Mavazi ya wazazi hospitali

Mavazi ya wazazi hospitali

Hahaha, kwa hali nionayo mle ndani sidhani kama huo ujasiri wa kufanyiwa massage utakuepo
kuna dada nadhani ilikua mimba ya kwanza, kashikwa na uchungu kabeba kyupi mkononi anakimbia wodini nesi anamwambia nani kakituma ufanye sista anamjibu jamaa alimlazimisha ila yeye alikua hataki. [emoji4][emoji4][emoji4]
😀😀😀
 
Sio kwamba tunaumwa vibaya, treatment nayo inachangia, wenzetu katika hali hiyo mama anajaliwa, nesi anamtreat vizuri, anapewa hata achague style ya kukaa ambayo anajisikia comfortable , tena mara nyingine anakua na mtu mume, mzazi au ndugu wa kumwangalia yani hadi raha.
Wabongo sie treatment tu ya nesi hadi unajiona leba umeenda kufa, unaumwa nesi anafoka, sauti ya juu vua nguo, panda kitandani lala ubavu, usiamke utaua mtoto hizi kauli uchungu utaacha kuzidi 😀😀
Muda huo upo mwenyewe mume nae kakimbia kusiko julikana aaaggghh tabu
Duh..
Kinamama hapa bongo mnapata tabu hivyo kumbe..
Poleni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom