Mauaji ya Polisi wetu ni Ujambazi, Ugaidi au Retaliation? Nini kifanyike kukomesha hali hii?

Mauaji ya Polisi wetu ni Ujambazi, Ugaidi au Retaliation? Nini kifanyike kukomesha hali hii?

Bashite Daud a.k.a Maliyamungu sasa yupo busy kuhakikisha kuwa anatengeneza skendo mfulukulizo mpaka watu wamsahau kabsa yupo tayari kuwatoa kafara hata viongozi wakubwa ili mladi abakie kuwa RC mpaka siku magufuli anatoka madarakani.
 
Kisifanyike chochote juzi kuna Wabunge wameomba hilo swala lijadiliwe bungeni kuna wanawake jenista mhagama na mwenzie bila hata aibu wanasema ni uchochezi!
Yakasikika makofi ya Wabunge wa ccm waaaa...waaaa....waaaa....
Acha tuendelee hivi hivi
Hatuwez jadili upuuz ka huo kwan walio kufa si sawa na walio kufa mto ruvu? Tujadili mambo makubwa ya nchi kama kuipiga mkwara korea kaskazin, kua taifa kubwa kuzid UsA, kufika mwezin na mambo mengine makubwa tu, hayo madogo tuwaachie wanawake tu.hao wamekufa kama wengine tu ndo walipangiwa kama wale wa mto ruvu kua siku imefika .labda kuwaombea tu waumzike salama. Kwana huja wah fiwa ww? Mwangos kwan yy hakufa na akazikwa na tuka sahau?,nikitu cha kawaida tu. Hata iweje tutakufa tu ikifika siku.
 
Kuna ile alisema majambazi walazwe chini badala ya kusema wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo husika.

Sasa naona majambazi wameamua ku-retaliate..ndo wanawalaza askari chini sasa. Inabidi kwa kweli kiongozi wa nchi apime kauli zake maana........
Tatizo linaazia juu. Watunga sheria wakivunja sheria huku chini linakuwa somo.
 
Lessons to be learnt, kwa muda mrefu utulivu wa watanzania umechukuliwa for granted.
juzi wabunge wa CCM wamewekwa kitimoto kukatazwa kuongelea Ugaidi na utekaji matokeo yake ndiyo hayo na huenda Bashite akatumia nafasi hiyo kuwakamata watu wengi kwa maksudi ya kuwakomoa kisha watawabbikia kesi kibao feki, ni mda wa Bashite kuwakomoa Wapinzani sasa.
 
Awali ya yote natoa pole kwa Familia ambazo zimepoteza Ndugu,jamaa, na hata Marafiki. Tukio hili limenishtua sana kila mtanzania mwenye mapenzi mema na nchi hii atakuwa ameguswa kwa namna moja au nyingine japo kuna watu vichwa vibovu kiukweli wanasikitisha na kushangaza kabisa namna wanavyocomment,! Hawa Polisi ni Ndugu zetu,Majirani zetu na hata Rafiki zetu. Jeshi la Polisi sasa liache kucheka na majambazi, wafuate maelekezo ya Mkuu nategemea kusikia vifo vingi vya Majambazi kuanzia sasa, Majambazi si Wa kupeleka mahakamani maana kule tunajua, watu hutishiwa kutoa ushahidi kwa kuhofia maisha yao matokeo yake yanarudi mtaani yakidunda.,, hapa kikubwa ni kuyaua tu ikiwezekana hata hadharani .. Hapa hautosikia haki za binadamu wakijitokeza kusemea hili la Jana.

Jambazi hastahili kuishi anastahili kufa......
Simpaka uwaone kaka, hawa jamaa wanaishi na raia kitaa kama watu wengine tu. Wananetwork hatari sana. Serikali ikae na wenyeji wa maeneo hayo wawaambie shida iko wapi?

Wanatatizika mwenye jambo gani ili serikali iweke mazingira mazuri nanwapate info kutoka kwa raia wema. Kwa hali ilivyo unaweza kuitisha mkutano wakijiji watu wakija wasichangie chochote kwani wanaogopa akisema jua likizama anakula za kichwa.

Mahusiano yanatakiwa kwa uakaribu mno na wasitumie wageni wa maeneo hayo. Watumie wenyeji. Wageni nirahisi kushtukiwa na kupigwa za kichwa.

Wanaweza kupeleka askari kama raia wakaanzisha makazi huko, wakafungua biashara kama zakuchaji simu, kuuza maji, hardwares na hata wakulima. Wakae na wazoeane na watu kindakindaki, ikiwezekana kuoa na kuoeleana kabisa.

Hapo wanaweza ku tress mambo mengi sana. Mbona zamani haya mambo yaliwezekana? Leo kuna nini?
 
