Do you know something known as 'Sexpionage Operation for Sexual Entrapment or Honey Trap? Do you know how it works?
'Mtego wa Asali' ni mbinu maarufu Sana nchini Urusi ambayo huwa inapangwa na kuratibiwa kitaalamu na Mawakala wa Siri wa ujasusi wa KGB/FSB. Walengwa na wahanga wakubwa zaidi wa mbinu hiyo chafu ni Wapinzani/wakosoaji wa Serikali, Mabalozi wa nchi za nje na Wanadiplomasia wa kimataifa, Wanasiasa maarufu, Viongozi wa Serikali ambao hawatakiwi au ambao wameingilia maslahi binafsi ya watu fulani fulani, na watu wengine maarufu kwenye jamii Kama vile Wafanyakazi au Wafanyabiashara maarufu, Viongozi wa dini, n.k. Lengo la kuwafanyia kampeni chafu za namna hiyo ni kuwachafua na kuwapunguzia makali ya umaarufu, kuhataribu kabisa hadhi zao kwa jamii au kuwapunguzia ushawishi katika jamii, kujaribu biashara zao ni mwisho kabisa kuwafanya Watu hao kuwa Watiifu kwa Serikali hata kama kufanya hivyo kunakwenda kinyume na dhamiri zao za moyoni.