Maulid Kitenge, propaganda ulizotumwa kuzifanya kwa wana-Ngorongoro hazitakuacha salama

Maulid Kitenge, propaganda ulizotumwa kuzifanya kwa wana-Ngorongoro hazitakuacha salama

Andiko lako ni zuri sana. Tena sana.
Kasoro yake ni pale unaposema Wafugaji waondolewe.
Lengo la kuanzisha Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, ni kutunza na kudumisha 'eco-system' ambayo Wafugaji na Wanyamapori wanaishi katika eneo moja.
Hali hiyo iendelee.
Kama ulivyosema, nami nakushukuru kwa kutoa 'data', kutoka Wafugaji 8271 mwaka 1959, mpaka Wafugaji 120,000 na Mifugo 30,000 mwaka 1959 hadi mifugo zaidi 1,000,000 ; Mamlaka ya Ngorongoro itoe Tamko kuhusu uhimilivu wa Hifadhi juu ya kuongezeka kwa idadi ya Wafugaji na Mifugo.
Tamko likitoka, Watanzania tukae pamoja kama Taifa na kukubaliana nini kifanyike.
Lakini tusitenganyishe Wafugaji na Wanyamapori.
Serengeti ni World Heritage kwa sababu ya Wafugaji na Wanyamapori kuishi pamoja.
Hali hii ilindwe na kudumishwa.
Miaka 20 ijayo ngorongoro itapotea kisa Tu ubinafsi wa mwanadamy na kuona ana haki ya kuishi popote...!! Upuuzi huu upingwee wamasai wakaishi mahali sahihi sio kwenye makazi ya wanyama poriii....
 
Maulid wako katumiwa kama daraja tu, kwa taarifa yako UTALII wa uwindaji ndi sababu KUU ya kuondolewa jamii ya kimasai ...nikuulize unajua ni hasara gani tutapata baada ya hayo kufanyika?

Tafakari.

Sent using Jamii Forums mobile app
Badilisha 'tune' ya lugha unayotumia.
Do not fight.
Educate.
Unaandika mambo mazuri sana kwa lugha inayoleta ukakasi.
Kisha unakwepa kujibu hoja za msingi.
Suala la Wawindaji kuwinda ndani ya Ngorongoro halikubaliki hata kidogo.
Na ukilisemea hili na ukatueleza jitihada hizo za kutaka kuweka Vitalu vya Uwindaji Ngorongoro, Watanzania tutaungana kulipinga kwa nguvu zetu zote.
Sambamba na hili zungumzia juu ya ongezeko la Wafugaji na Mifugo.
Kwamba idadi bado ni himilivu?
Kwa kuwa idadi inaendelea kuongezeka kila siku, nini kifanyike?
Hicho kinachotakiwa kufanyika, kianze lini?
Pia utaratibu wa Ujenzi ndani ya Hifadhi, unaratibiwa?
Au kila anayetaka kujenga, anajenga kiholela?
Haya ni mambo ambayo ukiyatolea ufafanuzi, yatatufanya Watanzania wote tuelewe kinachoendelea Ngorongoro.
 
Afadhali umetoka pangoni,nyie ndo mnaofanya mapenzi na mbwa,kuku,ng'ombe nk. ndio hasa mnaumia kwa wapenzi wenu hao wa kishetani kuondolewa.

Look here,dinosaurs wametoweka na wanyama wengine chungu mbovu hawapo tena duniani,where was your stupid ecosystems!? Usikariri,elewa...Mungu ndo fundi mkuu,kuwa na utu tetea survival ya jamii yako yaani wanadamu na sio wanyama poli jamii tofauti na ww...hili nalo hujui!,labda km na wewe ni jamii yao nitakuelewa.

Usiwe km ling'ombe,be human and fight for humans,yaani ata jumbu anakuzidi maarifa! Maana jumbu anatetea sana jamii yake dhidi ya simba.
Wewe shoga hao dinosaur umewahi kuwaona?
 
