Maumivu kwa wenye magari: Utaratibu mpya wa kulipia road licence, Gharama za fire zaongezwa

Maumivu kwa wenye magari: Utaratibu mpya wa kulipia road licence, Gharama za fire zaongezwa

Siku ikifika ya kuingia barabarani kuipinga serikali kwa kusababisha hali ya maisha kuwa magumu ,usibakie nyumbani na kuchungulia dirishani.
 
Unajua hii trend ni very worrying. Ni sawa na kile ambacho "marepublicans" kule marekani wanakipinga cha kuwageuza matajiri au watu wenye uwezo ndo mfuko wa serikali. Hii kodi naipinga na haitakiwi iwe kodi. Kwanza ni kuiongezea mamlaka ya TRA mizigo ya kukusanya mapato mengine ambayo si kodi na hivyo kuiongezea gharama za uendeshaji na kumzidishia mzigo mlipa kodi.

Hata kama wenye magari wana uwezo, ni vibaya na haifai kuwageuza mahali rahisi pa serikali kuchota fedha. Hii "overall" inaharibu uchumi. Hizi kodi kwa wenye magari baadaye zitageuka kuwa eneo jingine la kuongeza gharama za maisha, full stop. Wenye magari wengi kwa namna moja au nyingine wana jinsi ya kuihamishia kodi hiyo kwa walaji wengine wa chini zaidi.

Hayo mapato si kodi, kwa nini yakusanywe na TRA mamlaka ya kodi? Kuna sheria archaic inamtaka kila mwenye gari kuwa na fire extinguisher! Naiita hii sheria archaic kwa sababu hakuna ushahidi wowote wa kuthibitisha kuwa sasa hivi moto kwenye magari ni tatizo! Hata pale ambapo incidences za moto zimekuwa zikitokea, hizo fire extinguisher hazitumiki kwani ama zimesha-expire au watumiaji hawajui jinsi ya kuzitumia, au kutokana tu na jinsi moto ulivyotokea imekuwa ni vigumu kuitumia hiyo fire extinguisher sababu pengine mwenye gari hakuwa karibu au fire extinguisher haipo mahali inapoweza kupatikana kirahisi. Ni kuwa kwa kifupi, magari ya kisasa hayaungui ungui ovyo kwa sababu ya design za kisasa kiasi kwamba sheria hii ya kulazimisha fire extinguisher haina maana yoyote kuendelea kuwepo. Nipe hata case moja katika miaka mitano iliyopita ambapo ulitokea moto kwenye gari ukazimwa na fire extinguisher!! Sheria hii imebaki ni mradi wa askari wa usalama bara barani kujichukulia rushwa tu kwa wenye magari wasio na fire extinguisher!

Idara ya fire imebaki na hiyo biashara ya kuuza na kukagua fire extinguishers za magari kwa kuwa wenye magari ni wenye uwezo kidogo, wameona kuwa hapo hapo ndo pa kulalia. Idara ya fire inatakiwa iendeshwe kama idara nyingine zinavyoendeshwa. Hii neglect inayofanywa na serikali kwa idara hii imewafanya wawe wajasiriamali wa kuuza fire extinguishers. Sasa in the face of competition, hawawezi. Wameona kukagua fire extinguisher ndo mandate ambayo haina mpinzani kwa hivyo wakaona watumie tra kuwafanyia kazi ya kukusanya mapato kukagua fire extinguishers ambazo kusema ukweli kwenye asilimia tisini ya magari hazipo; ama zipo feki za kichina zinazouzwa mitaani kama njugu, kwa lengo la kukwepa harasment za traffic. Ukweli ni kwamba, fire watakusanya hizo fedha, sticker watatoa, ila hamna kitakachoendelea.

Kinachoendelea ni ile ile harassment ya serikali kwa watu wanaoonekana wana kipato. Fire ni idara ya serikali inayotakiwa ihudumiwe na kodi zetu. Sio wajiendeshe kwa kufanya uchuuzi wa fire extinguisher na kukusanya ada za kukagua fire extinguisher kwa nguvu. Sheria ya kumlazimisha mwenye gari kutembea na fire extinguisher haina maana tena. Hakuna moto kwenye magari. Moto uko kwenye majengo. Hamishieni kodi hizo kwa wenye nyumba.

