Mawakala wa M-PESA, TIGOPESA na AIRTELMONEY tunaochukua namba za warembo kupitia miamala tukutane hapa.

Bodaboda wanatuharibia sana mahaus girl

Sifa ya Bodaboda,huwa HAKUBALI MIMBA
Kuna Bodaboda mmoja huenda alikosea namba au aliingizwa mjini kwa kupewa namba sio sahihi.

Namba aliyoinasa ilikuwa yangu.

Akaanza kurusha ndoana kama kawaida yao kwa sms, mara paap sms ikaingia kwangu nikaicheki nikaona namba ni ngeni kwangu huku ujumbe ukawa unanitaka niende alipo. Nikamuuliza wewe ni nani na uko wapi? akaniambia niko geto, mimi ni Bodaboda ninayekupelekaga sokoni.

Hapo nikabaini kuwa kakosea namba nikamueleza umekosea namba, akakausha. Siku nyingine tena akarudia kunitext tena kwa kurusha ndoana kama kawaida yake, nikaamua kumpa makavu hadi leo hii hajarudia tena.

Hawa Boda boda wamezidi sana bora ninyi wanawake muwe mnanapewa namba hata za gari kabisa ili wakitaka kuwatafuta waambulie patupu.
 
Na hapa sijui nani aliwadanganya kuwa kuzungusha ndo kipimo cha ubora wa mwanamke na kipimo cha kumpima mwanaume kama amepende. Namuona hata emmyta ameongelea hapo juu. Unaweza kupishana na mtu sahihi kabisa kisa tu uavutavuta muda

Hahahaaa. Mwenye nia ya kweli anaonekana mkuu hivyo hata kiwango chake cha kuzungushwa kinakuwa kidogo.
 
Hahahaaa. Mwenye nia ya kweli anaonekana mkuu hivyo hata kiwango chake cha kuzungushwa kinakuwa kidogo.
Ha ha haaa, ujue nacheka sana kwa sababu nnareflect what is happening here down the street.
Ila nyie mna visa sana...................
 
Ndio Swahiba sasa utasifia nini kwenye kumpata mwenza wako ikiwa umemuomba namba tu akakupa, umerusha ndoano tayari ameshanasa mi sioni kama ni raha aisee, lazima ukikaa na mwenza wako saa nyingine ukumbushie ulivyosota hadi kumpata.

Dada yangu buana[emoji2]
 
Haha swahiba kwenu mnaona sawa, ila wapo wanaume wengine ukimzungusha sana atakomaa na wewe hadi mwisho siku unaachia tu anakula alafu humuoni tena
Watu kama hao hawakwepeki saa nyingine ila tu nikwambie Swahiba walio wengi wa hivyo huwa wanakata tamaa haraka na ukiona mtu king'ang'anizi basi jua huyo ana uhitaji wa mweli.
 
Ila sasa hapo unakuwa unacheza pata potea. Sababu kama mtoa uzi anakwambia aliambulia za mbavu.
Mtoa mada kuna kosa alilifanya baada ya kupata namba..............
Kwa hali ya sasa mtu yeyote makini akipata namba toka kwa mtu asiyemjua lazima awe makini sana, hawez kukurupuka tu....kwa hiyo ilimpasa kujipanga namna ya kumuondoa mashaka kwakua mhusika anaichukulia ile ni kama namba mpya na mtu siyemjua
 
Watu kama hao hawakwepeki saa nyingine ila tu nikwambie Swahiba walio wengi wa hivyo huwa wanakata tamaa haraka na ukiona mtu king'ang'anizi basi jua huyo ana uhitaji wa mweli.
Hiv unajua wapo wanawake wanavishwa mpaka pete ya uchumba na bado jamaa anakula kona
 
Hahahaa. Kweli ujue mdogo wangu saa nyingine mnaweza kaa hamna vya kuzungumza basi inatokea tu mnajikuta mnakumbushia ya nyuma hadi kufikia kuwa ilivyo sasa.
Kweli Dada yangu, ngoja na mimi siku moja nitaliprove hili jambo maana haliepukiki[emoji2] [emoji2]
 
Kweli kabisa usemalo mkuu ila siku hizi kwa jinsi dunia ilivyoharibika na watu wasiojulikana walivyokuwa wengi ni mara chache sana eti ukosee namba hata kama mwenye simu atakupokea kiungwana hawezi kupa ushirikiano utakaouhitaji.

Zaidi ya kukwambia umekosea namba na kukukatia simu na walio wengi huwa hawapokei tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…