Sultani anazaa na Mhabeshi na mwingine kazaa na Mjerumani
Bint Sultani kaolewa Ujerumani na watoto wake ni wajerumani tena Wakristo
na Binti mwingine hakuzaa kabisa akamuachia utawala nduguye
Labda kwa faida ya wengine ni kuwa Sultani sayyed wa Oman alikuwa na watoto wawili Majid na Thuwaini
Thuwain akatawala Oman na Majid akatawala Zanzibar
Vita vya kwanza vya muda mfupi vilitokeaje? baada ya Sultan Thuwain kufariki mtoto wa Barghash (Khalid) ambaye ndiye angerithi Waingereza hawakumpenda wakamtaka ajiuzulu, alikataa hivyo wakapiga Kombora na Jengo moja na kumumbia asalimu la sivyo watamshukia akatii na wakamuweka Hamoud
labda kwa kukusaidia ingia katika lugha za wenzetu usome Utawala huo kutoka Sayyid said mpaka kwa Sultan Jamsheed aliyepinduliwa 1964
List of Sultans of Zanzibar - Wikipedia
Kumradhi tumetoka nje ya MADA YETU (Mauaji ya Mzee Karume acha tuhoji .....) ila nilitaka tu kuweka mambo sawa ninavyoyajua kutokana na kumbukumbu za vitabu na hata pale Majengo ya makumbusho Zanzibar, waarabu kwao ni Omani si Zanzibar wamekuja kwa ajaili ya biashara ya Utumwa FULL STOP
 
View attachment 998406
The Sultan's harem after the bombardment.DateLocationResult
09:02–09:40 EAT (06:02–06:40 UTC), 27 August 1896
(38 minutes)
Zanzibar Town, Zanzibar Sultanate
Imperial British victory

Mkuu vita hivyo vilitokea baada mmoja kati ya warithi wa ufulme kuchukua madaraka kwa nguvu, alifanya hivyo akiamini yeye ndie anaestahiki lakini Waengera tayari walikwisha muandaa mtu wao. Na baada ya kupigwa kwenye vita Alikimbila Tanganyika kwa Wajerumani wakmpa hifadhi.
Hili linatoa picha ya wazi tu kwamba Wafalme walikua wakiendeshwa na Waengereza na hakuna aliyatawala bila kuwa kibaraka kwa Muengereza. Ukitaka kufahamu vvipi Muengereza aliutawala Usultan wa Zanzibar hiyo ni mada nyengine.
 
sasa nimekuelewa Mkuu,km hata Idd Amini aliondolewa na Muingereza hiyo nayo ni Historia mm basi ni FULL STOP ngoja nisikie kutoka kwako, lakini kila mwaka lazima nitembelee Historia ya Zanzibar na kuna Makumbusho zaidi ya 26 nimemeliza matatu tu
History of Zanzibar - Wikipedia
Leta sasa ujuayo nijifunze kuhusu ujio wa Wageni wa Zanzibar ya Wabantu Wahadimu na Watumbatu
 

Mkuu siasa ya dunia kama inakupiga chenga kidogo. Hivi unafikiri Nyerere angekua na Ubavu wakumuondoa Iddi Amini bila ya kuwa na support ya mataifa ya magharibi?
 

Mkuu kwa hoja yako hiyo Hata Wabantu nawao Kwao ni Afrika Magharibi.

Nalabda tungeanzia hapa Biashara ya utumwa Zanzibar ilianza mwaka gani? Na hao waOman wameanza kuja mwaka gani?
 
