Mkuu ni vizuri kwanza ujue sababu ya kuumwa na kichwa mara kwa mara kwasababu kinaweza kusababishwa na vitu vifuatavyo
-Kuna kichwa kinauma kwasababu ya kuwa na stress au mawazo sana
-Kwasababu ya ukosefu wa maji ya kutosha mwilini (kwani maji ndio yapo kwa% kubwa ktk damu ikipungua sana mishipa inapata tabu ktk mzunguko na kusababisha maumivu)
- Kwasababu ya kushinda njaa muda mrefu
-Kutopata usingizi wa kutosha kwa siku kadhaa (hili utagundua kwani haya macho yanakuwa red)
-Pia kukaa mahali penye kelele kwa muda mrefu inaweza kusababisha
Jitahidi kujua kati ya hivyo hapo juu chako kinasababishwa na nini hasa.
ONYO: Usikimbilie dawa za hospitalini,hebu kunywa maji ya kutosha na pumzika/lala mahali palipotulia kwanza.