Maviziano na Maridhiano ya Wao, Sisi, na Wale!

"Mahitaji kidogo" si yangewafanya CCM kutumia ibara ya 100 kama walivyofanya zamani? Yaani, tulete Katiba mpya kwa ajili ya "mahitaji kidogo"?
kwa wakati muafaka itakua tu gentleman.
wala hakuna haraka na mambo muhimu kama hayo
 

..Mgogoro wa Afrika Kusini ulihusisha pande mbili zilizokuwa na silaha.

..ANC, PAC, na vyama vingine vya Waafrika, vilijihusisha na mapambano ya silaha, na vilihusika na mauaji.

..Kwa hiyo, Waafrika walipokwenda kwenye maridhiano walikuwa wanakwenda kuwaomba radhi Wazungu waliowawa kimakosa.

..Hoja uliyoijenga ni ya msingi kweli kweli. Mpaka sasa hivi Ccm hawajaeleza Chadema imewakosea nini wao, wala Watanzania.
 
Kwamba, taifa zime tunatakiwa tukubali kuwa CCM ndio mtawala wetu wa milele na hisia yoyote ya kuichukia na kutaka kuitoa madarakani ni sawasawa na kutenda dhambi fulani ambayo watu wanatakiwa kuungama na kufikia toba!
Pascal Mayalla na Ccm wenzako ikiwemo Spika mstaafu Tulia mlituimbia sana hili pambio la Ccm kutawala milele.
 
Samia ni mcha Mungu sana, hapendi siasa za chuki, uhasama, fitina na uadui. Anataka siasa za kistaarabu. Hiyo maridhiano, ni kutaka kujenga uhusiano mwema, na hao wanaojifanya wapinzani.
Angekuwa kweli ni mtu muadilifu hivo asingekubali kuapishwa kwa matokeo ya uongo.
 
Rais Samia kahubiri na kuyatenda maridhiano toka aliposhika madaraka....Alimualika na hatimaye kumleta Lissu kutoka ughaibuni kwa nia njema ya maridhiano ...unaikumbuka 4 R ??
SWALI MUHIMU ...NI NANI HUYU NYUMA YENU ASIYETAKA NCHI IRIDHIANE...ANAFANYA HIVI KWA MASLAHI YA KINA NANI?
PASIPOKUWA NA MARIDHIANO MAANA YAKE PAWE NA NINI??
 
Kabla na baada ya Uchaguzi
Makamu Mwenyekiti bara Ndugu Wasira Masato huwa anasema kuwa CCM inaridhiana na wananchi.
Huwa sijui hayo maridhiano huwa ni ya nini ?
 
Jiwe aliua watu 10k? Jiwe alifanya ufisadi?
Kwendeni zenu wadini wakubwa na wanafiki nyie! Wapuuzi na matahila wanawaunga mkono kwa ujinga wao wakutokujua,mna chuki na Rais akiwa muislam...

Ili ujue kuwa Jiwe alikuwa fisadi angalia jinsi alivyomsumbua CAG, ili tu asianike ufisadi wake na serikali yake,ukiona kiongozi anapambana na CAG Moja kwa moja ujue uyo ni fisadi na jizi kubwa,ila nyie mazuzu alikuwa anawadanganya kuwa yeye ni mtetezi wa wanyongwe,wakati ni jizi tu...
 
Maridhiano ya kweli yaanzie kwenye upatiakanaji wa viongozi wanaotokana na wananchi (uchaguzi wa huru, wazi na haki )

Haiwezekani, Serikali iliyopo madarakani kwa asilimia 98 bado wananchi wanapotea, wanatekwa na kubambikiwa kesi za uongo.

Tupate viongozi wanaotokana na kura zetu kuanzia Serikali za mitaa, vijiji, vitongoji, kata, majimbo ma taifa kwa ujumla hapo ndipo tutakuwa tumefungua njia ya maridhiano.
 
Jiwe hajaua Watanganyika 10k. Jiwe hakupata div 4 ya D2.
 


Huoni hata aibu, alimleta Lissu kwani Lissu sio mtanzania wa kuzaliwa mwenye haki ya kuishi sehemu yoyote Tanzania?..

Hebu elezea nini kwanza kilimtoa Lissu Tanzania.

Kuhusu 4R za Samia , ni uthibitisho zilikua ni utapeli maana R moja kati ya 4 ni REFORMS kitu cha ajabu uchaguzi wa serikali za mitaa ambao ndio ulikua wa kwanza Samia akiwa rais haukua na tofauti yoyote na ule wa 2019 chini ya Magufuli.

Samia alibadili jina la tume na kuiita huru ilhali muundo umebaki ule ule ni sawa na kubadili chupa ya mvinyo ila mvinyo na kiwango cha kileo kinabaki kile kile.

Lissu aliona mbali ndio maana alipokua mwenyekiti hakuona sababu yoyote ya CHADEMA kushiriki ujinga ulioitwa uchaguzi ilhali ni uteuzi wa maccm na ndio wakaona wampe kesi ya kubumba ya uhaini ila alichokua anakidai ni reforms ambazo Samia alizihubiri kumbe hakua tayari kwa reforms za kweli bali maigizo.
 

..sio kweli.

..Ssh alianza vizuri alipokuja na 4R.

..hapo katikati kuna mtu alimshauri atumie nguvu badala ya reforms na maridhiano.

..kwa upande mwingine, zile BILLION 200 alizochangiwa zilikuwa zinatosha kulambisha watu wote asali, na Oct 29 asingekufa hata sisimizi.
 
Walioruhusu watu wauawe chini ya utawala wao watalipia hapa duniani (Tanzania) na akhera.
 
Samia ni mcha Mungu sana, hapendi siasa za chuki, uhasama, fitina na uadui. Anataka siasa za kistaarabu. Hiyo maridhiano, ni kutaka kujenga uhusiano mwema, na hao wanaojifanya wapinzani.
Hata yeye anakuona wewe ni fala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…