Madhara ya kuwa licenced to kill kwa polisi ni makubwa sana pascal hasa kwa askari wetu. Haya mambo yatasababisha watu kubambikiwa kesi na kuuawa. Hakuta kuwa na kutekwa tena. Watakuwa wanaua na kumwekea mhusika bastola au bunduki with simple explaination that the man was armed.
Kwa siasa zetu za chuki na ufisadi miongoni mwa polisi watu weng watauawa. But inaruhusiwa kuua wakat wa mapambano.... Ila si kuwa kila mtu aonekanaye kinyume nao wamuue kwa kuwa wameruhusiwa.




Wanabodi,
Taifa bado liko kwenye shock ya nini haswa kilichotokea kwa askari wetu?.

Mauaji haya ya Polisi Wetu ni Ujambazi tuu, ni Ugaidi au Retaliation?. Wakati vyombo vya uchunguzi vikiendelea na kazi yake, Sisi Watanzania kama taifa lazima tujiulize, Nini Kifanyike Kukomesha Hali Hii?,

Kwanza nikiri nimesikitishwa na vifo hivi vya vijana wetu askari polisi kushambuliwa na kuuwawa na majambazi wenye silaha.

Swali ni jee huu ni ujambazi tuu wa kawaida, uvamizi kwa lengo la kuiba silaha, ni ugaidi, ambush au nini haswa?.

Hili kuwaweka polisi wetu kwenye risk na kuwa an easy target, kwa majambazi wanaotumia silaha, niliwahi kulizungumza hapa kwa kirefu Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?
Kwa tukio kama la jana,jee mnadhani huu sasa ni wakati muafaka wa kuzibadili sheria zetu za jeshi la polisi ili kuwalinda polisi wetu wawe licenced to kill officially na serikali itangaze rasmi kuwa ujambazi wa kutumia silaha adhabu yake ni kifo cha papo kwa papo, no prosecution no kesi, bali ni hukumu ya kifo there and then ili kuwaogofya kabisa majambazi wote wanaotumia silaha wasithubutu?!.

Kama ni ugaidi au retaliation, tufanye nini?.

Natoa pole kwa rais wetu wa JMT, waziri wa Mambo ya Ndani, IGP na familia za askari hao!

RIP Askari Wetu.
Nini Kifanyike? .
Ijumaa Kuu Chungu!.
Paskali
Update 1.

Thanks very objective.

Paskali
Update 2 ya michango very objective

Thanks kwa mchango huu, very objective
Paskali
Update 3.
Huu ni mchango very objective

Thanks for this.
Paskali
 
ukiwa maeneo ya jaribu ,kibiti,ikwiriri wao wanadai hawa jamaa wanadai kuna wenzao wamekatwa na wanateseka gerezani,ifike wakati serikali ikae nao mezani .Mbona mkuu aliyepita alimshauri Kagame akae na wale wa rwanda ,ni wakati muafaka wa kumshauri Dereva wa roli akaei pembeni na kuwasikiliza abiria kwani wanataka kuchimba dawa.
Wakazi wa huko wanafai Polisi wamekuwa wakiwatesa sana, wanawadhalilisha kwa kuwabambikia kesi, kuwapekua pekua bila sachi warant, kuna uonevu mwingi sana upo kimya kimya ndiyo maana wamechoka wakaamua kuwaonyesha kuwa na wao wana uwezo mkubwa wa kuwakabili na hiyo ni msg japo kuna tetesi kuwa Bashite kapitishia kafara lake humo humo
 
Hadi pale Waislam watakapoacha kutetea magaidi, kuyasifu na kuyapa hifadhi. Hadi pale waislam watakapoanza kukemea ugaidi kwenye mihadhara na kila sehemu. Hadi pale waislam watakapoanzisha kampeni ya kuwakana magaidi kutoka katika miongoni mwao. Hadi pale magaidi watakapokoma kuwa sehemu ya waislam. Hadi pale Magnidi watakapokomeshwa kujibainisha kwamba wanafanya ugaidi kwa jina la allah.

Kinyume cha pale sahau!
Hahhahahaha, haya bwana kamateni basi hao waislamu. Mauwaji yataendelea au yatakoma. Ukiitenga jamii moja na kuikandamiza ukidhani ndio sulihisho unakosea sana.
 
