Mauaji ya Polisi wetu ni Ujambazi, Ugaidi au Retaliation? Nini kifanyike kukomesha hali hii?

Kisifanyike chochote juzi kuna Wabunge wameomba hilo swala lijadiliwe bungeni kuna wanawake jenista mhagama na mwenzie bila hata aibu wanasema ni uchochezi!
Yakasikika makofi ya Wabunge wa ccm waaaa...waaaa....waaaa....
Acha tuendelee hivi hivi
Ngushi unaongea nini mkuu.

Acha siasa njoo kwenye ubinadamu mkuu
 

Umeongea kwa hisia sana mkuu,,ila kweli ifikie wakati Jeshi la police wafanye kazi kisayansi na kujenga ukaribu na raia,, ila haya matukio inavyonyesha kama Kuna ulipizaji visasi fulani,,,,hapa ndio idara ya usalama wa Taifa inatakiwa wapandikize watu katika ivyo vijiji mkoa wa pwani ili kupata kiini aswa cha haya matukio yote
 
Mkuu;
Hii haipo kokote kati ya hayo ulioyataja. Wala watu wasidhan ati majambazi wamefikia mahali pa kuweza okota/kusanya bunduki nyingi hivyo. Za kazi gani?? Una maana hawana akili ya kujua kuwa wanawatibua jeshi?? Naomba Serekali, iache papara za hasira za kuwatafuta msituni. Sidhani kama wapo huko. Intelijensia yetu itulize vichwa na kulisoma hili somo.
Naamini watatoka na kitu cha kuweza kumaliza kabisa jambo hili na liwe somo kwa wahusika hao waovu. Bado tuna serekali makini Tz.
Nasema, hawa sio magaidi, sio majambazi bali ni watu wenye nia ya kututoa kwenye njia sahihi. Naunga mkono kuwa, kwa sasa nchi sio tulivu.
 
Ni kweli kabisa kuna mambo mengi nyuma ya pazia.ila ukweli utafahamika very soon
 
Kafara za Bashite hizo na njia anazosaka ni kuwasahaulisha watanzania juu ya vyeti vyake pia ameingia gharama kubwa kuwaleta waganga wa kienyeji toka pande nyingi Duniani anahofia akitumbuliwa jipu ni nani atampa pesa za kuwagharamia ikiwemo kuwarejesha kwao.
 

Mkuu;
Naogopa kabisa kuchangia neno hapo kwa sababu unayemtaja aweza hata tokea hapa kwenye hii pc yangu. Nitamjibu nini??
 
Umeongea Pumba tu, na uchochezi wa hali ya juu.
Inaeesekana pia weewe ni mmoja wa wahusika wa hili tukio, ndio unawahi kujikosha mapema kusingizia ugaidi.
Wewe unaujua ugaidi au unausikia redioni tu.
Kama hujui chochote nyamaza kimya, utakapochkuliwa utoe ushahidi wa kusema kuwa una asilimia 100 utasemaje saasa kama na wewe sio muhusika wa tokeo.
Acha upumbavu na ujinga wako huo wa Chuki binafsi, tafuta vitabu usome maana shule haikukusaidia kitu.
 
Askari kama Mtanzania yeyote ana haki ya kujilinda na kama kujilinda huko kunaitaji kuua ili asiuwawe yeye basi anaruhusiwa kuua. Haki ya kujilinda ipo kwenye Katiba ya JMT.
 

Paskali;

Shukrani kwa kufuatilia.

Nimesoma hiyo link; na kimsingi nisingeandika niliyoandika hapa kama sikuisoma hiyo link. In fact ningekuwa reader tu. Ni kweli umeuliza swali na watu wachangie. Bahati mbaya swali lako ni la kimkakati (a strategic question). Ingawa ni swali, platform ulipoliweka hilo swali hasa kwa kulink na thread ya nyuma; tayari ulitaka watu wafahamu hii ni ngoma ya aina gani na tunaenda na mavazi gani kuicheza. Na kimsingi ndicho kilichojitokeza kwa coments za watu humu.

Nimesema thread imekosa uzalendo, kwa maana structure ya swali imeibua mijadala amabyo haiwatendei haki wenyeviti karibu kumi waliouliwa na hawa wahalifu. Imekosa uzalendo pia kwa kutengeneza structure ya swali ambapo mijadala inayoibuka inakatisha tamaa kwa askari walioenda kulinda wananchi na wenyeviti wa vitongoji wasiuliwe na zaidi ya mia.

Ukichanganya thread ya leo na attachement yako, ni dharihi ulitaka wachangiaji wajenge uhasama kati ya serikali (jeshi la polisi) na wananchi.

Najua una uwezo mzuri tu. Kipindi kile ulikuwa unatangaza hoteli za Tanzania na nafikiri hii product ulitengeneza mwenyewe, na pia jinsi ulivyokuwa unaleta coverage za saba saba; basi ina imani ukijichimbia kule kibiti unaweza kuibuka hali halisi.

