Mwifwa
JF-Expert Member
- Apr 3, 2017
- 48,474
- 125,866
Bodaboda wanatuharibia sana mahaus girl
Kuna Bodaboda mmoja huenda alikosea namba au aliingizwa mjini kwa kupewa namba sio sahihi.Sifa ya Bodaboda,huwa HAKUBALI MIMBA
Namba aliyoinasa ilikuwa yangu.
Akaanza kurusha ndoana kama kawaida yao kwa sms, mara paap sms ikaingia kwangu nikaicheki nikaona namba ni ngeni kwangu huku ujumbe ukawa unanitaka niende alipo. Nikamuuliza wewe ni nani na uko wapi? akaniambia niko geto, mimi ni Bodaboda ninayekupelekaga sokoni.
Hapo nikabaini kuwa kakosea namba nikamueleza umekosea namba, akakausha. Siku nyingine tena akarudia kunitext tena kwa kurusha ndoana kama kawaida yake, nikaamua kumpa makavu hadi leo hii hajarudia tena.
Hawa Boda boda wamezidi sana bora ninyi wanawake muwe mnanapewa namba hata za gari kabisa ili wakitaka kuwatafuta waambulie patupu.