Maumivu ninayopata haijawai tokea, nisaidieni namna ya kupata nafuu

Maumivu ninayopata haijawai tokea, nisaidieni namna ya kupata nafuu

Siwezi kumlaumu mtoa mada, nyinyi nyote mnaomkebehi hata kesho zenu hamzijui. Hujui utaangukia kwa nani, msiongee kama maisha mmeyamaliza wakati bado mnavuta pumzi.


Niliwahi kuongea hivyohivyo, nikaambiwa hujapenda ndiyo maana nikipenda nitakaa kimya mwenyewe. Mungu si Athumani, nikaja kupenda kufa kuoza. Nilipokuja kupigwa chini nilikaribia kupagawa, nili move on kwa kuhakikisha ninamsahau tu.


Hivyo Mtoa Mada kama unataka umsahau ili upige hatua mbele, inabidi uondoe kila kitu ambacho kinakufanya umkumbuke. Hivyo vitu vyake kuwa na msimamo wa kueleweka, mwambie aje kuchukua la si hivyo unaviharibu, kuvitupa au kuvigawa. Muwekee deadline kabisa kuwa serious unapomwambia, ikifika siku hiyo hajaja viondoe. Maana ndiyo vinakukumbusha kuhusu yeye, huwezi kumsahau kama vipo.
HAPA KAMA KWELI ANAMAANISHA MWACHANE ATARUDI NA KUVICHUKUA, KAMA ANAKUPIMA IMANI ATAREJEA PIA ILA ATAFANYA KILA HILA ASIVICHUKUE ANAJUA KAACHA KUMBUKUMBU.




KAMA KESHACHUKUA VITU ENDELEA SASA;
Picha zote mlizokuwa pamoja ziondoe, ubaki kama ulikuwa humjui. Pia kama una simu ndogo ya kawaida tumia hiyo, smartphone fungia kwa wiki tatu au mwezi hivi kama hiyo whatsapp usioone kama haina tija kwako zaidi ya kuchat. Ukisema ubaki nayo utajikuta umeingia huko na kusoma hivyo vijembe tu, dawa ni kukaa mbali na simu.


Muda ambao mliokuwa mkiutumia kuwa pamoja, jaribu kutafuta kitu kingine cha kufanya. Mazoezi ya viungo ndiyo yanafaa zaidi, nyakati nyingine kuwa active kwenye kazi kuliko kitu kingine. Ukiwa kwako utahitaji kupumzika kuliko kitu chochote, hutoweza kumkumbuka tena maana huo muda wa free kwako utahitaji kupumzika tu na si kufikirisha akili.


Kipindi unajaribu kumsahau, tafadhali sana usijihusishe kimahusiano na mwingine. Hata kama utamsahau usikimbilie kuanza mapenzi mapya, pumzisha moyo na akili kiupande wa mapenzi.

HUWEZI JUA MUNGU KAKUEPUSHIA NINI ALIPOKUACHA, PIGA KAZI UJIONGEZEE KIPATO
Asante sana ndugu kwa kunielewa.
 
Ndo shida ya kuanza mahusian na utuuzima kwa bint aliye kubuh halaf unatak kuishinae
 
eti naumia kwani kuna mtu amekupiga!mi jitu likisema linaumia sbb y mapenz nashangaa sn.
 
Ndugu zangu mpenzi wangu ameniacha. Sijamkosea chochote ameamua tu kuondoka mbaya zaidi ananikashifu na kunipiga vijembe kwenye WhatsApp status zake.

Mwanzo nilidhani masihara lakini naona yupo serious ameondoka ameenda kwa mwingine. Nisichojua ni kwamba nimemkosea nini nilijaribu kumuuliza akanijibu vibaya akishajibu vibaya anani text tena nimsamehe mimi na yeye hatujagombana anaomba tusiwe na ugomvi.
Kwa kweli sijui kosa langu japo sometimes tulikuwa tunagombana anasema namfatilia sana simuamini. Mimi nimemkaushia japo naumia anataka kuja kwangu kuchukua vitu vyake nikitaka nivipeleke kwake au somewhere anapoweza vichukua ataki anataka avifate kwangu nikikataa anatoa lugha Kali, kwa hili pia sielewi lengo lake .

Kingine mimi nimeamua kumsahau lakini aachi kunipiga vijembe Watsapp ananichoresha kwa watu as if mimi kwake nilikuwa nothing japo tumepitia mengi mazuri.

Kiukweli inaniumiza inaniumiza kwa kuwa kaondoka wakati bado nampenda na inaniumiza zaidi hivyo vijembe vyake wakati mimi nimekaa kimya simjibu.

Nipeni ushauri kwenye mawili

Moja, nifanyeje ili nimsahau mapema ni-move on.

Pili, kama na mimi nikilipizia nitakuwa nakosea kumrusha roho pia?
una muandiko wa kike halafu we ni dume..... utakua mashallah
 
Shukran kwa ushauri
Tayari umepatiwa ushauri mzuri sana hapa. Lakini naongezea ushauri mdogo kuwa tafuta mpenzi mwingine utamsahau huyo wa mwanzo kabisa. Na akisikia una mpenzi mwingine mnapendana sana ataanza kukutafuta kuomba mrudiane na wewe usikubali.
 
Back
Top Bottom