Maulid ni sawa na saa mbovu. Tumuache.
Mkuu, umenena vyema, bahati mbaya ni kuwa watanzania wachache wanao muda wa kufanya tafakuri tunduizi. Naomba ijulikane mapema kuwa siko upande wowowte katika suala hili.
Umeongea vyema kuhusu nyaraka za siri. Leo kuna story za Julian Assange na Snowden, lakinj sijui kama tumesahau au tumejifanya hivyo kwa maslahi?
Gazeti la mwananchi, bila kupindisha maneno limetumika ndivyo sivyo kuhusu suala hili. Uongo mwingi uliochanganywa na ukweli kidogo, umetumika kuwaaminisha watu kile wanachotaka.
Katika habari yao weledi umewekwa kando. Hatuoni mahali ambapo mtuhumiwa amepewa nafasi ya kujitetea. Habari yote imejaa maelezo yanayolenga kumfanya, mtujumiwa ni mkosaji lakini hakupatikana hata mmoja wa kueleza vinginevyo.
Gazeti hilo linadai, tayari Sampuli za DNA za mwanamke huyo zimechukuliwa zikisubiri za mtuhumiwa. Hawa tayari wana uhakika na madai yanayotolewa.
Kuweka rangj katika mfupa ulioundwa wanapatikana watu walioshuhudia tukio hilo mwanzo mwisho. Lakini mashuhuda hao walishindwa kutoa msaada, wakasubiri uchuguzi wa Mwananchi ndio waelezee tukio.
Mwananchi ninyi, uandishi huu unastahili zawadi. Kwamba chanzo kingine kilichoko ofisi nyeti Dodoma, kimedai baada ya kufika kwenye gari, mtuhumiwa akatimiza haja zake!
Yaani mfanyakazi aliyeko ofisi nyeti tena Dodoma alishuhudia hilo tukio, badala ya kutoa taarifa Mza akaenda Dodoma kumsubiri mwandishi wa mwananchi mwenye uwezo wa kutabiri, mtumishi wa ofisi nyeti aliyekuwa mwanza siku ya tukio na alishuhudia kilichotokea.
Tujiulize, binti alibakwa the cask ghana, akaenda km zaidi ya 25 Malimbe. Vipi maeneo yote hayo alipita hospitali na vituo vingapi vya Polisi.
Kufika Malimbe akavua nguo na kulala kwa siku mbili katika chuo kinachofundisha kozi ya sheria na katika wakati huu ambapo elimu ya nini ufanye au usifanye ukikumbwa na hali hiyo inatolewa kila mahali.
Kwanini, mwananchi wanatoa habari za upande mmoja hivi?