Maviziano na Maridhiano ya Wao, Sisi, na Wale!

Maviziano na Maridhiano ya Wao, Sisi, na Wale!

"Mahitaji kidogo" si yangewafanya CCM kutumia ibara ya 100 kama walivyofanya zamani? Yaani, tulete Katiba mpya kwa ajili ya "mahitaji kidogo"?
kwa wakati muafaka itakua tu gentleman.
wala hakuna haraka na mambo muhimu kama hayo :1Head:
 
WA KUJIBU HIYO HOJA NI JOHN HECHE.

TAG HIS ASS

HECHE ANASEMA CCM NA SERIKALI WAKIKIRI MAASI YAO, NA KUMUACHIA LISSU, TUTAENDA KURIDHIANA KAMA KABURU NA MANDELA NA DESMOND TUTU.

KWANI HUKO SOUTH AFRIKA WAZULU NA WA XHOSA WALIWAKOSEA NINI KABURU?

KWA NINI TUFUATE MODEL YA KIPUMBAVU YA SOUTH AFRIKA ???

KWA SAAB HATUELEWI
WANANCHI AU CHADEMA WAMEIKOSEA NINI SERIKALI

HECHE, BAADA YA OCT 29 KWENYE MAJUKWAA NCHI NZIMA UMEHUBIRI NUREMBERG TRIAL YA MA OCD NA MA DSO WA USALAMA WA ADOLF HITLER.

AMETOA MA SPICHI AMBAYO HAYAJAWAHI KUSIKIKA KWENYE MAJUKWAA AFRIKA, KWAMBA DIKTETA LIKIUA LAZIMA NA LENYEWE LIJE LIJIBU, NA MA RPC WAKE NA WAKURUGENZI WAKE WA USALAMA.

GHAFLA UNATUHUBIRIA MARIDHIANO KAMA YA SOUTH AFRIKA. SASA KWA NINI ULIHUBIRI NEUREMBER TRIAL ON OPEN RALLYS ACROSS THE VILLAGES AND TOWNS OF THIS COUNTRY AFTER THE OCTOBER MASSACRE ??????


KWA NINI TWENDE NA MODEL YA KIPUMBAVU YA KABURU NA DESMOND TUTU? MUAFRIKA ALIMKOSEA NINI KABURU NA MTANGANYIKA AMEMKOSEA NINI SAMIA, KUMWAMBIA HAWAMTAKI URAIS HAWEZI, NI MWIZI NA MTE ?????

..Mgogoro wa Afrika Kusini ulihusisha pande mbili zilizokuwa na silaha.

..ANC, PAC, na vyama vingine vya Waafrika, vilijihusisha na mapambano ya silaha, na vilihusika na mauaji.

..Kwa hiyo, Waafrika walipokwenda kwenye maridhiano walikuwa wanakwenda kuwaomba radhi Wazungu waliowawa kimakosa.

..Hoja uliyoijenga ni ya msingi kweli kweli. Mpaka sasa hivi Ccm hawajaeleza Chadema imewakosea nini wao, wala Watanzania.
 
Kwamba, taifa zime tunatakiwa tukubali kuwa CCM ndio mtawala wetu wa milele na hisia yoyote ya kuichukia na kutaka kuitoa madarakani ni sawasawa na kutenda dhambi fulani ambayo watu wanatakiwa kuungama na kufikia toba!
Pascal Mayalla na Ccm wenzako ikiwemo Spika mstaafu Tulia mlituimbia sana hili pambio la Ccm kutawala milele.
 
Samia ni mcha Mungu sana, hapendi siasa za chuki, uhasama, fitina na uadui. Anataka siasa za kistaarabu. Hiyo maridhiano, ni kutaka kujenga uhusiano mwema, na hao wanaojifanya wapinzani.
Angekuwa kweli ni mtu muadilifu hivo asingekubali kuapishwa kwa matokeo ya uongo.
 
Rais Samia kahubiri na kuyatenda maridhiano toka aliposhika madaraka....Alimualika na hatimaye kumleta Lissu kutoka ughaibuni kwa nia njema ya maridhiano ...unaikumbuka 4 R ??
SWALI MUHIMU ...NI NANI HUYU NYUMA YENU ASIYETAKA NCHI IRIDHIANE...ANAFANYA HIVI KWA MASLAHI YA KINA NANI?
PASIPOKUWA NA MARIDHIANO MAANA YAKE PAWE NA NINI??
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Tunajaribu kuaminishwa kuwa tunahitaji maridhiano. Kwamba, tumekosana kiasi kwamba ili tuweze kupatana ni lazima tukae chini na kukubaliana kupatana. Manabii uchwara wa maridhiano wanataka taifa zima lipige magoti na kuanza kufukiza ubani kwenye madhabahu waliyoitengeneza wao; madhabahu yenye unyevu wa damu. Tatizo kubwa ambalo wajumbe na mabalozi hawa wa ulaghai hawataki kulisema ni kitu gani wao wametukosea sisi, au wamewakosea wengine.