Shukran
 

Nakubaliana na wewe ndugu. Polisi wetu hawajakaa kiutayari. Hata jinsi wanavyolinda mabenki. Amekaa na bunduki kaweka pajani. Kule kibiti ukipishana nao kwenye gari, wamejikusanya wote wanaangalia mbele. Pia aina ya magari wanaotumia yana chuma kwa juu. Sii rahisi kureact haraka . Kile chuma ni kizuizi. Hata pale kwenye kizuizi, mmoja anazuia na wengine wamejirundika hapo chini ya mti.

Jeshi letu la polisi linapaswa kufanya mapitio ya mkakati wao wa ulizi.
 
Reactions: SDG
Kuna watu huwa wanafuatilia masuala haya ya ugaidi kwenye vyombo vya habari sasa wewe bwege baki kutoa comments za kijnga wakati weledi wako ni kuwaza chai maharage.
kuna msemo usemao never argue with a fool.
 
Vikosi vya ulinzi kipolisi mkoa Wa pwani vibadilishwe haraka sana vimeshindwa kazi au kamanda siro ahamie pwani akakomeshe jambazi huo haiwezekani kila Siku habari watu kuuawa tu
 
Reactions: SDG

Pascal, kuhusiana na <<<Kwa tukio kama la jana,jee mnadhani huu sasa ni wakati muafaka wa kuzibadili sheria zetu za jeshi la polisi ili kuwalinda polisi wetu wawe licenced to kill officially na serikali itangaze rasmi kuwa ujambazi wa kutumia silaha adhabu yake ni kifo cha papo kwa papo, no prosecution no kesi, bali ni hukumu ya kifo there and then ili kuwaogofya kabisa majambazi wote wanaotumia silaha wasithubutu?>>>, bila shaka umesahau kwamba hii iliwahi kujaribiwa hapa nchini na matokeo yake yakawa maafa makubwa.

Utakumbuka Kikwete alipoingia madarakani 2005 alikuja na agenda ya kutokomeza ujambazi; akaanzisha wizara mpya mbali na ile ya mambo ya ndani iliyoitwa Usalama wa Raia na kumteua Harith Bakari Mwapachu kuwa waziri wake.

Moja kati ya mikakati wa Waziri Mwapachu ya kupambana na ujambazi ilikuwa ni kuwapa polisi mamlaka ya kupiga majambazi risasi (shoot and kill) papo kwa papo.

Matokeo ya mkakati huo yalikuwa ni majanga makubwa. Majambazi hayakuguzwa ila makumi ya raia wasio na hatia ndio waliokubwa na sekeseke la "shoot and kill" wakiomo wafanyabiashara wa madini wa Morogoro na taxi driver waliouawa kinyama na polisi katika maeneo ya Ukuta wa Posta, Sinza.

Yaliyoendelea baada ya hapo ikiwa ni pamoja na kuundwa tume ya uchunguzi ya Jaji Kipenka kuchunguza hayo mauaji ni historia. Itoshe tu kukushauri uondoe hilo pendekezo katika bandiko lako.
 
Reactions: SDG
Before granting license to kill to the police we need to assess the degree of honesty, integrity and sense of malice towards our security personnel. Otherwise let them arrest and take the jambazi into the court of law.
 
Reactions: SDG
Ngushi unaongea nini mkuu.

Acha siasa njoo kwenye ubinadamu mkuu
Ni kweli mkuu,ulisikia kauli ya jenista mhagama na Angela kairuki bungeni juzi?
Yaani kujadili kuhusu haya mauaji na utekaji ni uchochezi_?
Unahisi walikuwa sahihi?
Na wakapigiwa makofi kabisa kuungwa mkono.......unafiki wa aina gani huu!
Tukitaka kuteketeza haya maswahibu lazima viongozi waache unafiki....blue iitwe blue sio kuleta unafiki kama walivyofanya juzi!
Kuna yule ally kesi wanasema Roma angeuawa kabisa na anapigiwa makofi!
Halafu kwenye mambo kama haya eti tuwe pamoja......
 
Ni majambazi, neno gaidi tafsiri yake nini?
Gaidi ni mtu anaefanya vitendo vya kuvunja sheria ili kufikia malengo ya kisiasa. Hii inaweza kusababishwa na Imani za kisiasa ama kidini. Jambazi ni mtu anaeiba kwa kutumia nguvu. Kwa nini nasema hao sio majambazi, majambazi mara nyingi hununua silaha duniani kote, hawana ujasiri wa kuvamia kituo cha polisi kikubwa kama Sitaki Shari na kuua askari na kupora silaha. Psychological tu majambazi wanaogopa polisi na magereza. Hata ukiwauliza askari waliosomea hiyo kazi watakuambia hakuna jambazi ana ujasiri huo. Labda gaidi kwa sababu amejitoa kufa kwasbb ya imani flani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…