Mawakili Kutetea Mafisadi na Uzalendo

Mawakili Kutetea Mafisadi na Uzalendo

kwa kweli mimi nimudhiwa sana na huyo sophia simba how dare her insulting a man like Regi, Regi is tanzania's a lot of peoples saviors je hao wahindi mafisadi alimuona nani akitoa msaada kwa jamii au hata kupa soda za bure tu kama sio wanaendelea na kuendelea kujilimbikizia mali kina inapowezekana kutokana na tamaa za watanzania wachache wanaowaendea hao gabacholi. can u believe a tanzanian minister talking bulsheet kwneye vyombo vya habari eti labda wanamaugomvi yao, the issue here is ufisadi na si vinginevyo. she must be one of them.

it is high time tuandame tanzania nzima labda huyo numberi wani hasikii au hajali watu anaowaongoza tukiandamana itamwingia kwenye akili yake. wahindi wananguvu bwana wanajua jinsi ya kutumia pesa ambazo sihalali yao.

nawasilisha kwa uchungu
 
Inadhihirisha watz tusivyojipenda ama kuwapenda watu weusi wenzetu.

Muhindi yeyote yule si wetu huyo.....

Mengi kawajibu vizuri sana,....ooohhh my God,...Sofia ni kilaza na zezeta.
 
Inadhihirisha watz tusivyojipenda ama kuwapenda watu weusi wenzetu.

Muhindi yeyote yule si wetu huyo.....

Mengi kawajibu vizuri sana,....ooohhh my God,...Sofia ni kilaza na zezeta.
wacha ubaguzi wewe
 
ujumbe umefikia

mkulu wa kaya rais wa waislamu jmk kaupata.

2010 hana kura za wakristo.
 
Nani kakwambia Wakatoliki inendeshwa kihaki? ill informed!!! watoto kibao wa kiume wamelawitiwa na mapadre, bado mfalme wao anawatetea na kuwalinda, Rome haina tafauti na CCM mafisadi wanalindwa, wanalindana kwa taarifa yako

umeleta udini wako hapa,kuna walawiti wakubwa kama masheikh? kwikwikwi
 
Wana JF, najua kila mtu anayo haki ya kum-engage wakili amtetee katika kesi yake. Lakini hii ya mawakili kuwatetea mafisadi mahakamani je mawakili wanaokubali kuwatetea ni wazalendo kweli au kwao la muhimu ni business? Na lengo la kuwatetea hawa mafisadi si ni kwamba washinde kesi na kuachiwa? Je mawakili hawa wana uchungu na mali za nchi yetu? I'm not biased nachokoza mada tu tuijadili.
 
Wana JF, najua kila mtu anayo haki ya kum-engage wakili amtetee katika kesi yake. Lakini hii ya mawakili kuwatetea mafisadi mahakamani je mawakili wanaokubali kuwatetea ni wazalendo kweli au kwao la muhimu ni business? Na lengo la kuwatetea hawa mafisadi si ni kwamba washinde kesi na kuachiwa? Je mawakili hawa wana uchungu na mali za nchi yetu? I'm not biased nachokoza mada tu tuijadili.

Mkuu JB,

Hili linaweza kuwa na utata kutegemea na mtu anayeliangalia. Kama wewe ni mchukia ufisadi, na uko tayari kufa njaa kuliko kuwa upande mmoja na mafisadi basi itakuwa vigumu kuwatetea. Lakini wengi nadhani wanatafuta pesa na hawajali hizo pesa zinatoka wapi, nani anaumia n.k. Hili pia linawagusa waandishi wanaotetea ufisadi. Jamii sasa inatakiwa kugawanyika ili tujue nani yuko upande upi an anatetea maslahi ya na nani. Vinginevyo tutaendelea kujidanganya na kudanganyana. Ngoja tupate maoni ya wadau wengine.
 
Nenda ufungue vitabu vya sheria vinasemaje au waulize wanasheria utapata majibu mazuri sana.


Mimi sidhani kama hilo lina ubishi. Lakini kwani mawakili hawaruhusiwi kupima hali halisi na kuangalia aina ya mtu anayemtetea? Kuna usemi wa madaktari unaosema kuwa "diseses never read books". Kwani hilo haliwahusu mawakili?
 
Wana JF, najua kila mtu anayo haki ya kum-engage wakili amtetee katika kesi yake. Lakini hii ya mawakili kuwatetea mafisadi mahakamani je mawakili wanaokubali kuwatetea ni wazalendo kweli au kwao la muhimu ni business? Na lengo la kuwatetea hawa mafisadi si ni kwamba washinde kesi na kuachiwa? Je mawakili hawa wana uchungu na mali za nchi yetu? I'm not biased nachokoza mada tu tuijadili.

