Nilitaka kununua hisa za Vodacom, nikasikia mtaani kuwa kuna agizo kutoka mbinguni kuwa TTCL ndio chaguo la lazima.
Nikasema si mbaya, acha ninunue hisa za Twiga Cement...loh, huko ndio balaa. Nikasikia mitaani kuwa mshindani wake anaandaliwa mgodi na bomba la gesi ili auze saruji kwa 7000, kwa maana hy saruji yetu ya Twiga ipo mashaka ni
Si ndio nikakumbuka chama kubwa CRDB, ilibaki kidogo ninunie hisa ndio nikaona kwenye taarifa ya habari kuwa ya kwetu ni NMB na maelekezo yalishatoka kuwa njuruku zihifadhiwe huko na si kwingineko.
Soko la hisa limeanguka kwa kuwa sijanunua hisa.