Kutwa kucha, wanaimba wimbo wa ulazima wa maridhiano lakini hawako tayari kusema sisi tumewakosea nini wao. Na kama kinachozungumzwa ni CHADEMA NA CCM ni lazima ijulikane wazi kuwa hawa watu walikosana nini hasa hadi waitane kwenye kile kinachoitwa "meza ya mazungumzo" au kama ninavyoiona mimi - meza ya kusalimu amri. Kama CCM na CHADEMA ndio waliokosana kama inavyodaiwa kutokea Zanzibar kati ya CCM na ACT-Wazalendo basi wawe wa kweli kwanza.

CHADEMA imeikosea nini CCM? Kama mifano mbalimbali iliyokuwa inatolewa kwenye kesi ya Tundu Lissu na viongozi wenzake unaweza kuamini kabisa kuwa kuna uovu mkubwa sana umefanywa na CHADEMA. Yaani, inawezekana kabisa wanasiasa kutoka CHADEMA hawatakiwi kutoa mawazo, kujenga hoja, kupinga serikali au kuwa na misimamo tofauti na ile ya Chama tawala. Lakini, wanapotaka maridhiano ni lazima tuwaulize - kwani CHADEMA Iimewakosea nini nyinyi CCM?

Leo hii mwenyekiti wa CHADEMA yuko mahakamani kwa tuhuma za kudai wataenda 'kukijambisha' kwenye uchaguzi mkuu. Kwamba, kauli hizi za 'kukinukisha' inaweza kuwa ni uhaini. Kana kwamba ni makosa kuwafanya watu waichukie CCM na watake kuitoa madarakani. Imefika mahali kuna watu wanaamini kabisa kuwaza, kupanga na kufanya mikakati ya kisiasa ya kuitoa CCM madarakani ni makosa na ni uhaini. Kwamba, taifa zime tunatakiwa tukubali kuwa CCM ndio mtawala wetu wa milele na hisia yoyote ya kuichukia na kutaka kuitoa madarakani ni sawasawa na kutenda dhambi fulani ambayo watu wanatakiwa kuungama na kufikia toba!!

Na kama ni kinyume chake ni lazima tuulize; wao CCM wameikosea nini CHADEMA? Hili labda haliwezi kuwa na mjadala mkubwa kwa sababu CHADEMA wanaweza kuorodhesha vitu 100 ambavyo wamekuwa wakitendewa na serikali ya Chama cha Mapinduzi kiasi kwamba labda ni CCM ndio inahitaji kuwapigia CHADEMA magoti na kuomba maridhiano.

Lakini, kama maridhiano haya si ya vyama vya siasa bali kati ya wananchi na watawala wao ni wazi kubwa maswali yale yale lazima yaulizwe. Kwani wananchi wameikosea nini CCM? Matukio ya Oktoba 29 na mauaji yaliyofanyika baadaye ni makosa makubwa ambayo Watanzania wamewafanyia watawala wetu? Je, vijana kuandamana na kutaka kuidai nchi yao na kukataa mfumo mbovu wa uchaguzi ni dhambi dhidi ya CCM kiasi cha mamia kati yao kuuawa na mtu yeyote asiwajibishwe hadi leo?

Kwenye taifa na mazingira ambayo watu wanaishi katika hali ya kuviziana inawezekana vipi watu wakaridhiana? Leo hii mtu akisimamishwa na polisi hata kama anaulizwa nyumbani kwa Katibu Kata watu watakodoa macho kwa sababu hawajui litaishaje. Leo, hii unasikia polisi wameuawa au wamekufa watu hawana tena "wapumzike kwa amani" badala yake watu wanagongeana bia!! Watu tumekaa kuviziana na kuogopana! Kuna maneno sasa hivi watu hawatakiwi kuyasema hadharani na wakawa salama!

Wale wanaoitwa "viongozi" pamoja na vimulimuli na ving'ora vyao ni wazi kuwa wanajua hawako salama. Watu wamejipanga mstari na kuimba mapambio na qasida ili wasionekane wabaya au wenye mbinu mbaya. Huko ndani wanaviziana na kuogopana na wameshajifunza kwa yaliyomkuta Ndugai na Nchimbi; hakuna aliyesalama kati yao. Huko upinzani na wenyewe wanaogopana na kuviziana - ya Lema na Heche yanatukumbusha yalikoanzia ya kina Kaborou na Zitto! Upinzani bila migogoro ya ndani hauwezekani kama vile CCM bila makundi haiwezekani!

Ndiposa, swali lazima liulizwe - kwenye mazingira ya maviziano, maridhiano yanawezekana vipi? Kwenye siasa za kunyemeleana, kuelewana kutatokea vipi? Jibu langu ni rahisi - haiwezekani hadi mmoja ashindwe kwenye uchaguzi kihalali kabisa - ndipo maridhiano ya kweli yanaweza kutokea. Nje ya hapo, ni kusumbua ubongo wetu kama taifa!!! Hamtaki?
Kabla na baada ya Uchaguzi
Makamu Mwenyekiti bara Ndugu Wasira Masato huwa anasema kuwa CCM inaridhiana na wananchi.
Huwa sijui hayo maridhiano huwa ni ya nini ?
 
