tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Sikio halizidi kichwa. Huu ni msemo maarufu wa wahenga unaolenga kuwaonya watoto kuwaheshimu wazazi/walezi wao au wafanyakazi kuwaheshimu waajiri na viongozi wao wa kazi.
Anayejiita mtangazaji (mimi namuona kama mchekeshaji tu) Maulid Kitenge wa Wasafi FM ameshindwa kuuishi msemo huu wa wahenga. Leo asubuhi wakati wakiwa kwenye kipindi cha Good norning amewashawishi watangazaji wenzake kuacha kuisoma habari ya Lissu kushambuliwa na wasiojulikana kwa msaada wa kampuni ya simu ya tiGO. Habari waliyoacha kuichambua imeandikwa kwenye vichwa vya magazeti yote, likiwemo gazeti la mwananchi.
Sababu alizotoa ni kuwa habari hiyo ni nzito, hivyo haipaswi kwenda hewani na kwamba inaweza kuwaletea mgogoro. Lakini nimesikiliza redio zote zimeisoma na kuichambua hiyo habari isipokuwa Kitenge na wachekeshaji wenzake ndio wameiruka hii habari kama ilivyoandikwa na magazeti mbalimbali hapa chini:
Lissu kuwashtaki tIGO kwa kuwasaidia waliotaka kumuua
Sio mara moja Kitenge kutumia uchawa wake kuacha kutangaza habari ambazo zinaigusa moja kwa moja CCM na serikali yake. Sote tunakumbuka jinsi alivyotumia Wasafi FM Radio kuzima na kupotosha suala la DP World. Na wala sio mara ya kwanza Kitenge kulaumiwa na wasikilizaji kupotosha au kulazimisha habari anazozitaka yeye.
Siku za nyuma kuna mdau mmoja alialamika hapa JF kuhusu Kitenge kuitumia Wasafi Radio kama chombo.chake binafsi kupromote mambo ya timu ya Yanga na kuididimiza Simba. Siku za karibuni tumeshuhudia akiitumia Wasafi FM kumtukana mzee Magoma, kwa sababu tu Magoma kafungua kesi halali kuishitaki Yanga. Wala hakuogopa kutumia redio kumtukana mzee Magoma hadharani, hasa ukizingatia bado kesi ipo mahakamani.
MAONI YANGU
Wasafi FM ni chombo cha habari kinachoendeshwa kibiashara. Mmiliki wa chombo hiki asipokuwa makini na kumruhusu Kitenge kikutumia kama chombo binafsi cha kutangazia mambo anayoyapenda tu, kitapoteza mwelekeo na kupotea katika tasnia ya utoaji habari. Redio itapoteza wasikilizaji na mapato kutokana na matangazo yatapungua. Hapo ndipo chawa Kitenge atakapoanza kuhangaika huku na huku akitafuta kazi kwenye vituo vingine vya redio.
Namshauri mmiliki wa redio hii amuonye Kitenge na wachekeshaji wenzake waache kutumia Wasafi FM kwa manufaa yao binafsi kabla hajavuna mabua.