Maumivu ya viungo

Maumivu ya viungo

binty mzazi

Member
Joined
Jun 27, 2014
Posts
33
Reaction score
8
Habarini zenu. Naomba kujuzwa mtu anaeumwa sana viungo hasa joints za mikono, magoti na miguu, mgongo, kiuno na kichwa, kuna shida gani hapo? ni kuchoka sana stress au tatizo jengine?
 
Nashauri angalia sticky moja hapo,iko mwanzo tu ukifungua jukwaa hili unaiona, unaweza pata majibu yako japo bahadhi.
 
Jiangalie na mwenendo wa maisha yako. Kuna kitu kinakufanya uwe hivyo. Labda kazi ngumu unazofanya au unaumwa.
 
Habarini zenu. Naomba kujuzwa mtu anaeumwa sana viungo hasa joints za mikono, magoti na miguu, mgongo, kiuno na kichwa, kuna shida gani hapo? ni kuchoka sana stress au tatizo jengine?

DHIBITI MAUMIVU YA VIUNGO KIASILI ZAIDI



KATIKA makala yaliyopita nilipokea simu nyingi kutoka kwa wazee, wakilalamika na kuomba msaada wa tiba ya kupambana na tatizo la kuumwa viungo vya mwili. Lakini katika siku za hivi karibuni, siyo wazee tu, bali hata vijana pia wanasumbuliwa na maumivu ya viungo.

Wazee:
Kundi hili linajumuisha watu wa kuanzia umri wa miaka 45 na kuendelea. Idadi kubwa ya wenye matatizo ya maumivu ya viungo, huwa wamepoteza ile nyama ya plastiki kama tuliyozoea kuitafuna juu ya mfupa wa paja la kuku ambayo hukaa katika maungio ya mifupa ya binadamu kama sponji linalo kinga mifupa kugusana na kusagika, hasa sehemu za mgongo, kiuno, magoti na vifundo. Kitaalamu nyama hii hujulikana kama ‘cartilage'.


Wajawazito na wenye vitambi


Binadamu anapoumbwa hupewa mifupa kama fremu ya kumbeba kwa uzito uliokadiriwa kulingana na urefu wake na si vinginevyo. Tumewashuhudia akina mama wajawazito wakitembea kwa shida na hata kuanguka wakati mwingine kutokana na mifupa yao kushindwa kuubeba mzigo wa mtoto tumboni ambaye ni kama dharura kwa wakati huo.

Vivyo hivyo wenye vitambi nao hulalamika sana kuwa wanaumia sehemu za miguu, mgongo, nyayo na kiuno. Kitendo cha kuubadili mwili na kuwa na muonekano wa ‘V', yaani juu kukubwa chini kudogo, huifanya mifupa kushindwa kuubeba uzito wako na kukufanya usikie maumivu sehemu hizo tajwa.
Maumivu haya pia huweza kuwakuta watu wengine bila kujali umri, wakiwemo wagonjwa mahututi, waliopatwa na ajali, n.k. Hata hivyo, wengi hupatwa na matatizo ya viungo kutokana na mwili kukosa lishe inayotakiwa kuufanya mwili ujiendeshe wenyewe.


Tiba asilia za maumivu haya


Tiba za maumivu haya zipo nyingi, lakini leo nitazitaja tatu:
Mdalasini: Chemsha mdalasini na maji glasi nane kisha yaache yapoe, kunywa kidogokidogo kwa kutwa moja. Rudia zoezi hilo kwa siku 10 mpaka 15 na ndani ya muda huo utabaini mabadiliko mazuri, utatakiwa kufanya hivyo kila mara unapohisi maumivu.


Muarobaini:
Chuma na twanga majani ya muarobaini na uyakamue upate juisi yake robo ya glasi moja. Changanya juisi hiyo na maji ya kunywa glasi 7, kunywa kidogo kidogo mpaka yaishe kwa kutwa moja, kwa muda wa siku 10 mpaka 15.

ONYO:
Mwanamke Mwenye Mimba asitumie hii Dawa ya Majani ya Muarubaini.Tafadhali.

EsteoEze Gold:
Hii ni tibalishe maalumu ya vidonge (food supplement) ambayo ina ‘Glucosamine Sulphate' na ‘Chondroitin Sulphate' ambayo ukiitumia kwa mwezi mmoja kama ilivyo dozi yake, unaweza kupata nafuu ya muda mrefu. ‘Glucosamine' imethibitishwa na matabibu duniani kote

kuwa husaidia kujaza mapengo katika mifupa na ‘Chondroitin' hufanya ripea katika maungio yaliyosagika, kuzuia maumivu na uvimbe.

Miongoni mwa virutubisho vingine vilivyomo kwenye tibalishe hii ni pamoja na vitamin C na Manganese kwa wingi ili kurahisiha uponyaji na kumfanya mgonjwa ajisikie nafuu kwa muda mfupi sana. Kwa maoni na ushauri usisite kuwasilina nasi kwa namba iliyopo hapo juu.

UKIWA BADO HUJAPONA NA UNATAKA DAWA YA KUPONA KABISA NITAFUTE MIMI DAWA NINAYO KUNIPATA MIMI BONYEZA HAPA.
Mawasiliano

 
asante na mie ninasumbuliwa na maumivu ya viungo,ngoja nitumie sawa then nitaleta feedback.
 
unaweka mdalasini kias gan ktk hayo maji

mkuu achana na hizo habari za mdalasi wa mzizi mkavu...nenda hospitali inaweza ikawa ni rhematic fever baadae ikaja kukuletea complications za kwenye moyo, rhematic fever hua ina present na polyathrits (kuumwa na viungo tofauti tofauti), jaribu kwenda hospital mkuu huo ndo ushaurii wangu
 
mkuu achana na hizo habari za mdalasi wa mzizi mkavu...nenda hospitali inaweza ikawa ni rhematic fever baadae ikaja kukuletea complications za kwenye moyo, rhematic fever hua ina present na polyathrits (kuumwa na viungo tofauti tofauti), jaribu kwenda hospital mkuu huo ndo ushaurii wangu
Kaka nimeku DM unaweza kucheki au hapa pia naomba mawasiliano yako kuna vitu unaweza nishauri
 
Back
Top Bottom