Mauzo ya albamu za muziki Tanzania, Mkubwa Fela ataleta nafuu?

Mauzo ya albamu za muziki Tanzania, Mkubwa Fela ataleta nafuu?

KXY

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2011
Posts
885
Reaction score
341
Leo tarehe 21 mwezi wa nne 2015 bwana Said Fella amesikika akihojiwa redioni kwamba wanakuja na utaratibu wa kusimamia mauzo ya muziki hapa nchini kwa kuanzisha kampuni ambayo itasimamia mauzo ya wasanii watakaokubaliana nao. Kwa mujibu ya maelezo yake wao watakuwa wanakubaliana dau na msanii na kununua kazi yake kisha wao kufanya makubaliano na msambazaji.

My Take:
Kwanza nitoe pongezi kwa watanzania kuamua kuchukua hatua katika suala hili linalowaumiza sana wasanii

Pili napata mashaka kuhusu hatua hii kwasababu kampuni hii itakua inafanya kazi ya udalali ambayo si dhambi lakini naona walikuwa na uwezo wa kufanya makubwa zaidi ikiwemo kusambaza wenyewe.

Tatu ni utaratibu wa biashara yenyewe.
Miaka ya tisini mwishoni tulisikia kwamba msanii alikuwa anapewa shilingi mia mbili kwa kila kanda (tape) ikiwa ni kati ya asilimia 15 mpaka 20 ya mauzo. Tatizo hapa ilikua ni kujua idadi halisi ya mauzo yaliyofanyika, wengi walihisi wanaibiwa wakiamini wanauza zaidi ya vile wanavyoelezwa na 'wadosi'.

Mkubwa Fela yeye anasema wao watanunua kazi ya msanii (master) ikiwa na maana haki zote za mauzo zitakuwa zimenunuliwa. Mfumo huu hata kama utaleta nafuu lakini bado ni wa kinyonyaji, tutajua vipi nakala ngapi zimeuzwa, kodi italipwa kihalali na wote (msanii. dalali, msambazaji) watalipa kodi stahiki?

Kama huyu anayenunua kazi ya msanii ameweza kufanya mauzo makubwa sana katika hali ya kawaida hatopenda watu wajue kwasababu kibinadamu msanii atalinganisha kiasi alicholipwa na kile walichopata. Hii itaathiri kwa namna moja au nyingine biashara yao. Msanii hatakuwa na haki ya kuhoji tena kwa msambazaji ili kujua nakala ngapi zimeuzwa kwasababu yeye si mmiliki tena wa ile kazi.

Ushauri wangu ni kuwa tunahitaji mfumo wa kudhibiti mauzo na wasanii walipwe kwa asilimia kutokana na mauzo ya kazi. Mfumo huu ni rahisi kwasababu mgawanyo wa mapato unakuwa wa haki, mwandishi wa nyimbo, mtayarishaji, msanii, kampuni inayomuhodhi msanii, msambazaji, pamoja na kodi, kila kimoja kitapata stahili yake. kwa namna hii hata baada ya miaka 10 kama kazi ya msanii bado inauzwa msanii atanufaika. Kwa bahati mbaya Fella anaamini mauzo ni ndani ya juma tu (1 week, kwa maneno yake mwenyewe), hii ni ishara mbaya.

'Bad is never better than worse', njia ya kutatua tatizo ni kuondokana nalo na sio kulibadilishia jina.

Asanteni.
 
Yaani nimemsikiliza Mkubwa fella ilaa kwa kwelii analetaa unyonyaji kabisa, asidanganye watanzania kua album kutoka itauza ndani ya week moja, kwa hilo nakataa,
Mi nadhani kinachotakiwa hapa si kuuza kila kitu km msanii kwani kufanya hivyo ni sawa na kumnyima haki za msingi mtunzi wa nyimbo hizo ambazo hazisikilizwi kwa Juma moja wala kununuliwa kwa Juma moja
Nadhani wasanii wakae tena wafikiriee jinsi yakukabilianaa na tatzo hili.
Nimaonii tuu ila pia wengine wanakaribishwaa
 
Ndio yale yale ya Marehemu Kanumba kutoa movies nyingi halafu ya kwake hata moja hakuna.

Hakuna umaskini mbaya kama wa kuuza haki zako kipuuzi, wasanii kuweni makini huo ni wizi kama wizi mwingine.
 
Watu sasa hivi hawanunui album tena, wanashusha tu mtandaoni.

Wameweza kuiba Game of Thrones washindwe kuiba album ya mwanamziki bongo?

Hizo album wakawauzie wale wanaoishi porini.
 
Atakula hasara Bure sikuizi watu hawanunui album.
 
