KXY
JF-Expert Member
- Dec 31, 2011
- 885
- 341
Leo tarehe 21 mwezi wa nne 2015 bwana Said Fella amesikika akihojiwa redioni kwamba wanakuja na utaratibu wa kusimamia mauzo ya muziki hapa nchini kwa kuanzisha kampuni ambayo itasimamia mauzo ya wasanii watakaokubaliana nao. Kwa mujibu ya maelezo yake wao watakuwa wanakubaliana dau na msanii na kununua kazi yake kisha wao kufanya makubaliano na msambazaji.
My Take:
Kwanza nitoe pongezi kwa watanzania kuamua kuchukua hatua katika suala hili linalowaumiza sana wasanii
Pili napata mashaka kuhusu hatua hii kwasababu kampuni hii itakua inafanya kazi ya udalali ambayo si dhambi lakini naona walikuwa na uwezo wa kufanya makubwa zaidi ikiwemo kusambaza wenyewe.
Tatu ni utaratibu wa biashara yenyewe.
Miaka ya tisini mwishoni tulisikia kwamba msanii alikuwa anapewa shilingi mia mbili kwa kila kanda (tape) ikiwa ni kati ya asilimia 15 mpaka 20 ya mauzo. Tatizo hapa ilikua ni kujua idadi halisi ya mauzo yaliyofanyika, wengi walihisi wanaibiwa wakiamini wanauza zaidi ya vile wanavyoelezwa na 'wadosi'.
Mkubwa Fela yeye anasema wao watanunua kazi ya msanii (master) ikiwa na maana haki zote za mauzo zitakuwa zimenunuliwa. Mfumo huu hata kama utaleta nafuu lakini bado ni wa kinyonyaji, tutajua vipi nakala ngapi zimeuzwa, kodi italipwa kihalali na wote (msanii. dalali, msambazaji) watalipa kodi stahiki?
Kama huyu anayenunua kazi ya msanii ameweza kufanya mauzo makubwa sana katika hali ya kawaida hatopenda watu wajue kwasababu kibinadamu msanii atalinganisha kiasi alicholipwa na kile walichopata. Hii itaathiri kwa namna moja au nyingine biashara yao. Msanii hatakuwa na haki ya kuhoji tena kwa msambazaji ili kujua nakala ngapi zimeuzwa kwasababu yeye si mmiliki tena wa ile kazi.
Ushauri wangu ni kuwa tunahitaji mfumo wa kudhibiti mauzo na wasanii walipwe kwa asilimia kutokana na mauzo ya kazi. Mfumo huu ni rahisi kwasababu mgawanyo wa mapato unakuwa wa haki, mwandishi wa nyimbo, mtayarishaji, msanii, kampuni inayomuhodhi msanii, msambazaji, pamoja na kodi, kila kimoja kitapata stahili yake. kwa namna hii hata baada ya miaka 10 kama kazi ya msanii bado inauzwa msanii atanufaika. Kwa bahati mbaya Fella anaamini mauzo ni ndani ya juma tu (1 week, kwa maneno yake mwenyewe), hii ni ishara mbaya.
'Bad is never better than worse', njia ya kutatua tatizo ni kuondokana nalo na sio kulibadilishia jina.
Asanteni.