Maulid Kitenge, propaganda ulizotumwa kuzifanya kwa wana-Ngorongoro hazitakuacha salama

Miaka 20 ijayo ngorongoro itapotea kisa Tu ubinafsi wa mwanadamy na kuona ana haki ya kuishi popote...!! Upuuzi huu upingwee wamasai wakaishi mahali sahihi sio kwenye makazi ya wanyama poriii....
 
Maulid wako katumiwa kama daraja tu, kwa taarifa yako UTALII wa uwindaji ndi sababu KUU ya kuondolewa jamii ya kimasai ...nikuulize unajua ni hasara gani tutapata baada ya hayo kufanyika?

Tafakari.

Sent using Jamii Forums mobile app
Badilisha 'tune' ya lugha unayotumia.
Do not fight.
Educate.
Unaandika mambo mazuri sana kwa lugha inayoleta ukakasi.
Kisha unakwepa kujibu hoja za msingi.
Suala la Wawindaji kuwinda ndani ya Ngorongoro halikubaliki hata kidogo.
Na ukilisemea hili na ukatueleza jitihada hizo za kutaka kuweka Vitalu vya Uwindaji Ngorongoro, Watanzania tutaungana kulipinga kwa nguvu zetu zote.
Sambamba na hili zungumzia juu ya ongezeko la Wafugaji na Mifugo.
Kwamba idadi bado ni himilivu?
Kwa kuwa idadi inaendelea kuongezeka kila siku, nini kifanyike?
Hicho kinachotakiwa kufanyika, kianze lini?
Pia utaratibu wa Ujenzi ndani ya Hifadhi, unaratibiwa?
Au kila anayetaka kujenga, anajenga kiholela?
Haya ni mambo ambayo ukiyatolea ufafanuzi, yatatufanya Watanzania wote tuelewe kinachoendelea Ngorongoro.
 
Wewe shoga hao dinosaur umewahi kuwaona?
 
Miaka 20 ijayo ngorongoro itapotea kisa Tu ubinafsi wa mwanadamy na kuona ana haki ya kuishi popote...!! Upuuzi huu upingwee wamasai wakaishi mahali sahihi sio kwenye makazi ya wanyama poriii....
Rikiboy, sababu ya kuanzisha Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, ilikuwa ni kukubali na kutambua utaratibu uliokuwepo Bonde la Ngorongoro, la Wafugaji kuishi na kufuga Ng'ombe na Mbuzi zao huku wakizungukwa na Wanyamapori.
Hali hii ni kivutio kikubwa sana.
Na imechangiwa na ukweli kwamba Wafugaji wa Ngorongoro hawatumii nyama ya Wanyamapori kama kitoweo.
Hawali nyama ya Swala, wala ya Ngiri, wala ya Nyumbu.
Wanakula nyama ya Ng'ombe na Mbuzi.
Kinacholeta Mjadala hapa ni kuongezeka kwa idadi ya Watu na Mifugo yao.
Watu wameongezeka kutoka 8271 wakati Mamlaka inaanzishwa, mwaka 1959, hadi kufikia zaidi ya 120,000.
Ng'ombe walikuwa 30,000 lakini sasa wapo zaidi ya 1,000,000
Hakika ni lazima Watanzania tulijadili hili na tupendekeze jawabu.
 
Jawabu ni kutunga sheria ya kuweka mipaka ya mwisho kwa wanadamu kufanya shughuli za kimaendeleo lakini ni ngumu maana washaona wanastahili kuendelea kujenga na kujiachia hapo Ngorongoro. Hapo ndo suala la kuwaondoa linakuja maana wakiachwa kesho wanyama wataamua kuondoka kuwaachia wanadamu nafasii
 
Hazifatwi sababu wamasai washaona wanaimiliki ngorongorooo
Usitumie neno Wamasai, tuwaite Wafugaji.
Wahenga walisema Mdomo unaumba.
Haya maneno kuwa Ngorongoro ni kwa Wamasai, kumewafanya Wafugaji wa kabila la Kimasai wajione wamiliki wa Ngorongoro.
Jiulize, ikitokea 'epidemic' Ng'ombe wote wakafa, ikabidi kuingiza Wafugaji kutoka Kabila nyingine kama Wamang'ati, Wagogo, Wasukuma au Wakurya ili ku-maintain 'ecosystem' ya Ngorongoro, si itatokea Vita ya Kikabila maana tumewaamisha Wamasai kuwa Ngorongoro ni mali yao?
Tuwaite Wafugaji.
 
Uelewa wako ni mdogo. Listen up, ninachopinga ni kuondoa wanadamu ili wanyama waishi.

