Tetesi: Maulid Mtulia anataka kugombea Jimbo la Kinondoni kupitia CCM baada ya kujitoa CUF

Wewe umesaliti vingapi mbona hujapigwa risasi. Hata wazazi wako umewasaliti wamekupiga risasi, haya ngoja watoto wako watakapokusaliti uwapige risasi.

Sasa umeandika nini hapa?Stupidity is within you.Akili za kiccm ni hatari kwa ustawi wa nchi hii.
 
Sasa umeandika nini hapa?Stupidity is within you.Akili za kiccm ni hatari kwa ustawi wa nchi hii.
Utashi wako wa kufikiria ni mdogo mno, ndio maana unakimbilia kutukana. Hivi mtu akiamua kufanya na wewe unavyotaka ni msaliti? Kwa nini usiheshimu mawazo yake, hivi binadamu tunafanana kwa kila kitu? Kama ingekuwa hivyo basi pasingekuwa na vyama vya upinzani au migawanyiko ya kisiasa, maana wote tunazungumza lugha moja. Hivyo jifunze kuheshimu mawazo ya wenzako kama wazazi wako walivyoheshimu mawazo yako wakati umebarehe!!
 
Sasa kama bado anautaka ubunge,kilichomfanya ajiuzulu ni nini ?stupid kabisa huyu Abdallah.
 

Umebarehe=Umebalehe
 
Ccm watamnyoosha kwenye kura za maoni tu.

Hana ubavu wa kushindana na wana ccm ndani ya ccm, kama ana ndoto hizo asahau kabisa.
 
Kodi zetu zinachezewa sana jamani. Haingii akilini kuwa unamuunga mkono Mh. Rais kwa kuliingiza taifa hasara ya kurudia uchaguzi
 
Mimi nataka kuacha kazi ya ualimu ili kuunga mkono utendaji kazi wa mkuu wangu wa shule
 
Huyo Mbunge kama ni kweli anataka kugombea tena ,
Anatakiwa achukuliwe hatua kali kwa kuliingizia taifa hasara, kwa kasababu kuandaa uchaguzi ni hela ya mlipa kodi inatumika ,
Utakuwa ni ukichaa kumruhusu agombee pale pale alipoamua kujivua anachotaka kugombea tena.
 
Mimi nataka kuacha kazi ya ualimu ili kuunga mkono utendaji kazi wa mkuu wangu wa shule
Utatupa hasara ya kulipia tangazo la nafasi yako, kufanya usahili na muda wa huyo mpya kujifunza mazingira ya shule (learning curve). Usiache kazi ongeza bidii katika kazi zako utakuwa umemuunga mkono na kuninua shule yako kitaaluma
 
Msingi wa kurudi kwake CCM ni kumuunga Mkono Rais, kupata au kukosa Ubunge ni Matokeo tu

Aache tamaa zake za kifala, yeye ameshalipwa mpaka kiinua mgongo chake amabacho angelipwa 2020 sasa awaachie wafia chama nao waambulie.
 
Yy kwanza amalizane na wananchi wake kwa jinsi alivyowaacha ni dhahiri hawakumuelewa na sidhani kama watamrudisha bungeni huyu kijana.. Pole yake
 
Watanzania tuwapole sana,kuchaguliwa tena ubunge kwa tckt ya ccm hayo ni sawa na matusi kwa wapiga kura wAke
 
Sasa kama mtu anasema kuna mpango wa kumuweka. Unadhani nani atamtoa.
 

Yaani wewe una amini kabisa katika hili rais wetu "mbana matumizi" hausiki? Tumefika kwenye siasa chafu na za kibinafsi sana ambazo sio tu zina teketeza pesa na rasilimali nyingine za taifa letu (kupandikiza sababu zisizo za msingi za kurudia chaguzi) , bali pia zitakuja kugharimu maisha/ uhai wetu muda si mrefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…