Tatizo la Bongo kila mtu mwenye ki connection kidogo cha umaarufu basi tayari anahusishwa na serikali hasa usalama wa taifa. Sitostaajabu siku ukisikia Diamond au Ali Kiba nao wanahusishwa na 'kutengo'.
Hili tatizo kwa kiasi kikubwa linachangiwa na hao TISS wenyewe kuajiri watu wa ovyo wanaotoa siri za shirika kiasi kwamba hata madalali wa vyumba wanavaa kaunda suti na kibendera na wao wanajifanya watu wa serikali.
Kurudi kwenye swali lako, wewe chukulia ni muandishi wa habari tu kama anavyotambulika, hayo mengine hayana tija kwako wala kwa wengine wasio na nasaba nae yeyote
Nina hakika wazazi wake, mkewe, watoto, ndugu na marafiki zake wanajua zaidi. Ikiwa wewe hujui zaidi ya uandishi wa habari wake basi hupaswi kujua zaidi ya hilo.