Mzee wa Minyama Maulid Kitenge amesema amezungumza na Rais wa TFF, Wallace Karia, ambaye amemhakikishia kuwa si wachezaji wa Yanga SC pekee walioruhusiwa kuondoka kambini Taifa Stars nchini Morocco.
Baada ya mchezo wa Taifa Stars dhidi ya FAR Rabat, wachezaji wa Yanga, Simba SC na Singida Black Stars na timu nyingine waliopo kambini wataruhusiwa kurejea kwenye timu zao kwa ajili ya maandalizi ya michezo yao.
Awali, taarifa iliyosambaa ilieleza kuwa TFF imewaruhusu wachezaji wanne wa Yanga, Mudathiri Yahya, Ibrahim Hamad Bacca, Seleman Mwalimu na Mohamed Hussein, kurejea Dar es Salaam ili kujiandaa na Kariakoo Derby dhidi ya Simba SC itakayochezwa Oktoba 10, 2026.
Soma TFF yaruhusu wachezaji wa Yanga kuondoka Kambini Morocco
Hata hivyo, Kitenge amesema mazungumzo yake na Karia yameweka wazi kuwa utaratibu huo hauwahusu Yanga pekee, bali pia wachezaji wa timu nyingine waliopo kwenye kikosi cha Taifa Stars.
Chanzo: Kitenge Tv