Huu uzembe eti wenye magari wana fedha kwa hiyo kulipa elfu thelathini kwao si issue uishe. Hata hiyo elfu thelathini wenye magari wameipata kihalali acheni waitumie kwa matumizi wanayopenda wao; si kulazimisha kodi na ada zisizokuwa na maana yoyote! Mizigo ikizidi kwa wenye uwezo, wanashindwa kuwekeza kwenye miradi midogo midogo ambayo ndo inayotoa ajira kubwa kwa watanzania wengi; miradi kama ujenzi wa nyumba mitaani, utengenezaji wa magari kwenye gereji, n.k. Tozo za serikali zisizidi sana!
 
ujumbe ni kwamba kama hela yako haijatimia usinunue gari, otherwise unatoa wrong impression kuwa unazo kumbe kabwela tu. duniani kote wene kipato kikubwa ndio wanaolipa kodi kubwa..siitetei serikali lakini ukweli wa mambo ndio huo.

ukiona tabu uza gari yako upande toyo..

hii ni tofauti hapa kwetu mbna wengi wanacho lakini hawakilipii kodi mwenye kidogo ndo anaekilipia hyo kodi au ndo udhaifu wenyewe unaosemwa

Naona kama hapa ni malumbano kati ya wala kodi na walipa kodi Hebu tuone.
 
poor thinking,ukiwa na gari ndiyo kuwa na kipato kikubwa,yale yale ya ukiona foleni kubwa ya magari ndiyo kukua kwa kiwango cha maisha bora kwa watz. sio kodi ni ADHABU YA KUMILKI GARI TZ.
unakurupukia kujibu post usiyoielewa..
typical mdanganyika lacking analytical skills..
 
Jibu la kijinga au la wivu. HII KUMBUKA ITAKWENDA HADI KWENYE PUBLIC TRANSPORT NA ITAPELEKEA KUPANDA KWA GHARAMA YA UENDESHAJI NA MATOKEO YAKE NI NAULI KUPANDA PIA ITAONGEZ GHARAMA YA USAFIRISHAJI INGENERAL. NANI ANAUMIA HAPA KAMA SI WATANZANIA WOTE REGADLESS UNAGARI AU HUNA?
TRY TO BE SMART
jibu la kijinga au wewe ndio mpumbavu? chunguza tatizo vizuri.
 
poor thinking,ukiwa na gari ndiyo kuwa na kipato kikubwa,yale yale ya ukiona foleni kubwa ya magari ndiyo kukua kwa kiwango cha maisha bora kwa watz. sio kodi ni ADHABU YA KUMILKI GARI TZ.[/QUOTE=BOra wewe umesema busara ya mtu huonekana maneno yamtokayo moyoni mwake huyu jamaa kaamua kuwa kituko kwa majibu yake,hasira za nyumbani anazileta jf.
 
mi nashangaa kilio chote cha nini kwa 'mmiliki wa gari', ingekua mmiliki wa pikipiki nisingeshangaa.. hahaa..

Haya ni mawazo ya miaka ya 70. Mtu akiwa na gari anaonekana ni tajiri. Gari siku hizi si Luxury ni necessity. Tungekuwa na reliable public transport ningekubalina nawe kuwa hakuna haja ya kumiliki gari.

Unajua serikali ya Tanzania ya ajabu sana, badala ya kuweka misingi ya kukuza uchumi na uzalishaji ambao untaongeza tax base wao wanang'ang'ani kukamua walala hoi. Kuna makampuni na wafanyabiashara wakubwa sana wanakwepa kodi kwa kushirikiana na viongozi waliopo serikalini. Hali hii inanikumbusha siku za mwisho za uongozi wa Alhaj Ali Hassan Mwinyi. Afisi kuu ya nchi ikiwa inaendeshwa na mtu asiyetaka lawama wala kuonekana mbaya kwa maswahiba wake matokeo yake ndiyo haya.

Bado kurudisha kodi ya kichwa au kutoza kodi ya Oxygen kwa wanaoishi, ukifa unapata bahati ya kuwa exempted, ambayo nayo utahitaji kupeleka cheti daktari kuwa wewe ni marhum.
 
huwezi kuelewa kama huna gari....
nice try..
sticker haizimi moto...
wewe ulitegemea izime?
unaenda pale samora unalipa hiyo sticker nao hawauzi hiyo fire extinguisher wana kupa kikaratasi cha kubandika gari hawataki kuiona
ukisafiri mikoani wapo trafic wanakusimamisha na na pembeni kuna jamaa wana mitungi ya fire wanauza
hata ukiwa nao wana kulaimisha unune yao kisa ati ule haufai !
tra waione yanini,ili iweje? wao sio kazi yao. kazi yao ni kukusanya mapato!
usitetee jambo la uonevu
uonevu? kulipa kodi ni uonevu?
kodi hutozwa kwenye income
sio kila mahala inatozwa kodi
umejijibu mwenyewe!
na sio sahihi wenye magari kulipa gharama za mamlaka ya fire
moto unatokea zaidi kwenye majumba, viwanda kuliko kwenye magari
inachotakiwa ni wenye magari waweke vizimio sio kuwakamua
serikali yako tukufu inaanza kwanza kwene magari..
gari sio anasa ndugu yangu
kodi pia sio anasa, is very essential..
nikuulize kitu kimoja tu...kama kweli hawa watu makini katika kukusanya kodi kwa nini kwenye madini wanakua kama matahira vile(ashakum sio matusi)
  • nchi ina madini kibao anakuja mtu anapewa achimbe achukue yote
  • fedha zote zitokanazo na hayo madini zinakaa njee ya nchi
  • fedha zinaletwa hapa ni kwa ajili ya mishahara na uendeshaji
  • gold yote inawekwa kwenye hazina yao hayo makampuni yanayopewa ardhi kuchimba
  • akiba ya gold ya tanzania hai ongezeki kutokana uchimbaji huu
  • na juu ya hayo equipments zote za miradi hii hailipiwi kodi
  • na kubwa zaidi MAFUTA yanayotumika katika mitambo yao na kuzalisha umeme nao hawalipi kodi

