Maulid Kitenge, huoni aibu kuwasaliti Watanzania wenzako? Hatimaye ukweli umefichuka

Kumshutumu mtu bila ushaidi wa kutosha ni kuvunja sheria kwa sisi waamini ni zambi usikute na wewe una sababu zako weka visibitisho ili tuamini ujue jamii forums inasomwa na watu wengi kuliko unavofikiri nini mwandishi ata wewe unaweza kwenda uko ukatuambia nini kinaendelea

Hilo gazeti linaaminika kwa habari za kiuchunguzi na kiuhakika, sio gazeti la udaku hilo ndugu yangu, halafu hii si mara ya kwanza hao OBC kufanya hili jaribio
 
Walipouza Loliondo gazeti la kwanza kuripoti taarifa ile (Motomoto) lilifunguwa mazima hadi leo.. Na hilo hilo lilifungiwa pia kwa kusema Zanzibar ilipojiunga na OIC. Kama kawa, ilipingwa kwanza na Serikali na watu kadhaa kuliwa vichwa.. LAKINI HADI LEO LOLIONDO SIYO YETU TENA.. Hao hao akina so called royal family walifanya yao.

LEO WAMERUDI TENA
R.I.P Stan Katabalo.
 
Mwanzoni mwa mwezi huu wa pili 2022 kuliibuka ghafla na kwa kasi ya ajabu jitihada za makusudi za kujaribu kuwaondoa wamasai katika ardhi zao za kimila huko Ngorongoro kwa madai ya kwamba binadamu wamekuwa wengi huko Ngorongoro na hivyo wanaharibu ekolojia.

Vita hii ya kuwaondoa wamasai ilikuwa spear headed na nguli wa habari za michezo ndugu MAULID KITENGE ambapo alifanya ziara huko Ngorongoro na kutuambia WaTz kwamba eti ‘HALI INATISHA HUKO NGORONGORO’;

Wengi wetu tulihisi kuna jambo nyuma ya pazia, kwamba ghafla tu mtu wa michezo anaenda kushikia bango jambo lisilo la kimichezo; kiasi tulipata hisia kwamba amaelipwa pesa ili kueneza propaganda kwa maslahi ya waliomtuma.

Haya sasa, imekuja kugundulika kwamba hilo eneo la Ngorongoro anataka kuuziwa kampuni ya uwekezaji toka Falme za kiarabu inayomilikiwa na ‘Royal family’ kwa ajili ya kuendesha uwindaji wa kujifurahisha (game hunting), kampuni hiyo inaitwa OBC.

Sasa namuuliza ndugu yangu Kitenge, HUONI AIBU kuwasaliti WaTanzania wenzako?!

Kwani haujui tabia na watu wanaofanya vitendo vya hovyo mfano wa marehemu Defao uwa hawana akili.
 
Rais wa JMT akiwa mzenj basi mbuga zetu bara zitauzwa sana. Sitasahau mambo ya bi Siti Mwinyi. Wamasai wakomae tu wakatae kuhama. Wamasai wapo huko tokea 185.... leo ndo uwafukuze ?Stupid.
Iko hivi. Kati ya watu wenye fedha chafu, na wanapenda starehe na wako tayari kutumia fedha ili wakidhi matakwa yao ni waarabu. Sasa hawa jamaa kila anaposhika urais mtu ambaye wanaona wanaweza kumuingia kwa urahisi, kwa kutumia fedha huwa ni lazima watumie hiyo fursa. Kwa hiyo, kwa vile marais (soma marahisi) wengi wanaotoka Zenji wana connection za uarabuni, inakuwa ni rahisi kuwaingia. Pia kuna elements za udini huwa zina-play role.
 
Doesn't the end Justify the Means

Hata kama kitenge ni Msaliti Je kinachosemwa hakina ukweli ?

Mimi kama Mtanzania na Mwanamazingira nasema wamasai wasibaki huko na hao wanaotaka kujifurahisha wasipewe eneo, eneo libaki kwa manufaa ya Watanzania wote na walimwengu wote sio individuals (be it Wamasai au so called Royal Family)
 
Ukweli huu umeanza wiki iliyopita?, au huko nyuma ilikuwaje? Kama wanahamishwa ili pabaki wazi sawa, ila wana mpango wa kuhamisha wazawa ili mtu aje na magari yake kuua wanyama for leisure? Its insanity, vihoteli viwili vitatu vya kulala hao wauaji wa wanyama vitakavyomilikiwa na wao wenyewe ndio vitatusaidia nini? Waje kama watalii wengine kwa kutumia kamapuni za utalii za kizalendo zilizopo, na watalii kama kawaida waondoke, sio kuja kuua wanyama
 
Doesn't the end Justify the Means

Hata kama kitenge ni Msaliti Je kinachosemwa hakina ukweli ?

