PreGE2025 Mavunde kuwania ubunge jimbo jipya la Mtumba, atoa sababu tatu za kuiacha Dodoma mjini

PreGE2025 Mavunde kuwania ubunge jimbo jipya la Mtumba, atoa sababu tatu za kuiacha Dodoma mjini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mbunge wa Dodoma Mjini (CCM), Anthony Mavunde ametangaza katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 atagombea tena ubunge katika Jimbo jipya la Mtumba, akianisha sababu tatu za kuiacha Dodoma Mjini.
Uamuzi huo ameutangaza huku akilia kuwa hakuna namna na hawezi kujigawa katika maeneo mawili akabaki salama.

Mavunde ambaye ni Waziri wa Madini ametangaza uamuzi huo leo Alhamisi Mei 15, 2025 mbele ya wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Pia, Soma: Tume Huru ya Uchaguzi yatangaza majimbo mapya nane, Dar es Salaam yapata Kivule na Chamazi

Ametaja sababu ya kuhama Jimbo la Dodoma Mjini ni amani ya nafsi, pia kuendeleza ujenzi wa barabara za Ihumwa, Hombolo hadi Mayamaya na Ntyuka -Mvumi ambao alianzisha.

Pia mradi mkubwa wa Hombolo Thematic City na Bandari kavu ya Ihumwa.

Mei 12, 2025 Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi (INEC), Jaji Jacobs Mwambegele alitangaza mgawanyo mpya wa majimbo uliosababisha kuzaliwa kwa majimbo mapya manane ya uchaguzi na kufikisha jumla ya majimbo 272, Tanzania Bara na Zanzibar.

 
Safi sana, amejikatia mkate wake wa milele hataki competition
 
Kugawanywa majimbo ni kwenda kuwajaza na taletale, kibajaj n the like wengi zaidi.
Ni vyema wabaki haohao
 
Hana lolote huyu..yaani ile haiba ya umaskini wa kigogo unaiona wazi..anapigania vitu vidooogo, dodoma hadi sasa kulipaswa uwepo mradi wa maji ya uhakika toka ziwa victoria..kingine ni matumizi ya mkaa yanaimaliza dodoma..anashindwa ku-push bomba la gas lije dodoma? anang'ang'ana na vitu vidoooogo na havina impact yoyote kwa uchumi wa dodoma, huyu hata upadri asingeuweza kwa namna alivyo!so dull..
 
Dodoma kajitahidi kujenga vibanda vya bati na turubai wapadk boda boda. Kingine ni kuwagawia reflectors boda boda wavae zimiwa na jina lake. Hakuna impact ya maana naiona katika nafasi yake ya Ubunge hapa Dodoma
 
DODOMA: MBUNGE wa Dodoma Mjini ambaye pia ni Waziri wa Madini, Antony Mavunde jana Mei 15, 2025 amemwaga machozi wakati akitangaza kugombea ubunge katika Jimbo jipya la Mtumba iwapo atapitishwa na chama chake (CCM).

Akitoa tamko hilo kwenye mkutano maalumu wa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Dodoma, Mavunde alisema kuwa ametafakari baada ya kusikiliza na kupima hoja mbalimbali na kuamua jambo hilo ili apate amani ya nafsi.

Alisema kuwa amepitia jumbe mbalimbali kwenye makundi sogozi ya WhatsApp ambazo zimemtia unyonge.

"Niombe tusipeleke jambo hili kwenye ushabiki na kudhihakiana, Hii ni siku ngumu sana kwangu. Natangaza Uchaguzi ujao nitagombea Jimbo la Mtumba.” Alisema Mavunde huyo huku akichukua kitambaa na kujifuta machozi.

Mavunde alisema kuwa anazo sababu kwani kwenye jimbo hilo kuna changamoto nyingi zinazogusa maisha ya watu.

Kwenye Jimbo hilo jipya la Mtumba kuna Hombolo Satellite City ambayo inakwenda kujengwa, ukiwa ni mradi wa kimkakati na pia kuna ujenzi wa Ihumwa Yard na hayo yote yanahitaji usimamizi.

"Lile ni jimbo jipya, lina changamoto nyingi zinazogusa watu wengi ili nao wafaidike na matunda ya uongozi wangu,” Alisema Mavunde na kuongeza,

"Nikipitishwa kuwa mgombea nitafanya kampeni kwenye maeneo yote na iwapo nitateuliwa nitakuwa mbunge wa wote.” Alisema.

Awali kabla ya kutangaza uamuzi huo alisema Rais Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa katika Jimbo la Dodoma Mjini kutokana na kuwa na miradi mingi na kuifanya Dodoma iendelee kung'ara.

Kwa upande wake Katibu wa CCM Wilaya ya Dodoma, Sophia Chibaba alisema mgawanyo wa Jimbo la Dodoma utaleta ufanisi ikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Source: Habari Leo
IMG_6737.jpeg
 
Aende kwanza huko kitongoji cha muungano kata ya makutupora akamalize kero ya watoto wadogo mpaka wa chekechea kutembea mpaka kilomita 8 kwa siku kufata shule......ndio alie sasa tumuone
 
Hawa kijani wanapenda kububujikwa machozi kama mbinu yao, ndio kina Mashambwa
 
Bro namuona-ga ana akili leo amekumbwa na nini?
 
Ni Machozi Ya Furaha Kama Anayomwagaga Mjumbe Mwenzake Humu Ndani Au Ya Huzuni?
Cc:Lucas Mwashambwa
 
u
Mbunge wa Dodoma Mjini (CCM), Anthony Mavunde ametangaza katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 atagombea tena ubunge katika Jimbo jipya la Mtumba, akianisha sababu tatu za kuiacha Dodoma Mjini.
Uamuzi huo ameutangaza huku akilia kuwa hakuna namna na hawezi kujigawa katika maeneo mawili akabaki salama.

Mavunde ambaye ni Waziri wa Madini ametangaza uamuzi huo leo Alhamisi Mei 15, 2025 mbele ya wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Pia, Soma: Tume Huru ya Uchaguzi yatangaza majimbo mapya nane, Dar es Salaam yapata Kivule na Chamazi

Ametaja sababu ya kuhama Jimbo la Dodoma Mjini ni amani ya nafsi, pia kuendeleza ujenzi wa barabara za Ihumwa, Hombolo hadi Mayamaya na Ntyuka -Mvumi ambao alianzisha.

Pia mradi mkubwa wa Hombolo Thematic City na Bandari kavu ya Ihumwa.

Mei 12, 2025 Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi (INEC), Jaji Jacobs Mwambegele alitangaza mgawanyo mpya wa majimbo uliosababisha kuzaliwa kwa majimbo mapya manane ya uchaguzi na kufikisha jumla ya majimbo 272, Tanzania Bara na Zanzibar.

unajenga Barbara kwa hela zako?
 
Back
Top Bottom