Sasa huyu alimua Karume alifungwa au alikwenda wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wabantu nawao Kwao ni Afrika Magharibi.
Nalabda tungeanzia hapa Biashara ya utumwa Zanzibar ilianza mwaka gani? Na hao waOman wameanza kuja mwaka gani?
sawa kabisa Wabantu kwao ni Afrika sio Bara Arabu
Waarabu asili yao Bara arabu waarabu ni wafanyabiashara km hapo mwanzo nilivyoelezea, (Historia STD IV) walikuja kwa kutumia pepo za Moonson walipoona vimenoga wakahamisha makao kutoka Oman kuja Afrika (wakidai Kisiwa hicho kilikuwepo kwao kimesogezwa na upepo) wakionesha kilikuwa karibu sana na Madagasca wakati hakijakaribiana na Afrika na wakawakuta wenyeji si waerevu (wabantu na wenzao) wakaanzisha mauaji na mateso, ili kuchukua ardhi kwani wakiwa na tabia ya kumuua ndugu ndipo utawale ardhi, watumwa na vitu vya uliyemuua, waliponogewa wakafanya ni Nchi yao (bora hata wagefanya koloni lao wakabaki Oman)
Traders from Arabia (mostly Yemen), the Persian Gulf region of Iran (especially Shiraz), and west India probably visited Zanzibar as early as the 1st century AD. They used the monsoon winds to sail across the Indian Ocean and landed at the sheltered harbor located on the site of present-day Zanzibar Town. Although the islands had few resources of interest to the traders, they offered a good location from which to make contact and trade with the towns of the Swahili Coast.
Nalabda tungeanzia hapa Biashara ya utumwa Zanzibar ilianza mwaka gani? Na hao waOman wameanza kuja mwaka gani?
nimesema waOman walisogea ili kufanya biashara kwa karibu zaidi wakati huo kuliko huko nyuma
Every year, about 40, 000-50, 000 slaves were taken to Zanzibar.[20] About a third went to work on clove and coconut plantations of Zanzibar and Pemba while the rest were exported to Persia, Arabia, the Ottoman Empire and Egypt.[21] Conditions on the plantations were so harsh that about 30% of the male slaves died every year, thus necessitating the need to import another batch of slaves.[22] The Omani Arabs who ruled Zanzibar had in the words of the American diplomat Donald Petterson a "culture of violence" where brute force was the preferred solution to problems and outlandish cruelty was a virtue.[23] The ruling al-Busaid family was characterized by fratricidal quarrels as it was common for brother to murder brother, and this was typical of the Arab aristocracy, where it was acceptable for family members to murder one another to gain land, wealth, titles and slaves.[24] Visitors to Zanzibar often mentioned the "shocking brutality" which the Arab masters treated their African slaves, who were so cowed into submission that there was never a slave revolt attempted on Zanzibar.[25] The cruelty which the Arab masters treated their black slaves left behind a legacy of hate, which exploded in the revolution of 1964.[26]
yaani km mpaka hapa hutaelewa kuwa Waarabu Kisiwa hicho si chao ila walikuja kwa biashara tu na wakaleta ubabe na mauaji basi una yako
tungerudi kwenye Mada ya Karume
 

Mzungu anatuandikia jinsi waarabu walivokua makatili wa kwa Watumwa. Nivichekesho vikubwa sana.
Swali langu umelikimbia mkuu. Waarabu wamekuja lini na utumwa umekuja lini?
Mnapofeli pakubwa ni hapa. Pale mnapolazimisha kuwa Ujio wa Mfalme wa Oman ndio ujio wa waarabu Zanzibar. Hilo ndilo tatizo lenu kubwa. mkuu waarabu Zanzibar wapo zaidi ya one thousand years na huyo mfalme kaja juzi tu miaka 200 nyuma. Lakini mkianza kuwazungumza waarabu mnamzungumza Sultan. Umewah wasikia winyi wakuu? ambao mnatuminisha eti ndio walikua watawala wakibantu Zanzibar? Wafatilie ndio utajua kama walikua wabantu kweli kama mnavotwambia. Bado umeshindwa kunitajia kabila au jamii yoyote ya wabantu hao munaowaita ndio wenyeji asili wa visiwani na naendelea kusubiria kutoka kwako.

Na Mapinduzi ya Zanzibar hayana uhusiano wowote na Utumwa. 90% ya hao washiriki wa hayo mapinduzi ni either hawakuzaliwa Zanzibar kabisa kwa maana wamekuja wakubwa au Hao waliozaliwa basi wana kizazi kimoja tu. Sasa wao Utumwa umewahusu wapi?
 
Sasa huyu alimua Karume alifungwa au alikwenda wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu karume hakuuliwa kwa kisasi tu kama baadhi wanavosema, Ilikuwa ni revolution atmp. Alie muua alikua na shemegi yake ambaye nae aliuwawa hapohapo eneo la tukio. Na akiitwa Homoud.
Na leader wa hio plan alkua ni BABU. ni stori ndefu tu ila kwa ufupi ni hivo.
 