Angalau mvua ina faida kwa binadamu na ustawi wake ivyo miti haifai kukatwa na aliekata utonifananisha nae km umeelewa hoja yangu.
Hilo eneo lilitengwa kwa ajili ya wanyama pori mwaka 1959. Wanadamu waliokuweko wakati ule walikubaliwa kuendelea kuishi mle kwa masharti kuwa idadi yao isizidi kiwango kilicho sustainable kwa wanyama pori. Hao wanyama pori wametengewa eneo dogo sana ukilinganisha na eneo ambalo hao binadamu wana haki ya kuishi nje ya hili eneo. Na mbaya zaidi, hao binadamu wanaleta wanyama mbadala ambao ufugaji wao utaathiri hali ilivyo hivi sasa. Kama mnaona wanyama pori hawana maana yeyote basi bora patangazwe kuwa ranchi na kila mtu aruhusiwe kupeleka mifugo yao.

Hivi unadhani hiyo miti unayoitetea inarutubishwa na nani? Au unadhani na yenyewe ilikuwa kwenye plantation? Waliokata ile miti na wewe hamna tofauti.

Amandla...
 
Kajiado Gang... ...first people were Datoga then Maa
 
Utakuwa na jinsia mbili hueleweki kama popo.
NCA hawaja ona athari za mmasai za kutishia kutoweka kwake.
Kama zipo zitaje na chanzo chako?
 
Tatizo la kukithiri kwa wingi wa watu na mifugo ndani ya NCA ni kubwa kuliko Kitenge alivoripoti!
Mle ndani makazi holela na idadi kubwa ya mifugo ni kikwazo kikuu cha ustawi wa NCA.
 
Tatizo la kukithiri kwa wingi wa watu na mifugo ndani ya NCA ni kubwa kuliko Kitenge alivoripoti!
Mle ndani makazi holela na idadi kubwa ya mifugo ni kikwazo kikuu cha ustawi wa NCA.
NCAA walishindwa kumonitor more than decades kujua tatizo litakuwa kubwa kiasi gani ndani ya kipindi fulani, walikuwa wakiona raha kupokea pesa za wazungu wanaosaidia community ya jamii husika..

Kitenge alivyopresent tatizo utadhani kashushwa kutoka mbingu ya saba na ndio kaja na utafiti wenye majibu.

Agenda aliyokuwa nayo anaijua yeye na boss wake aliyemtuma.!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Well said!
NCAA wamelewa mapesa ya watalii.
Kwa sasa watalii wengi hawafurahii wanchokiona. Wenyeji nao malalamiko yamezidi!
Mafungu ya kuandaa GMP wanatafuna mwisho wa siku monitoring na evaluation zinasua sua!

NB: Kitenge ni mpuuzi kama wapuuzi wengine kwenye hizi redio za makelele! Kwenye hili hasiachwe hivi hivi!
 
Sasa kama monitoring zina sua sua kitenge ana Kosa gani kureport???? Bila kitenge kusema tungejuaje ngorongoro mamlaka zinakwama kufanya monitoring ya wamasai?? Mambo yanaenda mrama akiripoti mtu anaonekana mbaya...
 
Sasa kama monitoring zina sua sua kitenge ana Kosa gani kureport???? Bila kitenge kusema tungejuaje ngorongoro mamlaka zinakwama kufanya monitoring ya wamasai?? Mambo yanaenda mrama akiripoti mtu anaonekana mbaya...
Tatizo la Kitenge na Oscar wake wameripoti bila kuwa na basic facts. Wameripoti kama kutaka kuwaonea "wakazi" wa NCA. Hakuwa well informed make huwezi kupinga uwepo wa mifugo na watu ndani ya NCA.
Pili hili jambo tumelipigia kelele humu kwa miaka mingi sana! Kwa uzoefu wangu mifugo mingi inaletwa na "wageni" wakiwemo staff wa NCAA. Udhaifu wa NCAA pia unasababisha ujenzi makazi holela ya wenyeji hifadhini.

NB: Hili la mifugo na "wakazi" ni trela. Muvi nzima ipo kwenye ugawaji holela wa maeneo ya kambi na lodges za watalii. Funga kazi ni ubadhirifu na ukwapuaji wa fedha za NCAA.
Turuhusu mjadala mpana wenye ripoti za kina badala ya taarifa za gengeni kama ile ya Kitenge!
 
Utakuwa na jinsia mbili hueleweki kama popo.
NCA hawaja ona athari za mmasai za kutishia kutoweka kwake.
Kama zipo zitaje na chanzo chako?
Nilifikiri una akili timamu za kuongea hoja bila kujidhalilisha kwa maneno na misemo iliyo kinyume na Mila na Desituri za Kitanzania. Usiongee maneno ambayo hhuwezi kuyatamka mbele ya Wazazi wako.
Wosia huu utakusaidia sana katika maisha yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…