Kwenye miaka ya mwisho ya 1960, mavazi kama hayo yalikuwepo ila tofauti ni kuwa yale ya wakati huo hayakuwa yamechanwa. Wakati ho vijana wa TANU Youth League walikuwa wanatembea na mikasi kuchana suruali hizo kuanzia miguuni. Hata akina dada waliovaa nguo za kubana walisaidiwa hivyo hivyo.
Siku hizo ukifanya hivyo utaambiwa unataka kubaka nk.
Hata viatu vilivyochongoka mbele hadi ncha kuinuka juu vilikuwepo - tukiviita PINOKYO!
Mitindo hiyo ilipokwisha zikaja suruali zilizopanuka kidogo miguuni zikiitwa PECOS na baada suruali kubwa zaidi zikiitwa BUGALUU, na viatu virefu kwenda juu vikiitwa RAIZON
Ni fasheni ambazo zinapita na zitarudi tena baada ya miaka ila fasheni mbaya lazima zipigwe vita.