Hizi Habari za Kifo cha Mzee Karume zinakanganya...kuna sehemu nilisoma bandiko moja linadai kuwa Karume Alikuwa na uhasama na Na upande wa Mke wake ambaye ana asili ya Asia (hajatajwa) na Aliyefyatua risasi iliyochukuwa uhai wake ni Mdogo wake mkewe.(yaani Shemejiye Karume) na chanzo ni kwamba Karume aliwahi kuwatesa Ndugu wa huyo mkewe (wakiwemo wakwe zake ambao walikuwa na asili ya Kiarabu) ....hapa Napata ukakasi wa chanzo cha hicho kifo..labda tuseme Huyo Kept. Hamoud ndiye huyo shemejiye Mzee Karume?
 
Wafatilie ndio utajua kama walikua wabantu kweli kama mnavotwambia. Bado umeshindwa kunitajia kabila au jamii yoyote ya wabantu hao munaowaita ndio wenyeji asili wa visiwani na naendelea kusubiria kutoka kwako.
Mkuu mbona nimeshakujibu katika post # 216
The first permanent residents of Zanzibar seem to have been the ancestors of the Hadimu and Tumbatu, who began arriving from the African Great Lakes mainland around 1000 AD. They had belonged to various Bantu ethnic groups from the mainland,
hawa waHadimu na waTumbatu wametokea Maziwa Makuu (Ziwa Victoria /Nyanza) na wanatokana na jamii ya waBantu kutoka Bara na waliishi katika vijiji vidogo wakashindwa kuungana na kujitawala ndio maana wakavamiwa na wageni
they lived in small villages and failed to coalesce to form larger political units. Because they lacked central organization, they were easily subjugated by outsiders.
kutafsiri kila sentesi si mtaalam ndio maana nikakupa link ambapo inaweza kukutafsiria mbona yote yamo? History of Zanzibar - Wikipedia
View attachment 999165
na nilisema Mwarabu alikuja kama mtu mwema na mfanyabiashara mwaminifu jua huyu jamaa ni kigeugeu haswa fuatilia Saddam Hussein, Osama, Bashir Kashoggy wanageukwa na nani ni Mzungu?
mwenyewe ndiye uliyetaka nitumie Wikipedia zipo search nying tu lakini nilijua utazikataa km hii sasa unaikataa unasema Mzungu kaiandika)
Historia yako ni ile ya kuhadithia kuwa kisiwa hicho kilikuwa kitupu walipokuja waShiraz na wakaanza kutafuta pembe za Ndovu huku bara mpaka Congo wakakutana na Manyani na kuyakata mikia (sisi waafrika ni manayani tuna mikia) na kuwasafirisha, ndio maana nangoja tafsiri ya PUNDA HAPANDI MUSCAT (UANIJUA NA hutajibu asilani)
 

hayo ndio matango yenu pori mliolishwa.

Wahadimu wahawana hata zaidi ya miaka mia 3 ndani ya zanzibar. Wanatokea bara na wamekwenda unguja kwa Biashara ya utumwa.
Neno hadimu linatokana na lugha ya kiarabu lenye tafsiri kama mtumishi. Usiridhike na kakaririshwa. Mimi nishakutana nao tena wazee kabisa, na wanatokea mabara asili zao tena sio hiyo miaka unayoitaja weye. wengi wanapatikanwa maeneo ya kusini unguja kama Makunduchi, Kizimkazi, Paje, Jambiani, Chwaka.
Katika vuguvugu za vyama vya kijamii wengi wao walijiingiza kwenye umoja wa kishirazi. hii ikapelekea baadhi ya watu na hasa wakaskazini Unguja amabao wanajisabu ushirazi kuususia umoja huo wakitoa hoja ya kuwa kuna wasio washirazi wengi wamejiingiza ndani.

Na watumabatu asili yao ni mixture between Washirazi na wa Sudan/Somali/Ethopia ambao ndio watu weusi wa mwanzo kufika zanzibar. nasio kama hivo unavosema weye kabisa. katufute vitabu vya Saleh Farsi vya mtiririko wa historia ya Zanzibar mkuu uengeze ujuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…