Lakini suala hili la huyo RC ukiliangalia kwa jicho Kali la 'mwewe' utagundua kwamba ni kweli mtu huyo ametengenezewa skendo ili kumharibia sifa za kuendelea kuwa Mkuu wa Mkoa na kumharibia maisha yake yote kabisa. Ni muhanga wa targeted Sexpionage Operation and Sexual Entrapment/Honey trap.
Jaribu tu kufanya simple intelligence analysis kwamba ilikuwaje Nyaraka za Siri ( Classified Documents) ambazo Zina sensitive information za kutoka kwenye mamlaka ya Upelelezi Kama Jeshi la Polisi zivujishwe kirahisi namna hii humu mtandaoni??
Hii inawezekanaje?? Kitendo cha Kuvujisha Nyaraka za Siri za namna hii kwa mujibu wa Sheria za usalama wa Taifa katikà nchi yoyote ile hapa duniani inahesabika kama kosa la Uhaini, na katika nchi nyingi sana adhabu yake kwa kosa Kama hilo ni Kali Sana ikiwemo na kunyongwa Hadi kufa. Katika taasisi za kijeshi Kama Jeshi la Polisi watuhumiwa huwa wanapelekwa kwenye Mahakama za kijeshi (Court Marshall) na Kesi zao huendeshwa haraka sana na hatimaye wahusika wamekuwa wakinyongwa haraka kabisa. Sasa, Je, Askari Polisi aliyevujisha kwa umma hizo documents za Siri mmesikia kwamba tayari amekamatwa na Jeshi? Kwa nini?