Mavazi ya wanaume vimodo na jeans za matobo, tunaenda wapi?

Mavazi ya wanaume vimodo na jeans za matobo, tunaenda wapi?

Hawana hata haya, unakutana na mwanaume njiani kavaa modo inambanaa mtumbo_mkitambia huo mtisheti na wenyewe unambana basi yuko km pipaa fyuuu
 
Daah! Mkuu umeandika kwa hisia hadi imebidi nifungue kabati langu la nguo kuhakikisha kama na Mimi naweza kuwa mmoja katibya wanaokukera kwa namna yoyote ile. Lakini ashukuriwe Bwana naona namiliki kanzu, vikoi na majoho tu (msiniulize kama nahitimu). Si unajua sisi wengine hata hizo suruali na mambo yetu Yale hazitufai
 
naenda moja kwa moja kwenye point...
hivi kama wanaume tumefikia mahala kuvaa suruali/jeans za kubana hadi ifikie..
1 -kuipandisha hadi kiunoni si chini ya dk 5 na kuchomekea vest na shati dk 5
2 -kuivua lazma ukae uivute taratibu hatua kwa hatua
3 -kuchuchumaa haifai
4 -kuikunja unawe miguu haifai
5 -kuvuka mtaro haiwezekani
6 -n.k

yani imefika mahali tukiingia chumbani na madem wetu tunapokezana kuvutana suruali saa ya kuvua, zamani ilikuwa sisi ndo tunawavuta wao jeans zao show ianze sasa na wao wakitusapoti kuvuta jeans wakati wa kuvua inakuaje wadau?

haya, sisemei zile jeans fashion mpya zilizochanwachanwa mapajani..utakuja kijana wa kiume paja leupe lina vinyoya flani vile ukiangalia haraka utasema za mdada wa kiarabu eti na yeye kavaa jeans imeraruliwa mapajana matundu 6 kila upande..

tunaenda wapi jamani na fashion hizi?
Mimi sijui tunaenda wapi, labda muulizen Platnums na wenzake maana ndiye aliyeanzisha hii fasheni
 
Hawana hata haya, unakutana na mwanaume njiani kavaa modo inambanaa mtumbo_mkitambia huo mtisheti na wenyewe unambana basi yuko km pipaa fyuuu
Hahahaaaa!! Sasa wa hivyo ukute na mapaja kajaaliwa! Uwiiii aibu naona mimi.
 
Mnawaharibu watoto wa wenzenu kwa kutumia neno model, zipu ya suruali ya mwanaume shurti iwe nchi sita bwana.
Yes Madam, Eclat.

Ili kulijua hili. Kijana aende kwa Fundi nguo (Nb; Si Fundi cherehani) then ampe maelekezo kuwa ashonewe suruali (Hapa asiweke masharti yeyote) yeye akae kimya kuanzia mwanzo mpaka mwisho then baada ya siku kadhaa aje kuichukua suruali yake.

Vipimo vya suruali atakayokutana nayo ndiyo suruali halisi ya Mwanaume. Si hii bidhaa ya kike ya kubana mapaja wanazoziita Model.

Pia ni concept fulani ya GrouThink Groupthink - Wikipedia aliyoiita LeBon Gustave Le Bon - Wikipedia ambayo hutokea kidogo kidogo kutokana na mabadiliko ya kimazingira.

Pia Psychological mob ni sababu vilevile. Vijana wanaiga sana, Why factor is not considered.
 
Back
Top Bottom