Mavazi yanamtambulisha mtu?

Mavazi yanamtambulisha mtu?

muneera75

Senior Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
190
Reaction score
318
Kama ilivyo kawaida kwamba binadamu tupo tofauti socially, economically, physically, in religion na pia in cultural tupo tofauti. Kwa maana hiyo mionekano yetu inaweza ikasababisha mtu aijue tabia ya mtu fulani.

Kwa experience yako ni mavazi gani au muonekano upi humfanya mtu azijue tabia za mtu fulani?

Mfano: Ukivaa suti na briefcase mkononi unaonekana kama unaela au tajiri, mstaarabu, baba mwenye familia ya kisomi, pia unaeza ukahisi anaishi sehemu za matajiri labda Masaki, Mbezi.
 
Binafsi siwezi kuzijua tabia za mtu kwa mavazi lakini asilimia kubwa ya watu wanawezaga kunipa sifa zangu kwa kuangalia mavazi yangu/ninavyopendelea kuvaa.

Hivyo naamini inawezekana kuzijua tabia za mtu kwa staili hiyo.
 
Mavazi ni muonekano unamtambulisha mtu nakusitiri uhalilisia wa kimwili, Nguo haziwezi elezea mtazamo wa mtu au uwezo wake kiakili,kiuchumi.

Usimhukumu, au kumfikiria mtu tofauti sababa ya mavazi ,angali ndani ya Moyo was mtu au macho utaona uwezo wake na tabia zake Ila sio mavazi, Wengi mavazi huongeza unadhifu na umaridadi...
 
Binafsi siwezi kuzijua tabia za mtu kwa mavazi lakini asilimia kubwa ya watu wanawezaga kunipa sifa zangu kwa kuangalia mavazi yangu/ninavyopendelea kuvaa.

Hivyo naamini inawezekana kuzijua tabia za mtu kwa staili hiyo.

Outfits say a lot about someone's personality, moods even status., wengine tumeenda mbali zaidi hata rangi ya nguo nitakayoamua kuvaa asubuhi huwa inadefine mood ya siku husika.

Let's meet at the top, cheers 🍻
 
Mfano mavazi ya kahaba hayaendani na tabia yake? Mchungaji/ sheikh je?
si wote wanaovaa nguo fupi ni makahaba, masheikh na wachungaji yale ni mavazi ya rasmi kwa nafasi zao bt hayaakisi matendo yao, kuna masheik na maaskofu wazinz na wapigaji na hutumia mavaz yale kuficha uovu wao.
 
Mi binafsi huvaa kutokana na eneo husika,yaani naenda wapi na nitakua na kina nani,Siku moja nilipigiwa simu ya dharula mama mkwe amekimbizwa hospitali nikapitilizia huko nimevaa pensi ndefu kiasi tisheti na sendo.Niliwakuta na wengine tuliooa nao hiyo familia pamoja na mashemeji,Muda wa kujadili gharama wakanitenga wakajadili pembeni wakachanga kama robo.
Sasa kimbembe kuchangia damu kila mtu anatoa udhuru mwisho ikabidi wanishirikishe bahati nzuri nikawa grupu moja nikatoa damu,kwa ukuda nikaimalizia na hela ya matibabu iliyopelea,Wenzangu waliokua wamevaa suti na kuichukilia poa pensi yangu tukaanza na kupeana namba.
 
Kama ilivyo kawaida kwamba binadamu tupo tofauti socially, economically, physically, in religion na pia in cultural tupo tofauti. Kwa maana hiyo mionekano yetu inaweza ikasababisha mtu aijue tabia ya mtu fulani.

Kwa experience yako ni mavazi gani au muonekano upi humfanya mtu azijue tabia za mtu fulani?

Mfano: Ukivaa suti na briefcase mkononi unaonekana kama unaela au tajiri, mstaarabu, baba mwenye familia ya kisomi, pia unaeza ukahisi anaishi sehemu za matajiri labda Masaki, Mbezi.
Mavazi yana taathira kubwa sana kwa mtu na tabia zake. Ila ukitaka kumjua mtu tabia yake basi angalia wale watu anao suhubiana nao,mara nyingi mtu huchukua tabia za rafiki yake.

"Nawasalimia huku toka huku nilipo"
 
Binafsi siwezi kuzijua tabia za mtu kwa mavazi lakini asilimia kubwa ya watu wanawezaga kunipa sifa zangu kwa kuangalia mavazi yangu/ninavyopendelea kuvaa.

Hivyo naamini inawezekana kuzijua tabia za mtu kwa staili hiyo.
Swadaktaa.
 
si wote wanaovaa nguo fupi ni makahaba, masheikh na wachungaji yale ni mavazi ya rasmi kwa nafasi zao bt hayaakisi matendo yao, kuna masheik na maaskofu wazinz na wapigaji na hutumia mavaz yale kuficha uovu wao.

dhambio sio uzinzi tu mkuu
 
Nchi za wazungu katika vitu hawajali ni mavazi na inafanya maisha yanakuwa very simple, yaani ukienda hata kwenye nyumba za ibada watu wako simple, tshirt, pence na ndala, jeans na trainers, nk.
Hata baadhi ya maofisi hawajali unavaa nini mradi sio very revealing
 
Mi binafsi huvaa kutokana na eneo husika,yaani naenda wapi na nitakua na kina nani,Siku moja nilipigiwa simu ya dharula mama mkwe amekimbizwa hospitali nikapitilizia huko nimevaa pensi ndefu kiasi tisheti na sendo.Niliwakuta na wengine tuliooa nao hiyo familia pamoja na mashemeji,Muda wa kujadili gharama wakanitenga wakajadili pembeni wakachanga kama robo.
Sasa kimbembe kuchangia damu kila mtu anatoa udhuru mwisho ikabidi wanishirikishe bahati nzuri nikawa grupu moja nikatoa damu,kwa ukuda nikaimalizia na hela ya matibabu iliyopelea,Wenzangu waliokua wamevaa suti na kuichukilia poa pensi yangu tukaanza na kupeana namba.
Acha uongo,kutoa damu si lazima group zimatch.
 
Back
Top Bottom