Dr. Zaganza
JF-Expert Member
- Jul 15, 2014
- 1,414
- 2,181
Mara nyingi kama kuna pande 2 au zaidi, basi mabadiliko yoyote yakifanyika, kuna upande utanufaika zaidi na kufurahi na kuna upande utapoteza. Lakini habari ya Mbape kuhama PSG kwenda AL Hila ya Saudi Arabia,(Japo Mbape tetesi zinaonesha hakubali).kwa mtazamo wangu na upeo wangu mdogo imekuwa mbaya kwa kila upande kama ifuatavyo:
1. Wafaransa wanamuona Mbape ni nembo yao (Icon). Ni hili wako sahihi, Kitendo cha kufunga hat-trick mchezo wa fainali kiliwahi kufanyika mara moja tu 1966 na Geof Bust wa England. Kumbuka mwaka jana rais w nchi Macron alimpigia simu kumsihi asihame (Hii inamaanisha anasaidia upepo wa kisiasa kutulia).hivyo kuondoka ni HABARI MBAYA KWAO.
2. Real Madrid wamemuwinda kwa muda mrefu mno na wamemaliza njia zote. Kumbuka la liga kwa sasa hawana misuli ya kipes sana kama zama za kukusanya mastaa wote wa dunia timu moja, mradi ambao rais wa Madrid,Fiorentina Perez aliuita Galactos. Hivyo wamevunja benki. Pia Madrid wametumia sheria,wakiishtaki PSG UEFA kwa matumizi mabaya (Hapa utacheka wao inawahusu nini, pili pili wasoila).Hivyo Mbape kwenda Al hilal kwa Madrid ni HABARI MBAYA KWAO.
3. Alhilal ,Wasaudia na washirika kwa juu juu unaweza kuona wamefurahia. Lakini kiuhalisia wanaona kama ndiyo mwanzo wa kuanza kuchanganya tamaduni za Ulaya ndani ya ardhi ya uarabuni. Mwanzo akina Ronaldo waliponunuliwa, wadau walichukulia ni wastaafu waloenda kumalizia mpira. Pia kukataliwa ofa ya usajili na Messi ilikuwa ahueni maana kamera za michezo zingegeukia Saudia. Lakini usajili wa Mbape ni kuwasha taa nyekundu kumbe timu za Saudia ziko serious . Utakumbuka world cup ya Qatar walivyopaa tabu kuchuana na wahamasisha ushoga (LGBT). Wadau wa Saudia wanaona kama sasa kiwingu cheusi kinatanda. Ukiacha timu husika, wadau wa tamaduni. Kwa wadau usajili wa Mbape kwenda Al hilal ni HABARI MBAYA KWAO.