Mauzo soko ya hisa Dar es Salaam yashuka kutoka bilioni 32 hadi billion 3.3

Mauzo soko ya hisa Dar es Salaam yashuka kutoka bilioni 32 hadi billion 3.3

Nilitaka kununua hisa za Vodacom, nikasikia mtaani kuwa kuna agizo kutoka mbinguni kuwa TTCL ndio chaguo la lazima.

Nikasema si mbaya, acha ninunue hisa za Twiga Cement...loh, huko ndio balaa. Nikasikia mitaani kuwa mshindani wake anaandaliwa mgodi na bomba la gesi ili auze saruji kwa 7000, kwa maana hy saruji yetu ya Twiga ipo mashaka ni

Si ndio nikakumbuka chama kubwa CRDB, ilibaki kidogo ninunie hisa ndio nikaona kwenye taarifa ya habari kuwa ya kwetu ni NMB na maelekezo yalishatoka kuwa njuruku zihifadhiwe huko na si kwingineko.

Soko la hisa limeanguka kwa kuwa sijanunua hisa.
Wakati huu ambao hisa zimeshuka ndio muda mzuri wa kununua za kutoka zikipanda unavuna mara dufu
 
Jitose huu ndio wakati wa kununua nenda kwa Mawakala wote wanakiri mwamko wa ununuzi ni mkubwa Nina hakika mwezi wa tano zikiingia sokoni kama sikosei tar 16 zitapanda mara mbili au zaidi. Kama umenunua za 8,500,000/= utapata 17,000,000/=. Hautajuta ukinunua hisa za awali (IPO). Barikiwa
naogopa kutake risk kweli yaani!!
 
Kwa hali hii ukiona kuna watu wanafurahia hiyo hali ujue amelogwaaa huyo
 
Wakati huu ambao hisa zimeshuka ndio muda mzuri wa kununua za kutoka zikipanda unavuna mara dufu
Hisa ni SEHEMU YA UMILIKI WA KAMPUNI kwa asilimia hizo, utakazojitwisha. Unaponunua hisa, unashare faida na hasara kwa hiyo ni jukumu lako kuangalia aina ya uwekezaji na matarajio ya kibiashara ya kampuni unayotaka kuimiliki kwa asilimia hizo unazozimudu.

Ikiwa tishio la mnyauko wa biashara na kukosekana na usawa wa ushindani katika sekta kunakotokana na kuingiliwa na 'maagizo kutoka juu' kutaendelea kushamiri namna hii, basi unaweza kujikuta unanunua hisa za kampuni inayoelekea ukingoni.

Mdororo wa biashara hauna mipaka na uwekezaji huanzia kwenye fursa, basi tujifunze kusoma alama za nyakati na athari za siasa katika uchumi kabla hatujaweka mikono kichwani.

Kuna kakitu sikumbuki vyema jina lake lakini something like Fair Competition Commission sijui kana jukumu gani katika kuhakikisha uwekezaji unafanyika kwenye platform iliyonyooka?
 
Nadhani siyo wakati sahihi wa kununua hisa
The best time is to buy when there is blood in the streets. Biashara nikubuy low and sell high, sasa kama kuna anguko la bei people will rush to sell and the price will decline "huo ndio wakati mwafaka kununua hisa"
 
Mijizi ndio imetufikisha hapa tulipo sasa [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji111]
 
kwa uelewa wangu and i stand to be corrected..... IPO ni pale MARA YA KWANZA hisa za kampuni binafsi fulani zinatolewa kwa ajili ya mauzo kwa UMMA. Na mara nyingi huwa zinatolewa na kampuni ndogo ili kukuza mtaji na sababu nyingine hta kampuni kubwa zinaweza issue hizi IPO kma zinataka kuoperate publicly na umma wote uhusike kwenye manunuzi ya hisa!!!

wataalam wanaweza nisahihisha pia
Thanks mkuu. Japo u ain't certain but your explanations make sense
 
Back
Top Bottom