Mawakili na Wanasheria wafika gerezani kuzungumza na aliyehukumiwa miaka 22 jela kwa kukutwa na nyama ya swala

James Hadley Chase

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2020
Posts
1,984
Reaction score
3,695

Chama Cha Mapinduzi wa Iringa kwa kushirikiana na Mawakili wa TLS pamoja na Wanasheria toka Jumuiya ya Wanawake Taifa kufuatia Tamko la Mwenyekiti Merry Chatanda kuhusu kesi ya mama Maria Ngonda aliyehukumiwa miaka 22 kisa nyama ya swala jopo hilo lilifika gerezani na kuzungumza na mama huyo ili kuona namna gani ya kumsaidia.

Tiyari jopo la wanasheria wanawake wameshafika mkoani Iringa kwaajili ya usikilizwaji wa kesi hiyo upya na tiari wameshaonana na mama Maria Ngoda na kuongea na mawakili pamoja na wanasheria


Mwenyekiti wa umoja wa wanawake mkoa wa Iringa Zainabu Mwamwindi amesema wanaimani mwanamke mwenzao atapatiwa haki yake

Ikumbukwe mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Iringa ilimuhukumu kifungo cha miaka 22 jela Maria Ngonda mkazi wa mtaa wa zizi la n’gombe iliyopo manispaa ya Iringa baada ya kukutwa na hatia ya kukutwa na ndoo yenye vipande 12 vya nyama ya swala kinyume na sheria.
 
mbona hizo sura sio za mahakamani, sijawahi kuziona kwenye mahakama yeyote? wanauza sura tu hao na nguo zao za majani. mahakama sio siasa.
 
Nimecheka kufa [emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
These people are heathens!Hawajifunzi hadi litokee tukio la kuamsha hisia za jamii tu utadhani wanatokea Jupiter.Wana tofauti gani na yule aliyejiliza jana kaburini utadhani siku zote hakujua kama hilo kaburi lipo Chato.Maigizo.
 
Mbona ni kama wanachama wamekwenda kwenye ofisi za chama
 
Eti wanatatua kero, kwanini wasiwe proactive ili hizo kero zisitokee?
Kuna mtu anazunguuka huku na kule akitoa amri eti anatatua kero, kero zoote hizi zimesababishwa na serikali ya CCM. Mfano kero ya viwanja (double allocation) wizara iko chini ya waziri wa CCM, siku zote waziri Yuko wapi mpaka watendaji wanauza kiwanja kimoja kwa watu wanne?
 
Upendeleo wa wazi wazi wa kijinsia huu, angekuwa mwanaume wala wasingejisumbua
 
Hilo chama linawafanya watanzania wanasesere. Eti makonda anajifanya magu, hiyo ni mbinu ya kuwadanganya wajinga wachache.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…