Haya ni ya kufikirisha. Hivi yalikuwapo toka zamani au ni wakati huu ambao watu wengi wana hasira na ukata? Wanachi wanalia na kukata tamaa, vitu vyapanda bei wakati pesa haipo. Inawezekana kweli kila mtu alikuwa mpiga dili hata huku uchochoroni? HAPANA.
Ujambazi huu wa kuua walinzi wetu na kuchukua silaha zao si jambo la kuangalia tu hivi hivi laziama INTELIJENSIA ya kipolisi itumike kuzidi ile watumiayo kuzuia mikutano ya wanasiasa wa upinzani. Silaha zinapelekwa wapi ili zikafanye nini??
Inasikitisha polisi wana resources zote za kuwezesha kuwasaka hawa maharamia na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola.......
AU pengine ni desparation kuona kuna double standard katika kutoa justice. Kama mtu kapoteza kibarua chake kwa sababu ya ubashiteism wakati bashite yuko anakula bata, WHAT DO YOU EXPECT?
 
Mimi hapa kwa jicho langu la 3 naona kama kuna chezo linachezwa.....ngoja kwanza niwe na akiba ya maneno nisijeitwa Mchochezi
 
Roho za marehemu zipumzike kwa amani[emoji120] Nahisi tumejichanganya au kupotoka kwani askari kwa sasa wamekua na kujiona sehemu ya wakusanya kodi..::nahisi umakini utakuwa umetoweka hence kilings zinazoendelea. Tulitarajia kulindwa na askari sasa wanapokufa ktk mazingira yasiyo ya kivita inaleta mashaka in all wises. Wizara ina minister kitu gani sasa mtuambie.
 
Hapo mh, atume Jeshi Kwa hili
Oparation tafuta watu kwa fujo huja na majanga mengine kwani wanajeshi wataenda kuwavuruga watu wasio na hatia maana wauaji pengine Bashite aliwatoa Burundi au Rwanda na Uganda na wameshakimbia huko, endapo wataenda kuwavuruga wananchi wasio na hatua watazidisha chuki zaidi, ni bora uchunguzi wa kisayansi kwa kushirikiana na wakazi wa huko ufanyike taratibu ndipo watabaini Ukweli wote.
 
Nionavyo mimi ni makundi ya maharifu yanakusanya silaha.


Tatu viongozi wa dini ya kiisilam, wale wanaowaza mema, wakae na wajadili namna ya kukomesha mitazazmo mibovu ya baadhi ya watu walio nao juu ya maisha. Bila shaka wanafahamu haya ni kwa nini yanatokea kwa kuwa eneo yanakotokea haya ni kule kwenye wingi wa wafuasi wao ambao wameshindwa maisha. Wanatakiwa wawape elimu sahihi namna wataboresha maisha yao badala ya kutafuta njia za kiharamia au kutaka kuharibu nchi ili wakose wote. Hii ni roho ya shetani yule mwenye wivu.

.

Wewe mbona akili yako finyu sasa swala la 'uislam' na kuwahusisha viongozi wa kiislam limekujaje? Kwa hiyo una-assume watu waliouwa askari ni waislamu? Sasa ikitokea wakawa wakristo utasemaje? Kwa hiyo kwa statics zako unafikiri sehemu lilikotokea tukio ni sehemu wanaishi waislamu watupu. Kwani ujambazi au ugaidi unaweza kufanywa tu na watu wa sehemu lilipotokea tukio? Haiwezekani watu wakatoka sehemu nyingine? Wewe na Paskali wote mnashindwa hata kuongelea pia vipi wale raia waliokutwa wamekufa Pwani, mpaka leo hatujui walikufaje na wala miili yao imezikwa bila kufanyiwa uchunguzi.
 
Wanaposema kazi ya jeshi la polisi ni kulinda raia na mali zao nilidhani kweli....alafu nilidhani ile midege inayozunguka angani kufanya mazoezi kazi yake mojawapo ni kuangalia wahalifu wakiwemo watekaji na magaidi na wale wanaotorosha twiga kumbe hamna kitu mbwembwe tu kazi kuzuia mikutano ya upinzani....
Nasikia pia kuna rada,,,,,,sijuagi kazi yake nn ktk nchi hii wkt ni kitu cha matrillioni ya shilling
 
Uwe ugaidi uwe ujambazi suluhisho lake ni lile lile nalisema kila siku.
Askari wetu wawezeshwe kwa vifaa, mafunzo na hata akili zao ziwe boosted kwa kugewa mafunzo ambayo dunia inaenda nayo kwa sasa.

Pia wasitumiwe kisiasa, askari anatakiwa kutii bila kuhoji. Hawa viongozi wanaowapa maagizo ya kisiasa waache hivyo, wanawachonganisha raia na askari.

Waziri wa Mambo ya Ndani ajiuzulu, IGP ajiuzulu pia. Kitu kimoja kinatokea sehemu moja zaidi ya mara mbili lakini bado wapo ofisini na hawaoneshi kama wana mkakati wowote wa kutatua tatizo.
 
Back
Top Bottom