Jibaba,
Mawakili hufanya kazi yao kwa kufuata misingi iliyowekwa na katiba na sheria za nchi. Kama ukisoma katiba vizuri utaona kuwa mawakili wanaruhusiwa kumtetea yeyote kwa kuwa watu wote ni sawa mbele ya sheria na hakuna aliye na haki zaidi.
Ibara hiyo nainukuu hapa chini:
13. (1) Watu wote ni sawa mbele ya sheria na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria.

13. Usawa mbele ya sheria Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 8; 3 ya 2000 ib. 5
(1) Watu wote ni sawa mbele ya sheria na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria.
(2) Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake.
(3) Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu na jumuiya ya watu yatalindwa na kuamuliwa na Mahakama na vyombo vinginevyo vya Mamlaka ya Nchi vilivyowekwa na Sheria au kwa mujibu wa sheria.
(4) Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya Mamlaka ya Nchi.
(5) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara hii neno "kubagua" maana yake ni kutimiza haja, haki au mahitaji mengineyo kwa watu mbalimbali kwa kuzingatia utaifa wao, kabila, pahala walipotokea, maoni yao ya kisiasa, rangi, dini, jinsia au hali yao ya maisha kwa namna ambayo watu wa aina fulani wanafanywa au kuhesabiwa kuwa dhaifu au duni na kuwekewa vikwazo au masharti ya vipingamizi ambapo watu wa aina nyingine wanatendewa tofauti au wanapewa fursa au faida iliyoko nje ya masharti au sifa za lazima, isipokuwa kwamba neno "kubagua" halitafafanuliwa kwa namna ambayo itaizuia Serikali kuchukua hatua za makusudi zenye lengo la kurekebisha matatizo katika jamii.
(6) Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria, Mamlaka ya Nchi itaweka taratibu zinazofaa au zinazozingatia misingi kwamba–
(a) wakati haki na wajibu wa mtu yeyote vinahitaji kufanyiwa uamuzi wa mahakama au chombo kinginecho kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa na haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na pia haki ya kukata rufaa au kupata nafuu nyingine ya kisheria kutokana na maamuzi ya mahakama au chombo hicho kinginecho kinachohusika;
(b) ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo;
(c) ni marufuku kwa mtu kuadhibiwa kwa sababu ya kitendo chochote ambacho alipokitenda hakikuwa ni kosa chini ya sheria, na pia kwamba ni marufuku kwa adhabu kutolewa ambayo ni kubwa kuliko adhabu iliyokuwapo wakati kosa linalohusika lilipotendwa;
(d) kwa ajili ya kuhifadhi haki ya usawa wa binadamu, heshima ya mtu itatunzwa katika shughuli zote zinazohusu upelelezi na uendeshaji wa mambo ya jinai na katika shughuli nyinginezo ambazo mtu anakuwa chini ya ulinzi bila uhuru, au katika kuhakikisha utekelezaji wa adhabu;
(e) ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazomtweza au kumdhalilisha.


hivyo basi wakili anapomtetea fisadi anatimiza wajibu wake wa kikatiba.

Pia ukumbuke kuwa chombo pekee chenye mamlaka ya kutamka kuwa mtu ana hatia ya kosa lolote ni mahakama. Hii ni kwa mujibu wa ibara ya 107 ya katiba ya nchi yetu ambayo nainukuu hapa kwa faida yako na wengine.

107A. (1) Mamlaka ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano itakuwa mikononi mwa Idara ya Mahakama na Idara ya Mahakama ya Zanzibar, na kwa hiyo hakuna chombo cha Serikali wala cha Bunge au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kitakachokuwa na kauli ya mwisho katika utoaji haki.
(2) Katika kutoa uamuzi wa mashauri ya madai na jinai kwa kuzingatia sheria, Mahakama zitafuata kanuni zifuatazo, yaani–
(a) kutenda haki kwa wote bila ya kujali hali ya mtu kijamii au kiuchumi;
(b) kutochelewesha haki bila sababu ya kimsingi;
(c) kutoa fidia ipasayo kwa watu wanaoathirika kutokana na makosa ya watu wengine, na kwa mujibu wa sheria mahususi iliyotungwa na Bunge;
(d) kukuza na kuendeleza usuluhishi baina ya wanaohusika katika migogoro.


Baada ya kukueleza haya nafikiri utagundua kuwa mafisadi nao pia wana haki ya kusikilizwa na kama kuna mtu anao ushahidi kuwa wameiba basi na aulete mahakamani ithibitishwe.

Hivyo kazi ya wakili ni kujaribu kuiridhisha mahakama kuwa ule ushahidi haujitoshelzi kumtuhumu mtu.

Kama bado una nia ya kuchokoza mada na mjadala karibu tukusaidie.
 
Chaumbeya,

Sio tu watu wote ni sawa mbele ya sheria lakini pia wanasheria wanakula kiapo kutenda hiyo haki bila ubaguzi.

Ni sawa na daktari tu kumwambia akatae kumtibu jambazi au fisadi.

