Maumivu ya ziwa la kushoto wakati wa kunyonyesha

Maumivu ya ziwa la kushoto wakati wa kunyonyesha

Issuna

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
3,203
Reaction score
7,628
Naomba msaada wenu Madaktari na Kina Mama mlio na Uzoefu na Hii hali jamani,yani mke wangu Tangu ajifungue alikua ananyonyesha vizuri kabisa maziwa yote mtoto ananyonya bila shida yoyote ile mpaka anashiba analala.

Lakini Ghafla kuanzia Juzi maumivu yakawa yanatokea kila anapomnyonyesha mtoto ziwa la kushoto,yalikua kidogo kwa mbali akawa anamnyonyesha ivyo ivyo kwa shida,Jana hali ikaongezeka mtoto akigusa nyonyo yani hayo maumivu yake acha kabisa yani,ikabidi nimshauri asimnyonyeshe ziwa la kushoto atumie moja tu la kulia.

Basi akafanya ivyo jana jioni,usiku,mpaka leo asubuhi nikamwambia ebu jaribu kumnyonyesha tena tuone kama utasikia yale maumivu,alipompa tu nyonyo mtoto Yani alisikia maumivu kiasi kwamba ilibidi nimpokee mtoto akainama analia kama mtoto kwa dakika kama mbili ndio ziwa likaachia,hakika nilitamani kulia kwa jinsi mke wangu alivyoumia nashndwa hata yaelezea hayo maumivu.

Kwasasa yupo anatumia ziwa moja tu kumnyonyesha mtoto,lakini mimi bado sina raha kwani sitamani kuona mke wangu anateseka kama nina uwezo wa kumsaidia japo kimawazo,Niko na Mama angu na mama angu mkwe wote nawambia tumpeleke mke wangu hospitali eti wao hawataki wanasema ni kawaida hiyo hali itakuja kuisha yenyewe.

Sasa mimi nipo zangu kazini huku naombeni mwenye ushaufi au ambae alishawahi pitia hali hii au anaejua sababu ya hili tatizo na Tiba yake ni kitu gani,ili nitakapoudi huko nyumbani namimi nitoe mawazo yangu maana nakosa cha kuchangia maana wahusika kina mama wanadai n kawaida namimi sioni cha ukawaida wakati mke wangu anateseka kifungoni.

TUKUMBUKE: Maumivu haya anayapata Tu anaponyonyesha lakini akiacha akikaa kawaida hamna maumivu yoyote anayoyapata.

Ushauri wenu JAMANI.

*nawasilisha*
 
huyo dogo ananyonya kuzidi ndama, dogo anamnyonya mamayake mpaka misuli ya ziwa inataka kupasuka, bro tatizo hilo lilimkuta pia mkewangu, ...tuanzie hapa, mtoto ana umri gani mpaka sasa, je ni wakiume
 
Itakuwa tu amechubuka!
Kbsa alianza kuchubuka kwenye chuchu lkn mtoto akianza kunyonya maumiv yanapotea ila ajabu sasa maumivu yanavuta ndani ya ziwa na si chuchu kama mwanzo.
 
huyo dogo ananyonya kuzidi ndama, dogo anamnyonya mamayake mpaka misuli ya ziwa inataka kupasuka, bro tatizo hilo lilimkuta pia mkewangu, ...tuanzie hapa, mtoto ana umri gani mpaka sasa, je ni wakiume
Mtoto ana siku 4...wa kiume
 
huyo dogo ananyonya kuzidi ndama, dogo anamnyonya mamayake mpaka misuli ya ziwa inataka kupasuka, bro tatizo hilo lilimkuta pia mkewangu, ...tuanzie hapa, mtoto ana umri gani mpaka sasa, je ni wakiume
Ana siku nne lakin ukimuona utasema ana wiki mbili maana Kazaliwa kwa opareshen Akatoka na Kilo 6...yani ni Heavy Man ukimuona huez amini kama ana siku 4..kunyonya ananyonya hasa na akivuta anavuta ipasavyo had mama ake Anataman amkamulie kwnye chupa coz n anavuta kama anavuta nini sjui.
 
Kbsa alianza kuchubuka kwenye chuchu lkn mtoto akianza kunyonya maumiv yanapotea ila ajabu sasa maumivu yanavuta ndani ya ziwa na si chuchu kama mwanzo.
Ni hiyo hiyo! Mwambie amuweke mtoto vizuri (saa mtoto ananyonya ahakikishe chuchu yote iingie ndani ya mdomo wa mtoto) ila atapona tu.
 
Ni hiyo hiyo! Mwambie amuweke mtoto vizuri (saa mtoto ananyonya ahakikishe chuchu yote iingie ndani ya mdomo wa mtoto) ila atapona tu.
Mkuu unamaanisha chuchu yote iingie ndan ya mdomo wa mtoto? itasaidia kweli maana sasa ivi anaogopa hata kumpa tena nyonyo kwa maumivu aloyapata asubuhi.
 
Mtoto hajacheulia iyo nyonyo mana nasikia mtoto akicheulia nyonyo ni hatari
 
Nenda hospital mama kadogoo! Tatizo dogo likiachwa husababisha tatizo kubwa. Waone wataalam wa afya.
 
Wakati ukipokea ushauri kwa wadau, jaribu kuwaona madaktari. Siku hizi kuna kansa ya matiti hivyo usichukulie poa sana
 
Wakati ukipokea ushauri kwa wadau, jaribu kuwaona madaktari. Siku hizi kuna kansa ya matiti hivyo usichukulie poa sana
n kweli na ndo mana sitaki kuwasikiliza sana kina mama mimi.
 
Back
Top Bottom