Maulid Kitenge, propaganda ulizotumwa kuzifanya kwa wana-Ngorongoro hazitakuacha salama

Maulid Kitenge, propaganda ulizotumwa kuzifanya kwa wana-Ngorongoro hazitakuacha salama

Kitenge na Oscar wamefikiri ni kuchambua mpira.Hilo la Ngorongoro ni tatizo complex. Huwezi kuleta vi clip vya dakika 2 ukapata ukweli.
Eti wamasai wanaishi kwenye umaskini. Kwani tatizo la Ngorongoro Conservation Authority ni wamasai kuishi kwenye umaskini au utajiri?
Kama kuna tatizo lipatiwe ufumbuzi kitaalamu na sio ripoti ya makanjanja wawili wasiojua lolote kuhusu NCA.
 
Wewe jamaa ndo mkuu wa wilaya au ndo Mkurugenzi hapo Ngorongoro?? Mbona Kama unaogopa kutumbuliwa....maulid apo anahusika vipi wakati yy alikua akichambua magazeti?
Atakuwa ni mfugo wa nyoronyoro anataka nae awe kwenye conservation plan maana haiwezekani mtu na akili yake ang'ang'anie kuishi na fisi, tembo, nyumbu nguruwe pori na anataka atambulike kwamba nae awe kwenye conservation.

Mifugo inataka kukaa na mifugo wenzao. Atakayekasirika koroga sementi unywe uji wake.
 
Utafiti ulifanywa ndio maana wakaruhusiwa kukaa toka 1959.
Wanachodai ni utafiti upi umefanyika kuona kuna athari hizo?
Wanadai hizi habari zimeshikiwa bango na wawekezaji kama uficho
wa kuwatoa ili wapate kuingia.
Bandiko lako linainua hoja mbili, moja chanya, na nyingine hasi, kwa uwepo wa Ngorongoro.
Hoja chanya ni hiyo uliyosema kuwa kuna 'Wawekezaji' wanashikia bango kuwatoa Wamasai ili waingie wao.
Hao siyo 'Wawekezaji', hao ni 'Waharibifu na Wauaji' wa Serengeti Conservation Area.
Inaonekana unayajua mengi juu ya hili na wewe kama Mtanzania unatakiwa ufunguke ili Watanzania wote tuwe na uelewa wa pamoja, kwa lengo la kujenga 'National consensus' juu ya kuilinda Ngorongoro.
Watanzania wanaojenga Makazi ya kudumu Ngorongoro ni wabaya, sawa na hao waitwao Wawekezaji wanaonyemelea kuingia Ngorongoro.
Wote ni Waharibifu na Wauaji wa Ngorongoro.
Watanzania tusikubali.
Tuitunze na kuilinda Ngorongoro.
Ndiyo sababu hii hoja yako ni Hoja chanya.
Hoja hasi ni hiyo ya kuuliza Utafiki uliofanyika baada ya ule wa mwaka 1959, ambao ulihalalisha Binadamu (na hapa tusisitize neno Binadamu, badala ya Wamasai, ili kuondoa 'notion ya Ukabila'), kuishi pamoja na Wanyama.
Hatuwezi kukaa na kusubiri Utafiti ufanyike wakati Ngorongoro inateketea.
Tuinue sauti zetu kama alivyofanya Maulid Kitenge ili tuiokoe Ngorongoro.
Mods, upo umuhimu wa JamiiForums kuishikia Bango hoja ya Kuiokoa Ngorongoro, ili mamlaka zinazohusika zitimize wajibu wao.
JF imeisha thibisha kuwa na uwezo huo.
Founder @maxencemello, ukiweka uzito wako unaoeleweka na kukubalika Kitaifa na Kimataifa, tunaweza kuiokoa Ngorongoro.
Ninaomba ufunguliwe UZI MAHUSUSI kuiokoa Ngorongoro.
 
moja ya hoja dhaifu kuwai tokea JF ni hii ya huyu jamaa .. yeye analeta siasa kwenye uhalisia , sasa ulitaka Maulidi akae kimya? amefichua alichokiona kwa manufaa makubwa ya Hifadhi
 
Watu wanahamishwa barabara ikijengwa, watu wanahamishwa pakigundulika ardhi Ina madini yaani nyie ni kina nani msihamishwe ???

The fact kwamba mlikuwepo hapo from 1950's haiwapi legality ya kuendelea kukaa Kama itaonekana mnaweka threat kwa wanyama pori.