Yaani nimemsikiliza Mkubwa fella ilaa kwa kwelii analetaa unyonyaji kabisa, asidanganye watanzania kua album kutoka itauza ndani ya week moja, kwa hilo nakataa,
Mi nadhani kinachotakiwa hapa si kuuza kila kitu km msanii kwani kufanya hivyo ni sawa na kumnyima haki za msingi mtunzi wa nyimbo hizo ambazo hazisikilizwi kwa Juma moja wala kununuliwa kwa Juma moja
Nadhani wasanii wakae tena wafikiriee jinsi yakukabilianaa na tatzo hili.
Nimaonii tuu ila pia wengine wanakaribishwaa

Sitaki kuamini kwamba wasanii kama Diamond, Shaa na Mwana FA wamekubaliana na hili, nafikiri Fella hakuwa mtu sahihi kuelezea kampuni yao itakavyofanya kazi(maybe some details are missing). Kama ndio hivyo basi wasanii wetu wana safari ndefu sana ambayo bado haijaanza
 
Watu sasa hivi hawanunui album tena, wanashusha tu mtandaoni.

Wameweza kuiba Game of Thrones washindwe kuiba album ya mwanamziki bongo?

Hizo album wakawauzie wale wanaoishi porini.

Mauzo yamepungua sana kwa sasa, nguvu zinaelekezwa kwenye 'digital sales'. Hofu ni kama hiyo mikataba yao itaangalia hili
 
Atakula hasara Bure sikuizi watu hawanunui album.

CD zinanunuliwa bado huku mitaani ila ndio kwa zile bei za watandaza chini buguruni na kwingineko, mikoani biashara ya ku 'burn' CD inaendelea kama kawaida.
Bei ya 5000 itakubalika sokoni?
 
Tuna safari ndefu sana. Wanaohodhi tasnia kwa Tanzania ni kimeo pia.
 
  • Thanks
Reactions: KXY
Tuna safari ndefu sana. Wanaohodhi tasnia kwa Tanzania ni kimeo pia.

Wasanii wetu wanatakiwa watambue kuwa soko lao ni zaidi ya Tanzania, wengi wanapotea kwa kuwasikiliza miungu watu badala ya kufanya kazi zao ziongee. Dunia ni kijiji, inabidi kutumia vizuri fursa zilizopo kujitangaza kimataifa, angalau hata soko la hapa Afrika mashariki lisiwashinde basi.
 
Huyu mjomba labda kaitwa redioni la kuongea hana, akaamua azuge tu.
 
  • Thanks
Reactions: KXY
Atakula hasara Bure sikuizi watu hawanunui album.

Mbona huko Marekani msanii anatoa albam ndani ya siku 3 anauza copy Mill 1 inamaana kwao hamna mitandao ya kuweza kudownload bure? kuna movie ya Fast & furious 7 imetoka ndan ya siku 2 walipata faida ya Bill 1!
 
Wasanii wetu wanatakiwa watambue kuwa soko lao ni zaidi ya Tanzania, wengi wanapotea kwa kuwasikiliza miungu watu badala ya kufanya kazi zao ziongee. Dunia ni kijiji, inabidi kutumia vizuri fursa zilizopo kujitangaza kimataifa, angalau hata soko la hapa Afrika mashariki lisiwashinde basi.

Tatizo wasanii wa bongo hawana ushirikiano! akisha nunua vitz anakuwa na dharau!
 
Mauzo yamepungua sana kwa sasa, nguvu zinaelekezwa kwenye 'digital sales'. Hofu ni kama hiyo mikataba yao itaangalia hili

Fella atawakamata underground washamba. Wajanja hakubali mtu.
 
Mbona huko Marekani msanii anatoa albam ndani ya siku 3 anauza copy Mill 1 inamaana kwao hamna mitandao ya kuweza kudownload bure? kuna movie ya Fast & furious 7 imetoka ndan ya siku 2 walipata faida ya Bill 1!

Mkuu umeshasema Marekani ni tofauti na Bongoland wizi wa kazi za wasanii ni mkubwa ikiwemo ku burn macd imagine album inauzwa buku kwa kumagwa ingekua Kuna usimamizi madhubuti at least mwenyewe binafsi siwezi kununua album ya Bongo flavour au hata bongo movie ni wastage of money hakuna jipya.
 
Fella atawakamata underground washamba. Wajanja hakubali mtu.

Sijajua wajanja ndio wakina nani ila Fella amesema wameshakubaliana na wasanii kumi, aliowataja ni Ya Moto Band, Diamond, Mwana FA na Shaa
 
chupa mpya mvinyo wa zamani..hakuna unafuu... mkubwa fela ni dalali wa wasanii.. zaid msanii atazid kunyonywa maana mtu wa kati nae anataka afaidike kwa jasho hilohilo..bora msanii aende mwenyewe kwa mhindi
 
Back
Top Bottom