Miaka 20 ijayo ngorongoro itapotea kisa Tu ubinafsi wa mwanadamy na kuona ana haki ya kuishi popote...!! Upuuzi huu upingwee wamasai wakaishi mahali sahihi sio kwenye makazi ya wanyama poriii....
Rikiboy, sababu ya kuanzisha Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, ilikuwa ni kukubali na kutambua utaratibu uliokuwepo Bonde la Ngorongoro, la Wafugaji kuishi na kufuga Ng'ombe na Mbuzi zao huku wakizungukwa na Wanyamapori.
Hali hii ni kivutio kikubwa sana.
Na imechangiwa na ukweli kwamba Wafugaji wa Ngorongoro hawatumii nyama ya Wanyamapori kama kitoweo.
Hawali nyama ya Swala, wala ya Ngiri, wala ya Nyumbu.
Wanakula nyama ya Ng'ombe na Mbuzi.
Kinacholeta Mjadala hapa ni kuongezeka kwa idadi ya Watu na Mifugo yao.
Watu wameongezeka kutoka 8271 wakati Mamlaka inaanzishwa, mwaka 1959, hadi kufikia zaidi ya 120,000.
Ng'ombe walikuwa 30,000 lakini sasa wapo zaidi ya 1,000,000
Hakika ni lazima Watanzania tulijadili hili na tupendekeze jawabu.
 
Rikiboy, sababu ya kuanzisha Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, ilikuwa ni kukubali na kutambua utaratibu uliokuwepo Bonde la Ngorongoro, la Wafugaji kuishi na kufuga Ng'ombe na Mbuzi zao huku wakizungukwa na Wanyamapori.
Hali hii ni kivutio kikubwa sana.
Na imechangiwa na ukweli kwamba Wafugaji wa Ngorongoro hawatumii nyama ya Wanyamapori kama kitoweo.
Hawali nyama ya Swala, wala ya Ngiri, wala ya Nyumbu.
Wanakula nyama ya Ng'ombe na Mbuzi.
Kinacholeta Mjadala hapa ni kuongezeka kwa idadi ya Watu na Mifugo yao.
Watu wanaongezeka kutoka 8271 wakati Mamlaka inaanzishwa, mwaka 1959, hadi kufikia zaidi ya 120,000.
Ng'ombe waikuwa 30,000 lakini sasa wapo zaidi ya 1,000,000
Hakika ni lazima Watanzania tulijadili hili na tuoendekeze jawabu.
Jawabu ni kutunga sheria ya kuweka mipaka ya mwisho kwa wanadamu kufanya shughuli za kimaendeleo lakini ni ngumu maana washaona wanastahili kuendelea kujenga na kujiachia hapo Ngorongoro. Hapo ndo suala la kuwaondoa linakuja maana wakiachwa kesho wanyama wataamua kuondoka kuwaachia wanadamu nafasii
 
Hazifatwi sababu wamasai washaona wanaimiliki ngorongorooo
Usitumie neno Wamasai, tuwaite Wafugaji.
Wahenga walisema Mdomo unaumba.
Haya maneno kuwa Ngorongoro ni kwa Wamasai, kumewafanya Wafugaji wa kabila la Kimasai wajione wamiliki wa Ngorongoro.
Jiulize, ikitokea 'epidemic' Ng'ombe wote wakafa, ikabidi kuingiza Wafugaji kutoka Kabila nyingine kama Wamang'ati, Wagogo, Wasukuma au Wakurya ili ku-maintain 'ecosystem' ya Ngorongoro, si itatokea Vita ya Kikabila maana tumewaamisha Wamasai kuwa Ngorongoro ni mali yao?
Tuwaite Wafugaji.
 
Uelewa wako ni mdogo. Listen up, ninachopinga ni kuondoa wanadamu ili wanyama waishi.

Angalau mvua ina faida kwa binadamu na ustawi wake ivyo miti haifai kukatwa na aliekata utonifananisha nae km umeelewa hoja yangu.
Hilo eneo lilitengwa kwa ajili ya wanyama pori mwaka 1959. Wanadamu waliokuweko wakati ule walikubaliwa kuendelea kuishi mle kwa masharti kuwa idadi yao isizidi kiwango kilicho sustainable kwa wanyama pori. Hao wanyama pori wametengewa eneo dogo sana ukilinganisha na eneo ambalo hao binadamu wana haki ya kuishi nje ya hili eneo. Na mbaya zaidi, hao binadamu wanaleta wanyama mbadala ambao ufugaji wao utaathiri hali ilivyo hivi sasa. Kama mnaona wanyama pori hawana maana yeyote basi bora patangazwe kuwa ranchi na kila mtu aruhusiwe kupeleka mifugo yao.