As long as eneo hilo lilishatangazwa kuwa protected na sheria sioni sababu ya hao wamasai kung'ang'ania after all hakina walichojenga au wanacholima zaidi ya kufuga ng'ombe wanaonyang'anyana malisho maana wanacholazimisha ni kupata Yale mapori ambapo kwingine wanajua hawataweza kufuga kwa style Ile .

Tuwe na uchungu na taifa letu, ng'ombe wanaongezeka na familia zao zinaongezeka siku Hadi siku, better late than never.

Hii nchi tunaongozwa kwa sheria, mbona wengine wanahamishwa kupisha maslahi mapana ya Taifa?? Kwa nini wao wajione ndio wenye nchi pekee?
Wale Wamasai na wanyapori wa Ngorongoro wapo Kisheria. Ngorongoro imekuwa designated kama World Heritage Site na shirika la UNESCO, kwa kuwa hawadhuriani na wanyama pori. Hali iliyopo Ngorongoro ndiyo iliyopo maeneo mengine ya wilaya za Monduli, Babati nk ambako kuna mapito ya wanyama ama mbuga za . Hakuna sababu ya kuwaondoa, waachwe waendelee ku coexist na wanyamapori
 
After Ngorongoro where is next?Tarangire watu wanaishi pamoja na wanyama.
Kitenge hana data za kiuchunguzi.Anafikiri ni kuchambua mpira au kusoma magazeti.
Hili tatizo ni complex tuachie wataalamu.Huwezi kuwa so called Mwenyekiti wakati hujui kwa kina tatizo ni nini?
Kulikuwa na makubaliano ya 1959.Baadaye ikaja hukumu ya mahakama.What happened next?
 
Bandiko lako linainua hoja mbili, moja chanya, na nyingine hasi, kwa uwepo wa Ngorongoro.
Hoja chanya ni hiyo uliyosema kuwa kuna 'Wawekezaji' wanashikia bango kuwatoa Wamasai ili waingie wao.
Hao siyo 'Wawekezaji', hao ni 'Waharibifu na Wauaji' wa Serengeti Conservation Area.
Inaonekana unayajua mengi juu ya hili na wewe kama Mtanzania unatakiwa ufunguke ili Watanzania wote tuwe na uelewa wa pamoja, kwa lengo la kujenga 'National consensus' juu ya kuilinda Ngorongoro.
Watanzania wanaojenga Makazi ya kudumu Ngorongoro ni wabaya, sawa na hao waitwao Wawekezaji wanaonyemelea kuingia Ngorongoro.
Wote ni Waharibifu na Wauaji wa Ngorongoro.
Watanzania tusikubali.
Tuitunze na kuilinda Ngorongoro.
Ndiyo sababu hii hoja yako ni Hoja chanya.
Hoja hasi ni hiyo ya kuuliza Utafiki uliofanyika baada ya ule wa mwaka 1959, ambao ulihalalisha Binadamu (na hapa tusisitize neno Binadamu, badala ya Wamasai, ili kuondoa 'notion ya Ukabila'), kuishi pamoja na Wanyama.
Hatuwezi kukaa na kusubiri Utafiti ufanyike wakati Ngorongoro inateketea.
Tuinue sauti zetu kama alivyofanya Maulid Kitenge ili tuiokoe Ngorongoro.
Mods, upo umuhimu wa JamiiForums kuishikia Bango hoja ya Kuiokoa Ngorongoro, ili mamlaka zinazohusika zitimize wajibu wao.
JF imeisha thibisha kuwa na uwezo huo.
Founder @maxencemello, ukiweka uzito wako unaoeleweka na kukubalika Kitaifa na Kimataifa, tunaweza kuiokoa Ngorongoro.
Ninaomba ufunguliwe UZI MAHUSUSI kuiokoa Ngorongoro.
Hizi stori za Ngorongoro inateketea wakati ngorongor ni zaidi ya mkoa wa kilimanjaro,
na wamasai wanaishi tarafa moja ni ajabu.
Wahifadhi wa Ngongoro mbona hawajaona kama inateketea wewe na maulidi ndio mnaoona hilo?
Haya mambo ya kukwepa utafiti yanatia shaka.
Utajuaje huo uharibifu unasababishwa na wamasai kama hujafanya utafiti na kiwango gan.
Mtuambie pia ni uharibifu upi ambao upo na unatishia eneo la ngorongoro hivyo
wamasai watoke.
 