hawa hawalipi kodi....hawa wapo sawa..ila watanzania wanyonge tunayalipia ushuru magari yetu yanapoingia , tunalipa road licence kila mwaka , vijibiashara vyetu tunavilipa kodi lakini kama haitoshi tunalipishwa kodi ya karatasi ya fire kuzidi kukamuliwa

serikali inayojali inaweka wananchi kwanza sio wageni kwa jina la investors

waambie wakajifunze kwa Chavez wa Venezuela, wajifunze Brazil, Peru , India na hata Afrika Kusini...uwaulize kama wanatoa rasilimali zao kwa bure kama hivi

hili si la Kikwete..ni la mfumo mzima mfumo wa ubinafsi...unaojali masklahi binafsi
/
all well, pengine ungeona haya mapema na kuishauri serikali yako sikivu ya Kikwete, labda wasingekaba huku kwene stika za fire..ulipokua ukimtetea (i bet hata sasa is still a saint kwako) hukujua haya? usiseme ni mfumo, maana yeye ndio bosi wa kusimamia huo mfumo!
 
Hata kama mwenye gari anazo, ni zake, si za serikali kuchukua tuuu. Haya ni mawazo ya kikomunisti kuwa wenye mali ndo tatizo kwa hiyo kila siku zinatungwa kodi za kijinga jinga tu kwa lengo la kuwakomoa wale wanaoonekana kuwa nazo.
 
Haya ni mawazo ya miaka ya 70. Mtu akiwa na gari anaonekana ni tajiri. Gari siku hizi si Luxury ni necessity. Tungekuwa na reliable public transport ningekubalina nawe kuwa hakuna haja ya kumiliki gari.

Unajua serikali ya Tanzania ya ajabu sana, badala ya kuweka misingi ya kukuza uchumi na uzalishaji ambao untaongeza tax base wao wanang'ang'ani kukamua walala hoi. Kuna makampuni na wafanyabiashara wakubwa sana wanakwepa kodi kwa kushirikiana na viongozi waliopo serikalini. Hali hii inanikumbusha siku za mwisho za uongozi wa Alhaj Ali Hassan Mwinyi. Afisi kuu ya nchi ikiwa inaendeshwa na mtu asiyetaka lawama wala kuonekana mbaya kwa maswahiba wake matokeo yake ndiyo haya.

Bado kurudisha kodi ya kichwa au kutoza kodi ya Oxygen kwa wanaoishi, ukifa unapata bahati ya kuwa exempted, ambayo nayo utahitaji kupeleka cheti daktari kuwa wewe ni marhum.
kwa mtu mwene gari tz, 30--50K per year is nothing. mafuta yenyewe ni 2+K kwa lita..tusikuze mambo.
 
kwa mtu mwene gari tz, 30--50K per year is nothing. mafuta yenyewe ni 2+K kwa lita..tusikuze mambo.

Hujaelewa point yangu. Issue si materiality of the amount. Issue ni kwa nini wacharge?. Kila kitu kinataka justification, Mimi nime insure gari yangu kwa fire and safety. Nina kila kitu stahili kwa nini serikali iniwekee masharti ya kukaguliwa na chombo chake? tena kwa hela? is Tanzania a free country or we are living in a dynasty of tyrannies. What if wakianza kusema waliooa nao walipie maternity charges kila mwaka kwani wanaweza wapatia ujauzito wake zao na kwenda jifungulia muhimbili.

Binafsi huwa ninajisikia mwenye amani sana ninapolipia kitu hata kwa mamilioni ambacho kipo justified kuliko kulipia kitu shilingi mia kwa hila. Kuna siku nilienda Black point kula jamaa wa vinywaji akaniletea Juice ambayo bei yake ni mia tatu akaniambia nilipe mia tano, nikampa, nilipoagiza mtu mwingine akaniambia mia tatu nikampatia mia tano na kumwambia a keep change ila yule wa mwanzo nilimtafuta na kumdai akalia sana nimsamehe kwani anaweza fukuzwa kazi. Sikumsamehe mpaka nikamuita meneja wake.

Hakuna kitu kibaya kama hadaa. Kwa mawazo yako wewe upo tayari bank kukukata alfu kumi kila mwezi ambazo hazina maelezo kwa kuwa tu kwenye account una millioni mia tano.
 
Back
Top Bottom