Hivi unadhani hiyo miti unayoitetea inarutubishwa na nani? Au unadhani na yenyewe ilikuwa kwenye plantation? Waliokata ile miti na wewe hamna tofauti.

Amandla...
 
IMG_20220207_143057_879.JPG
 
Kajiado Gang...
Are you sure?Ngorongoro as Ngorongoro Conservation Authority ilianza lini?
Bonde la Ngorongoro lilikuwa na wamasai tokea lini?
Wacha kuja na majibu mepesi kwa maswali magumu.
Watoke na lugha rahisi hazimsaidii yeyote.
Tatizo litatuliwe kitaalamu na kwa utafiti wa kisayansi na sio hocus pocus za kina Maulid Kitenge na wapambe wao.
...first people were Datoga then Maa
 
Kwa nini Wafugaji watoke?
Acha kujikita kwenye kivuli cha Ukabila.
Mamlaka ya Ngorongoro ilianzishwa mahsusi ili hali iliyokutwa hapo, ya Wafugaji na mifugo yao, na Wanyamapori, kuishi pamoja, iendelee na kudumishwa.
Wanaotaka Wafugaji watoke ni maadui wa Ngorongoro Conservation Area.
Wanaojenga kiholela ndani ya Hifadhi, nao pia ni maadui wa Ngorongoro Conservation Area.
Wanaharakati wanaopiga kelele kwa kutaja Ukabila, kuwa Ngorongoro ni ya Wamasai, lengo lao ni ku-alienate Watanzania ambao siyo Wamasai ili walifumbie macho suala hilo, waone haliwahusu, ili waendeleze nia zao ovu za kushibisha matumbo yao huku Ngorongoro ikiteketea.
Watanzania hatuwezi kukaa kimya wakati Mazingira ndani ya Hifadhi yetu ya Ngorongoro yanaharibika, kwa sababu ya kelele za Wanaharakati wanaojificha ndani ya kichaka cha Ukabila.
Tunatakiwa tuliseme hili waziwazi na kulipatia ufumbuzi.
Tusiogope kufanya maamuzi magumu.
Lengo letu daima liwe kuhakikisha Wafugaji na Wanyamapori wanaishi ndani ya Ngorongoro kama ilivyokusudiwa mwaka 1959.
Utakuwa na jinsia mbili hueleweki kama popo.
NCA hawaja ona athari za mmasai za kutishia kutoweka kwake.
Kama zipo zitaje na chanzo chako?
 
Somebody said, AirPods journalist is looking towards being District Commissioner or equivalent in this regime.

FYI my Brother Mshambuliaji, hawa ndugu zetu pale wapo kihalali na walihamishwa toka miaka 1950's kutoka Serengeti na nakukumbusha kuna amri ya mahakama ya Afrika Mashariki EACJ inaikataza Serikali kuwaondoa na serikali imekuwa ikiheshimu Amri hiyo tangu sept 2018 (under Magu regime).

Kabla hujasema ya wanangorongoro chukua time ujifunze kwanza. Kwanza hushangai wanyamapori wanaweza vipi kuishi na binadamu bila kudhuriana?

Hivi kweli hujui kwamba hiyo coexistance iliyopo kati ya wanyamapori na na ng'ombe ipo miaka mingi na ndio kitu mojawapo inayovutia watalii, (pengine huna exposure )na ni aibu kwa kijana wa jamii ya pale kula swala au pundamilia wakati mbuzi wapo..

Anyway ni hivi kama unalipwa pesa kufanya propaganda acha mara moja, japo tunasikia kuna kitengo cha Intel NCCA wanahusika kufanya installment ya malipo..(tutacomfirm baadaye)

Tafuta takwimu ujue kama kweli hii hifadhi ipo hatarini , nanakuhakikishia HAKUNA, na kama ipo inakinzana na hali iliopo.

Nakukumbusha acha mara moja hizi propaganda,

Zitakuaharibia.

Pia soma > Hali ya Ngorongoro na wana-habari wanaoshinikiza wamasaai waondolewe hawajui chochote wanatumika vibaya bila kujua
Tatizo la kukithiri kwa wingi wa watu na mifugo ndani ya NCA ni kubwa kuliko Kitenge alivoripoti!
Mle ndani makazi holela na idadi kubwa ya mifugo ni kikwazo kikuu cha ustawi wa NCA.
 