Mwanasheria aanayejua wajibu wake na anayeheshimu maadili ya kazi yake anawajibika kumtetea mtu yeyote ili mradi masharti mengine kama malipo na mambo mengine yametimia.

Kuwaandama mawakili kwenye hili labda ni kwasababu sisi wenyewe hata hatujui sheria zetu na zile za dunia zinasemaje. Kwa mtu anayejua hawezi hata ku question uzalendo wa wakili kwasababu tu eti kamtetea mtu ambaye ni jambazi, fisadi au mwuuaji.
 
Chaumbeya, sijasema kuwa mawakili hawafanyi kazi zao kwa misingi ya sheria na wala mada yangu haiko huko. Argument yangu si watetewa(mafisadi) bali uhusiano wa wanaowatetea (mawakili) na uzalendo wao (mawakili). Ni kweli ni mahakama tu yenye uwezo wa kumtia hatiani mtu lakini uzalendo wa mawakili upo wapi? kwanini wasifanyie utafiti wa ushahidi uliopo ili kubainisha ukweli ama uongo wa tuhuma zinanzowakabiri mafisadi halafu ndiyo waamue kuwatetea(kama wamejilidhisha kwamba ushahidi uliopo siyo wa kweli) ama wasiwatetee kabisa kama wamejilidhisha na ushahidi? je ni business au? kumbuka mawakili ni wananchi na wanaguswa kwa namna moja au nyingine na athali za ufisadi huu. je wana uzalendo kweli? na sisi wananchi wanyonge tusiojua sheria nani atatusaidia kutukomboa maana nilitegemea katika hili mawakili wawe mstari wa mbele kutetea mali ya wananchi isiibie kifisadi au kwa namna yoyote ile.
 
teh teh nadhani wadau mnaotumia nambari za VODA mnawachangia mitaji mafisadi kwani hamjui kuwa RA ni mwanahisa mkubwa wa VODA? teh teh

Nchi imetekwa nyara na wachache. ni utashi wa dhati wa viongozi ndio utakaotuokoa.
 
Nenda ufungue vitabu vya sheria vinasemaje au waulize wanasheria utapata majibu mazuri sana.

Mimi sidhani kama hilo lina ubishi. Lakini kwani mawakili hawaruhusiwi kupima hali halisi na kuangalia aina ya mtu anayemtetea? Kuna usemi wa madaktari unaosema kuwa "diseses never read books". Kwani hilo haliwahusu mawakili?

In that context, kuna watu wengi sana hawatakiwi kuoatiwa huduma na mawakili, Zombe, Watuhumiwa wa Ujambazi, you name it... Ukuhisiwa au kutuhumiwa wewe ni muhalifu basi Mawakili waweke njaa na professional yao nyuma WAKUNYANYAPAE. GO TZ GO.

Kuna jirani yangu mmoja anawatetea wezi wa SAMAKI WA MAMIA YA TANI
 
Tatizo ni pesa. Mawakili pamoja na kuwaheshika mawakali na wanasheria na wengi ni marafiki zangu taaluma yao 'ni scavengers of money". Wao wanaposikia kuna mgogoro ndio furaha yao. Hivyo ndio maana unasikia mawakili wengi wanachochea watuhumiwa mafisadi papa waende mahakamani. Hii ndio DECI yao na sasa ni wakati wa kuvuna! Lakini kuna wengine kama wazee wa yanga ambao kimsingi ni omba-omba. Kwao hata kama ni hela za wizi ni sawa mradi wanafadhiliwa na Manji. Mzee Kenyatta aliwaita watu wa namna hii kama "walambaji wa ****** ya.......". Kuna wale amabao kwa namna moja au nyingine wanafaidika na ufisadi ama kwa kufanya biashara na watuhumiwa au kuajiriwa nao. Unategemea nini kutoka kwa kundi hili kama sio kusema " mfalme kavaa nguo" hata kama yuko uchi?!
 
Mimi shida yangu iko kwa mahakimu ambao hukubali kununuliwa na mafisadi wakapindisha sheria na kuwa acha huru!

Ebu fikiria yule hakimu alivo vurunda kumpa dhamana Liumba? yaani hata mtoto wa darasa la nne alikuwa na uwezo wa kuona kwamba haiji!

Nina hakika mahakama isipo ingiliwa, na mahakimu wakawa wazalendo kwa kutopindisha sheria, ahhhh.. mbona keko patakuwa hapatoshi?
 
Mimi naona wote hao ni VILAZA tu. Hawana jipya kwetu watanzania.
 
Hao wanaotetea mafisadi wasome barua ya Salva kwa fisadi wake na waone kama ukitetea fisadi akifanikiwa atakukumbuka. Fisadi ni fisi aktakula mpaka atapike na ale matapishi yake na atapike tena.
Salva Rweyemamu aliambulia kazi ya ukurugenzi Ikulu at the expense of his dignity among his fellow jounalists kwani he proved that he is a mamluki!!
 
Last edited:
Back
Top Bottom