FK7se9aXwAEwzFk.jpeg
 
Hoja ni kwamba, hao watu ipo siku watazidi na hiyo itasababisha wanyama kukimbia kutokana na makazi ya binadamu kukua zaidi.

Kwa mtindo wa sasa, ngorongoro miaka 50 ijayo haitakuwepo.
Wameshazidi mbona,
Kila kitu kina capacity ndugu mtoa hoja .... unataka watalii waende kwenye Crater kushangaa ng’ombe na idadi kubwa ya watu!?

Hiyo mwaka 1950s population ya watu na mifugo ilikuwaje ukilinganisha na sasa hivi ?
Hii tayari

Screenshot_20220207-102105_Samsung Internet.jpg
 
moja ya hoja dhaifu kuwai tokea JF ni hii ya huyu jamaa .. yeye analeta siasa kwenye uhalisia , sasa ulitaka Maulidi akae kimya? amefichua alichokiona kwa manufaa makubwa ya Hifadhi
Wale wahifadhi wanaoshinda kila siku hifadhini hawajaona hillo.
maulid mchambuzi wa mpira kwa dakika mbili ameliona hilo duh!!.
 
Sasa mkiwafukuza hao Wamasai si wataingia kwenye ujangili wamalize kabisa hao wanyama pori? Kuna kitu kinaitwa "law of uninteded consequences" lazima kiangaliwe. Kuwafukuza Wamasai unaweza kuwa unatatua tatizo moja halafu unaleta tatizo lingine la ujangili bila kutegemea.
WanapewA maeneo mengine
 
Kama wanyama wanakula watu, Maulid akasema baada ya kuona serikali ya pale iko kimya je kuna ubaya?

Watu wapishe hifadhi.
 
Kuhusu Ngorongoro, kama shida ni nyumba za kisasa basi mahoteli yote yabomolewe Ngorongoro kwani hakuna hata moja ya matope. Kama shida ni idadi ya watu, waanze kuondolewa waliokuja na kuwakuta wamasai. Ukiachilia mbali Kelele za kina Kitenge na Wapuuzi wengine, hakuna Utafiti wa Kisayansi unaoonesha athari zinazotamkwa kuhusu eneo hilo la mamlaka ya Ngorongoro. Kama ni athari wangeandamana mamilioni ya miti yalipofyekwa Selous KWA ajili ya mradi wa Umeme.
Kingine, ukiwaondoa Wamasai Ngorongoro maana yake umeiondoa Ngorongoro. Huwezi kuitenganisha Ngorongoro na Masai. Never
 
Ilianza NGORONGORO ndio wakafuata WAMASAI
 
Ngorongoro Conservation Area siyo ya Wamasai pekee, ni ya Watanzania wote, na inahitaji Mjadala wa kina.
Itakuwa aibu na fedheha kubwa kwa Taifa letu kama hii World Heritage itapotea kutokana na kuogopa kelele za Wanaharakati ambao wameigeuza Ngorongoro kuwa mali ya Wamasai.
Hii ni hatari.
Serengeti nayo iwe ya Wakurya?
Ruaha iwe ya Wahehe?
Mikumi iwe ya Wakaguru?
Mazingira ya Ngorongoro ya Binadamu kuishi na Wanyamapori yanakubalika, lakini ni lazima kuwe na Ulinganifu wa Kiekolojia, 'Ecological balance'.
Majumba yanajengwa ndani ya Ngorongoro. Hii siyo sawa.
Ngorongoro ikipotea, sisi sote tutaingia katika fedheha isiyo na kipimo.
Kumtukana Maulidi Kitenge kwa kuandika kilichopo, hakuisaidii Tanzania wala Wamasai wanaoishi Ngorongoro.
Malisho yakiharibiwa, Wanaharakati hawataonekana kuwafadhili Wamasai.
Watakimbilia kusikojulikana.
Tuiokoe Ngorongoro.
Mkuu kunywa Soda baridi nakuja kulipa
 
Ilianza NGORONGORO ndio wakafuata WAMASAI
Are you sure?Ngorongoro as Ngorongoro Conservation Authority ilianza lini?
Bonde la Ngorongoro lilikuwa na wamasai tokea lini?
Wacha kuja na majibu mepesi kwa maswali magumu.
Watoke na lugha rahisi hazimsaidii yeyote.
Tatizo litatuliwe kitaalamu na kwa utafiti wa kisayansi na sio hocus pocus za kina Maulid Kitenge na wapambe wao.
 
Back
Top Bottom