Tatizo la kukithiri kwa wingi wa watu na mifugo ndani ya NCA ni kubwa kuliko Kitenge alivoripoti!
Mle ndani makazi holela na idadi kubwa ya mifugo ni kikwazo kikuu cha ustawi wa NCA.
NCAA walishindwa kumonitor more than decades kujua tatizo litakuwa kubwa kiasi gani ndani ya kipindi fulani, walikuwa wakiona raha kupokea pesa za wazungu wanaosaidia community ya jamii husika..

Kitenge alivyopresent tatizo utadhani kashushwa kutoka mbingu ya saba na ndio kaja na utafiti wenye majibu.

Agenda aliyokuwa nayo anaijua yeye na boss wake aliyemtuma.!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NCAA walishindwa kumonitor more than decades kujua tatizo litakuwa kubwa kiasi gani ndani ya kipindi fulani, walikuwa wakiona raha kupokea pesa za wazungu wanaosaidia community ya jamii husika..

Kitenge alivyopresent tatizo utadhani kashushwa kutoka mbingu ya saba na ndio kaja na utafiti wenye majibu.

Agenda aliyokuwa nayo anaijua yeye na boss wake aliyemtuma.!

Sent using Jamii Forums mobile app
Well said!
NCAA wamelewa mapesa ya watalii.
Kwa sasa watalii wengi hawafurahii wanchokiona. Wenyeji nao malalamiko yamezidi!
Mafungu ya kuandaa GMP wanatafuna mwisho wa siku monitoring na evaluation zinasua sua!

NB: Kitenge ni mpuuzi kama wapuuzi wengine kwenye hizi redio za makelele! Kwenye hili hasiachwe hivi hivi!
 
Well said!
NCAA wamelewa mapesa ya watalii.
Kwa sasa watalii wengi hawafurahii wanchokiona. Wenyeji nao malalamiko yamezidi!
Mafungu ya kuandaa GMP wanatafuna mwisho wa siku monitoring na evaluation zinasua sua!

NB: Kitenge ni mpuuzi kama wapuuzi wengine kwenye hizi redio za makelele! Kwenye hili hasiachwe hivi hivi!
Sasa kama monitoring zina sua sua kitenge ana Kosa gani kureport???? Bila kitenge kusema tungejuaje ngorongoro mamlaka zinakwama kufanya monitoring ya wamasai?? Mambo yanaenda mrama akiripoti mtu anaonekana mbaya...
 
Sasa kama monitoring zina sua sua kitenge ana Kosa gani kureport???? Bila kitenge kusema tungejuaje ngorongoro mamlaka zinakwama kufanya monitoring ya wamasai?? Mambo yanaenda mrama akiripoti mtu anaonekana mbaya...
Tatizo la Kitenge na Oscar wake wameripoti bila kuwa na basic facts. Wameripoti kama kutaka kuwaonea "wakazi" wa NCA. Hakuwa well informed make huwezi kupinga uwepo wa mifugo na watu ndani ya NCA.
Pili hili jambo tumelipigia kelele humu kwa miaka mingi sana! Kwa uzoefu wangu mifugo mingi inaletwa na "wageni" wakiwemo staff wa NCAA. Udhaifu wa NCAA pia unasababisha ujenzi makazi holela ya wenyeji hifadhini.

NB: Hili la mifugo na "wakazi" ni trela. Muvi nzima ipo kwenye ugawaji holela wa maeneo ya kambi na lodges za watalii. Funga kazi ni ubadhirifu na ukwapuaji wa fedha za NCAA.
Turuhusu mjadala mpana wenye ripoti za kina badala ya taarifa za gengeni kama ile ya Kitenge!
 
Utakuwa na jinsia mbili hueleweki kama popo.
NCA hawaja ona athari za mmasai za kutishia kutoweka kwake.
Kama zipo zitaje na chanzo chako?
Nilifikiri una akili timamu za kuongea hoja bila kujidhalilisha kwa maneno na misemo iliyo kinyume na Mila na Desituri za Kitanzania. Usiongee maneno ambayo hhuwezi kuyatamka mbele ya Wazazi wako.
Wosia huu utakusaidia sana katika maisha yako.
 
Back
Top Bottom