Mimi kama Mtanzania na Mwanamazingira nasema wamasai wasibaki huko na hao wanaotaka kujifurahisha wasipewe eneo, eneo libaki kwa manufaa ya Watanzania wote na walimwengu wote sio individuals (be it Wamasai au so called Royal Family)
Sawa kabisa eneo libakie wazi, mmaasai waondoke na mwarabu asipewe kitu.
Sasa kama kweli RC ndiyo alienda kutangaza Nia ya kuwapa waarabu eneo!? Hii serikali ijitafakari, kuna namna nyingi za kupata fedha!
 
Hujui sakata kwa undani ndiyo maana unasema hivi. Kitenge anafanyia kazi tumbo lake na watu wa aina hii ni hatari mno mno kwa Taifa letu. Hao waarabu wanatumia fedha kutaka kuchukuwa hilo eneo ni hatari mno mno. Kama ni mambo ya mazingira kuharibiwa ujuwe hata utalii usipokuwa-controlled nao unaleta madhara makubwa kuliko hata ya wamasai.
 
Kwa sisi ambao tupo kwenye tasnia ya Habari hasa habari za mtandaoni (Online Media).

Kitenge ukiachilia mbali kama kweli alilipwa, alichokuwa akifanya ni kuvuta wafuasi na kujiongezea fame ili afuatiliwe na wengi.

Hii imejizihirisha kwa sababu hata FRANCIS DA DON umemuandalia uzi huyo kitenge.

Ila jambo hilo alilo fanya kitenge si zuri...
 
Sawa kabisa eneo libakie wazi, mmaasai waondoke na mwarabu asipewe kitu.
Sasa kama kweli RC ndiyo alienda kutangaza Nia ya kuwapa waarabu eneo!? Hii serikali ijitafakari, kuna namna nyingi za kupata fedha!
Mkuu kama kuna ukweli hapa basi ujue kuna watu wakubwa nyuma ya RC. Siyo rahisi RC aongelee jambo kubwa kama hilo bila kutumwa. Hint: RC anateuliwa na nani?
 
Mwanzoni mwa mwezi huu wa pili 2022 kuliibuka ghafla na kwa kasi ya ajabu jitihada za makusudi za kujaribu kuwaondoa wamasai katika ardhi zao za kimila huko Ngorongoro kwa madai ya kwamba binadamu wamekuwa wengi huko Ngorongoro na hivyo wanaharibu ekolojia.

Vita hii ya kuwaondoa wamasai ilikuwa spear headed na nguli wa habari za michezo ndugu MAULID KITENGE ambapo alifanya ziara huko Ngorongoro na kutuambia WaTz kwamba eti ‘HALI INATISHA HUKO NGORONGORO’;

Wengi wetu tulihisi kuna jambo nyuma ya pazia, kwamba ghafla tu mtu wa michezo anaenda kushikia bango jambo lisilo la kimichezo; kiasi tulipata hisia kwamba amaelipwa pesa ili kueneza propaganda kwa maslahi ya waliomtuma.

Haya sasa, imekuja kugundulika kwamba hilo eneo la Ngorongoro anataka kuuziwa kampuni ya uwekezaji toka Falme za kiarabu inayomilikiwa na ‘Royal family’ kwa ajili ya kuendesha uwindaji wa kujifurahisha (game hunting), kampuni hiyo inaitwa OBC.

Sasa namuuliza ndugu yangu Kitenge, HUONI AIBU kuwasaliti WaTanzania wenzako?!

Hey mr Don, wa Tanzania na watanzania zina maana mbili tofauti, kwenye Post yako ulitakiwa utumie watanzania na siyo wa Tanzania.
 
Hujui sakata kwa undani ndiyo maana unasema hivi. Kitenge anafanyia kazi tumbo lake na watu wa aina hii ni hatari mno mno kwa Taifa letu. Hao waarabu wanatumia fedha kutaka kuchukuwa hilo eneo ni hatari mno mno. Kama ni mambo ya mazingira kuharibiwa ujuwe hata utalii usipokuwa-controlled nao unaleta madhara makubwa kuliko hata ya wamasai.
Mimi kumuongelea Kitenge au an individual naona ni kupoteza rasilimali yangu ya muda..., nachoweza kujadili ni kinachoongelewa na impact yake kwahio binafsi hao wamasai au hao wanaotaka kumilikishwa eneo la UMMA / JAMII kwa manufaa yao; wote wapigwe chini eneo libaki kwa kutunzwa ili kila atakaye aweze kwenda kuburudika na sio kuharibu wala kuishi....
 
Back
Top Bottom