Watu huwa wanaamini wanaumia na kitendo ambacho kimefanywa na mtu mwingine, lakini hapana kiuhalisia watu wanaumia na FIKRA zinazotafsiri hicho kitendo hicho, hivyo unaweza chagua kuumia au kutokuumia kwa kubadilisha FIKRA zako juu ya kitendo ambacho kimefanywa na mtu mwingine, adui wa maumivu anatoka kwenye FIKRA zako mwenyewe zinazotafsiri kitendo ila sio kwenye kitendo chenyewe kilichofanywa, chukulia huu mfano watu wawili wamewafumania wake zao, mmoja akaweka FIKRA zake kwa dunia imejaa watu ambao sio wakamilifu hivyo akachagua kumsamehe mke wake huyu mme hataumia wala kuteseka na maumivu kabisa, ila mwingine akachagua kuwa na FIKRA kuwa kitendo alichofanya mke wake ni kibaya sana anatakiwa kupewa adhabu kali na kuchagua kushikiria ilo kosa kwenye FIKRA, hivyo matokeo yake atateseka muda wote kutokana na FIKRA zake mwenyewe zitazopelekea hasira, visasi na magonjwa yasiyoambukiza, kwa tafsiri ya mfano huo tiba ya maumivu ipo kwenye akili yako mwenyewe kwa maana kila kitu kinaanzia kwenye FIKRA zako hivyo maamuzi kuumia au kutokuumia unayo mwenyewe kama umechagua kuumia utaumia ipasavyo FIKRA zitakuletea kila hisia za maumivu mpaka unyooke si umekubali kuumia kama utaki kuumia badilisha FIKRA zako kwa kuangalia tunaishia dunia ya watu ambao sio wakamilifu maumivu hayatakusogelea kwenye FIKRA zako. Adui yupo kwenye FIKRA zako sio kwenye kitendo ulichofanyiwa