Jiwe aliua watu 10k? Jiwe alifanya ufisadi?
Kwendeni zenu wadini wakubwa na wanafiki nyie! Wapuuzi na matahila wanawaunga mkono kwa ujinga wao wakutokujua,mna chuki na Rais akiwa muislam...

Ili ujue kuwa Jiwe alikuwa fisadi angalia jinsi alivyomsumbua CAG, ili tu asianike ufisadi wake na serikali yake,ukiona kiongozi anapambana na CAG Moja kwa moja ujue uyo ni fisadi na jizi kubwa,ila nyie mazuzu alikuwa anawadanganya kuwa yeye ni mtetezi wa wanyongwe,wakati ni jizi tu...
 
Maridhiano ya kweli yaanzie kwenye upatiakanaji wa viongozi wanaotokana na wananchi (uchaguzi wa huru, wazi na haki )

Haiwezekani, Serikali iliyopo madarakani kwa asilimia 98 bado wananchi wanapotea, wanatekwa na kubambikiwa kesi za uongo.

Tupate viongozi wanaotokana na kura zetu kuanzia Serikali za mitaa, vijiji, vitongoji, kata, majimbo ma taifa kwa ujumla hapo ndipo tutakuwa tumefungua njia ya maridhiano.
 
Kwendeni zenu wadini wakubwa na wanafiki nyie! Wapuuzi na matahila wanawaunga mkono kwa ujinga wao wakutokujua,mna chuki na Rais akiwa muislam...

Ili ujue kuwa Jiwe alikuwa fisadi angalia jinsi alivyomsumbua CAG, ili tu asianike ufisadi wake na serikali yake,ukiona kiongozi anapambana na CAG Moja kwa moja ujue uyo ni fisadi na jizi kubwa,ila nyie mazuzu alikuwa anawadanganya kuwa yeye ni mtetezi wa wanyongwe,wakati ni jizi tu...
Jiwe hajaua Watanganyika 10k. Jiwe hakupata div 4 ya D2.
 
Rais Samia kahubiri na kuyatenda maridhiano toka aliposhika madaraka....Alimualika na hatimaye kumleta Lissu kutoka ughaibuni kwa nia njema ya maridhiano ...unaikumbuka 4 R ??

SWALI MUHIMU ...NI NANI HUYU NYUMA YENU ASIYETAKA NCHI IRIDHIANE...ANAFANYA HIVI KWA MASLAHI YA KINA NANI?
PASIPOKUWA NA MARIDHIANO MAANA YAKE PAWE NA NINI??


Huoni hata aibu, alimleta Lissu kwani Lissu sio mtanzania wa kuzaliwa mwenye haki ya kuishi sehemu yoyote Tanzania?..

Hebu elezea nini kwanza kilimtoa Lissu Tanzania.

Kuhusu 4R za Samia , ni uthibitisho zilikua ni utapeli maana R moja kati ya 4 ni REFORMS kitu cha ajabu uchaguzi wa serikali za mitaa ambao ndio ulikua wa kwanza Samia akiwa rais haukua na tofauti yoyote na ule wa 2019 chini ya Magufuli.

Samia alibadili jina la tume na kuiita huru ilhali muundo umebaki ule ule ni sawa na kubadili chupa ya mvinyo ila mvinyo na kiwango cha kileo kinabaki kile kile.

Lissu aliona mbali ndio maana alipokua mwenyekiti hakuona sababu yoyote ya CHADEMA kushiriki ujinga ulioitwa uchaguzi ilhali ni uteuzi wa maccm na ndio wakaona wampe kesi ya kubumba ya uhaini ila alichokua anakidai ni reforms ambazo Samia alizihubiri kumbe hakua tayari kwa reforms za kweli bali maigizo.
 
Rais Samia kahubiri na kuyatenda maridhiano toka aliposhika madaraka....Alimualika na hatimaye kumleta Lissu kutoka ughaibuni kwa nia njema ya maridhiano ...unaikumbuka 4 R ??
SWALI MUHIMU ...NI NANI HUYU NYUMA YENU ASIYETAKA NCHI IRIDHIANE...ANAFANYA HIVI KWA MASLAHI YA KINA NANI?
PASIPOKUWA NA MARIDHIANO MAANA YAKE PAWE NA NINI??

..sio kweli.

..Ssh alianza vizuri alipokuja na 4R.

..hapo katikati kuna mtu alimshauri atumie nguvu badala ya reforms na maridhiano.

..kwa upande mwingine, zile BILLION 200 alizochangiwa zilikuwa zinatosha kulambisha watu wote asali, na Oct 29 asingekufa hata sisimizi.
 
Walioruhusu watu wauawe chini ya utawala wao watalipia hapa duniani (Tanzania) na akhera.
 
Back
Top Bottom