Maulid Kitenge, propaganda ulizotumwa kuzifanya kwa wana-Ngorongoro hazitakuacha salama

Wamasai wanaishi Ngorongoro kwa mujibu wa sheria,hawapaswi wala hawawezi kuondoka.
Your browser is not able to display this video.
 
Lazima uwepo mkakati wa kuitunza Ngorongoro
Kwani nani kaiharibu Ngorongoro? Nini kimeharibika Ngorongoro? Dunia nzima inapitia mabadiliko ya tabia ya nchi. Ukame kidogo tu ulioikumba nchi nzima, wanaokula kupitia NCAA wakapaniki. Salaried guys ni tatizo sana.
Halafu hata kama ni kuzilinda hizi hifadhi zetu, sisi binadamu ndio priority. Sio Wanyamapori hata siku moja.
Itafika baadaye vizazi vijavyo itabidi kuwe na Zoo kwa ajili ya maonyesho ya wanyama.
Njaa zenu zinawafanya muone mnyama wa porini wa muhimu kuliko mwanadamu.
 
Habari za Magufuli wachana nazo maana tayari kashamaliza mwendo wake.

Ila ukae ukijua kuwa Ngorongoro lazima ibakie salama kwenye uhalisia wake.

Tunawajua watu kama nyinyi ndiyo mnatumiwa na maadui wa taifa kutaka kutukwamisha .
Mkuu asante kwa kuliona hilo Wanaviengio vya kipumbavu vinavyopata pesà kutoka kwa wapumbavu...WABAGUZI sana hawa nawajuwa sana wako Ololosokwani
 
kabugi nn kitenge simtu wampira mpira ameshaaza Tena na utalii jamani

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Na hapo si kwamba wanyama watakimbia tu.
Kuna jamii ya wanyama watatoweka kabisa.

Tunahatarisha maisha yao, maana wanakula mabaki ya vyakula vya viwandani vinavyotumika na binadamu.
Hali hiyo itawaletea maambukizi ambayo hatuna uwezo wa kuyadhibiti.

Ng'ombe kwakuwa tunaishi nao majumbani kila siku wanadungwa sindano kuwaponya na sumu zitokanazo na vyakula vyetu, hali itakuwaje kwa digidigi, nyumbu, twiga na Simba?
Wahamishwe tu hakuna kuchekeana.
 
Kitenge amesukumwa na moyo wa kizalendo, hajatumwa.
Vitisho vyako havitafua dafu.
Hawa watu waandaliwe utaratibu mzuri wahamishwe.
Kama tumefanikiwa kuvunja nyumba zaidi ya alfu 10 Kipawa ili kujenga Viwanda na Uwanja wa ndege wao ni nani wasihame?
 
Kama ni kweli anafanya propaganda kwa masilahi ya mtu au kundi fulani, anajitafutia downfall. Watu wanamuamini kwa utangazaji wake kwa hili atajiharibia. Ushauri wa bure kaa kwenye ethics za shughuli zako uitunze heshima binafsi na ya fani yako.
 
Kitenge amesukumwa na moyo wa kizalendo, hajatumwa.
Vitisho vyako havitafua dafu.
Hawa watu waandaliwe utaratibu mzuri wahamishwe.
Kama tumefanikiwa kuvunja nyumba zaidi ya alfu 10 Kipawa ili kujenga Viwanda na Uwanja wa ndege wao ni nani wasihame?
Argument ya kijinga!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao wanaozurura na ng'ombe wafanye ufugaji wa kisasa, dunia ya Sasa majitu yanazagaa na mifugo
 
Huyu Kakubali kutumiwa kwa maslahi ya Walaji wachache pale NCAA.

Hili lilishatokea kipindi cha nyuma utawala wa JMKikwete aliruhusu operation ya kusafisha maeneo ktk hifadhi na kusababisha mauaji ya watu wengi sana, askari waliwalawiti vijana mbele ya wazazi wao, mabint walibakwa, watu walikuwa wanatundikwa kama digidigi...

Maulid anafanya kampeni ambayo hajui athari yake hapo baadae.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ecosystem ya Serengeti inategemea sana Ngoro2 na hasa eneo la Loliondo. Masai si jangili ila makundi yenu ya ngombe yanaharibu vyanzo vya maji ktk eneo hilo muhimu kwa mazalia ya nyumbu na ecosystem nzima. Subiri uone
 
Hao wanaozurura na ng'ombe wafanye ufugaji wa kisasa, dunia ya Sasa majitu yanazagaa na mifugo
Kwa hiyo hata machinga waache kuzurura na bidhaa za kina Bakhresa, Mo, Muzar, GSM and the like?
Kuzurura nini?
Kuchunga ng'ombe ni sawa na kuzunguka na dala dala yako mjini kutafuta hela. Ni sawa na kuzunguka na boda boda yako. Ni kazi tu zimetifautiana.
Tatizo lako unatumia akili za kushikiwa na kucheza ngoma inayopigwa na wengine.
Inakukera nini mtu kuzunguka na mali yake?
 
Kuchunga mifugo haina tofauti na kuzurura mjini kufuatilia michongo yako au kusambaza CV. Acheni kuwaondoa watu akili.
Nchi kibao wanachunga. Jamii ya Wafulani nchini Nigeria, Wasomali wa Kenya, Somalia na Ethiopia, Wahindi kule kwao, Wasukuma, Wakurya, Wanyaturu, Wairaq, Wabarbaig etc.
Acha kutumia kichwa kama kopo wazi ambalo laweza kujazwa chochote.
 
Mkuu usiumize kichwa chako kubishana na wapuuzi wanaopenda kuhurumiwa kishwamba. Watu wamevunjiwa na kuachwa nje na familia zao kupisha "upanuzi" wa barabara sembuse masai hawa wanaoguga kwa kukodishwa ng'ombe na wakenya ili waharibu hifadhi zetu.
 
Duu! Ni vizuri ukituwekea hapa ushahidi wa hayo matendo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…