Utafiti ulifanywa ndio maana wakaruhusiwa kukaa toka 1959.
Wanachodai ni utafiti upi umefanyika kuona kuna athari hizo?
Wanadai hizi habari zimeshikiwa bango na wawekezaji kama uficho
wa kuwatoa ili wapate kuingia.
Bandiko lako linainua hoja mbili, moja chanya, na nyingine hasi, kwa uwepo wa Ngorongoro.
Hoja chanya ni hiyo uliyosema kuwa kuna 'Wawekezaji' wanashikia bango kuwatoa Wamasai ili waingie wao.
Hao siyo 'Wawekezaji', hao ni 'Waharibifu na Wauaji' wa Serengeti Conservation Area.
Inaonekana unayajua mengi juu ya hili na wewe kama Mtanzania unatakiwa ufunguke ili Watanzania wote tuwe na uelewa wa pamoja, kwa lengo la kujenga 'National consensus' juu ya kuilinda Ngorongoro.
Watanzania wanaojenga Makazi ya kudumu Ngorongoro ni wabaya, sawa na hao waitwao Wawekezaji wanaonyemelea kuingia Ngorongoro.
Wote ni Waharibifu na Wauaji wa Ngorongoro.
Watanzania tusikubali.
Tuitunze na kuilinda Ngorongoro.
Ndiyo sababu hii hoja yako ni Hoja chanya.
Hoja hasi ni hiyo ya kuuliza Utafiki uliofanyika baada ya ule wa mwaka 1959, ambao ulihalalisha Binadamu (na hapa tusisitize neno Binadamu, badala ya Wamasai, ili kuondoa 'notion ya Ukabila'), kuishi pamoja na Wanyama.
Hatuwezi kukaa na kusubiri Utafiti ufanyike wakati Ngorongoro inateketea.
Tuinue sauti zetu kama alivyofanya Maulid Kitenge ili tuiokoe Ngorongoro.
Mods, upo umuhimu wa JamiiForums kuishikia Bango hoja ya Kuiokoa Ngorongoro, ili mamlaka zinazohusika zitimize wajibu wao.
JF imeisha thibisha kuwa na uwezo huo.
Founder @maxencemello, ukiweka uzito wako unaoeleweka na kukubalika Kitaifa na Kimataifa, tunaweza kuiokoa Ngorongoro.
Ninaomba ufunguliwe UZI MAHUSUSI kuiokoa Ngorongoro.