Issuna
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 3,203
- 7,628
Naomba msaada wenu Madaktari na Kina Mama mlio na Uzoefu na Hii hali jamani,yani mke wangu Tangu ajifungue alikua ananyonyesha vizuri kabisa maziwa yote mtoto ananyonya bila shida yoyote ile mpaka anashiba analala.
Lakini Ghafla kuanzia Juzi maumivu yakawa yanatokea kila anapomnyonyesha mtoto ziwa la kushoto,yalikua kidogo kwa mbali akawa anamnyonyesha ivyo ivyo kwa shida,Jana hali ikaongezeka mtoto akigusa nyonyo yani hayo maumivu yake acha kabisa yani,ikabidi nimshauri asimnyonyeshe ziwa la kushoto atumie moja tu la kulia.
Basi akafanya ivyo jana jioni,usiku,mpaka leo asubuhi nikamwambia ebu jaribu kumnyonyesha tena tuone kama utasikia yale maumivu,alipompa tu nyonyo mtoto Yani alisikia maumivu kiasi kwamba ilibidi nimpokee mtoto akainama analia kama mtoto kwa dakika kama mbili ndio ziwa likaachia,hakika nilitamani kulia kwa jinsi mke wangu alivyoumia nashndwa hata yaelezea hayo maumivu.
Kwasasa yupo anatumia ziwa moja tu kumnyonyesha mtoto,lakini mimi bado sina raha kwani sitamani kuona mke wangu anateseka kama nina uwezo wa kumsaidia japo kimawazo,Niko na Mama angu na mama angu mkwe wote nawambia tumpeleke mke wangu hospitali eti wao hawataki wanasema ni kawaida hiyo hali itakuja kuisha yenyewe.
Sasa mimi nipo zangu kazini huku naombeni mwenye ushaufi au ambae alishawahi pitia hali hii au anaejua sababu ya hili tatizo na Tiba yake ni kitu gani,ili nitakapoudi huko nyumbani namimi nitoe mawazo yangu maana nakosa cha kuchangia maana wahusika kina mama wanadai n kawaida namimi sioni cha ukawaida wakati mke wangu anateseka kifungoni.
TUKUMBUKE: Maumivu haya anayapata Tu anaponyonyesha lakini akiacha akikaa kawaida hamna maumivu yoyote anayoyapata.
Ushauri wenu JAMANI.
*nawasilisha*