A
Anonymous
Guest
Habari, naitwa Fadhili, ninaishi Dar es Salaam na ni Wakala Mkuu wa HALOPESA, Tawi la Temeke.
Mawakala Wakuu wa HALOPESA hadi leo hatujalipwa stahiki zetu za kamisheni za mwezi Septemba. Kuna bosi mpya wa HALOPESA aliyeanza kazi mwaka huu 2026, anaitwa NGHIEM ANH THONG, raia wa Vietnam. Tangu alipoanza kazi, amewafuta kazi Mawakala Wakuu karibu 10.
Yaani, ukienda kulalamika kuhusu kamisheni au suala lolote, unafutwa kazi, na huwezi kwenda popote kwa sababu hadi leo hatuna mikataba. Tulijaza mikataba miwili na kupeleka makao makuu, lakini hadi leo haijarudi. Kwa sasa tupo Mawakala Wakuu 382.
Pia, kuna tetesi kwamba kamisheni zinakatwa na kuna fedha zinazochukuliwa bila maelezo. Tunaomba mamlaka zinazohusika, TCRA na BoT, ziingilie kati suala hili. Tunaogopa kwenda popote kwa sababu tunahofia kukosa hata hicho kidogo tunachopata.
Tumewekeza fedha nyingi, lakini wao hawaoni shida yoyote Wakala Mkuu anapoingia hasara. Tunapata shida kwa ajili ya mtu mmoja ambaye hajui hata tunavyohangaika.
Hiyo picha ndiyo inayoonesha fedha zinazotakiwa kulipwa. Nimeshatoa risiti, na sisi pia tunalipa kodi. Tunaomba mtupazie sauti ili tulipwe stahiki zetu, tafadhali. Tuna wafanyakazi ambao hadi sasa hatujawalipa. Kuna vijana wengi wanaotegemea fedha hizi; siku wakiamua kutuondoa, vijana wengi watakosa ajira.