Mawakili wa Makonda na Le Mutuz waomba kumtafuta aliyedai kutapeliwa Range Rover

Mawakili wa Makonda na Le Mutuz waomba kumtafuta aliyedai kutapeliwa Range Rover

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
KONDAMA.jpg

Suala la Uraia wa Mfanyabiashara Patrick Kamwelwe limeibuliwa Mahakamani kwenye kesi ya Utapeli inayowahusu aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na William Malecela (Le Mutuz).

Mawakili wa Makonda na Le Mutuz wamedai kuwa wameshindwa kumpata Kamwelwe anayetaka kulipwa Tsh. Milioni 247.2 kwa maelezo ya kutapeliwa gari aina Range Rover, hivyo wameiomba Mahakama kumtangaza kwenye Vyombo vya Habari kwa sababu jitihada zao zimeshindikana.

Paul Makonda na William Malecela (Le Mutuz) walifungua maombi madogo baada ya kuwa na shaka na uraia wa Mfanyabiashara huyo kwa maelezo kuwa hana mali zinazohamishika Nchini.

====================

URAIA wa mfanyabiashara Patrick Kamwelwe, aliyemfungulia kesi ya madai aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa DSM, Paul Makonda na William Malecela, umeibua utata baada ya mawakili wa wadaiwa hao kuiomba mahakama imtangaze kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwa sababu wameshindwa kumpata.

Makonda na Malecela ambaye ni mmiliki blogu ya Lemutuz, walifungua maombi madogo baada ya kuwa na shaka na uraia wa Kamwelwe na kutokuwa na mali zinazohamishika nchini, kwa sababu kisheria anatakiwa kulipa gharama za uendeshaji wa shauri hilo.

Taarifa hiyo ilitolewa jana na wakili wa wajibu maombi hao, Reuben Simwanza, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rhoda Ngimilanga wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kusikilizwa.

Simwanza alidai kuwa wameshindwa kumpata Kamwelwe, hivyo wanaiomba mahakama hiyo kumtangaza kwenye vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu jitihada zao zimeshindikana.

"Tumefanya jitihada za kumtafuta Kamwelwe lakini imeshindikana, hivyo naiomba mahakama itupe ruhusa ili tuweze kumtangaza kwenye vyombo vya habari pamoja na kwenye mitandao ya kijamii," alidai Simwanza.

Alidai kuwa kesi ilipoitwa kwa mara ya mwisho, wakili anayemwakilisha Kamwelwe, Wabeha Kung'e, alijiondoa kwenye kesi ya msingi na kesi ndogo iliyofunguliwa.

"Kwa hivyo tunaomba tumtangaze kwenye magazeti na mitandao ya kijamii ili aweze kulipa gharama za uendeshaji wa shauri alilolifungua na tunaomba mahakama hii itumie busara ili kesi iendelee upande mmoja,"alidai Simwanza.

Desemba 8, 2022 Wakili Kung'e aliyekuwa akimwakilisha Kamwelwe alijiondoa kwa sababu mlalamikaji (mteja wake) alishindwa kumpatia maelezo sahihi ili kujibu hoja zilizotolewa na wajibu maombi (Makonda na Lemutuz).

Baada ya maelezo hayo mahakama hiyo iliahirisha shauri hilo hadi Machi Mosi, 2023 kwa ajili ya usikilizwaji mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate ambaye ndiye anayesikiliza shauri hilo.

Kamwelwe anayeishi New York, Marekani, amefungua kesi ya madai namba 234/2022 dhidi ya Makonda na Malecela maarufu kama Le Mutuz akiwataka wamlipe fidia ya Sh. milioni 247.2 kwa madai kuwa wamemdhulumu gari lake aina ya Range Rover Sport.

Kamwelwe anaiomba mahakama imuamuru Makonda na Malecela, kumlipa kiasi hicho cha fedha kama fidia anayodai kuwa imetokana na hatua ya wadaiwa hao kumdhulumu gari lake jeusi aina ya Range Rover Sport lenye namba 20153.

Mdai huyo (Kamwelwe) katika hati yake ya madai anataka Makonda na Malecela, walimpe Dola za Marekani 11,250, kama gharama ya kodi ya kuliingiza gari hilo, Dola za Marekani 50,000, fidia ya kulichukua gari hilo pamoja na dola 45,000, ambayo ni thamani ya gari hilo.

Pia Kamwelwe alidai Makonda ameendelea kuitumia gari hiyo hata baada ya kuondolewa madarakani licha ya kwamba si mali yake halali.

Katika hati yake ya madai, Kimwelwe amedai mwaka 2017 alifuatwa na William Malecela maarufu kwa jina la Le Mutuz na kumueleza kuwa Makonda anaomba amuazime gari aina ya Range Rover.

NIPASHE
 
Mlalamikaji pumbaf zake!

Eti " mlalamikiwa anaendelea kulitumia hata baada ya kutoka madarakani"!

Kwa hiyo waliingia mkataba kuwa alitumie akiwa madarakani na akiachia ngazi ndiyo amrejeshee au alipaki?
 
Hahaaaa je kwa sasa Makonda anakonda au ananenepa? Yeye binafsi kwa sasa anapenda kukonda au kunenepa? naomba mawakili wasikose kumuuliza maswali haya.
 
WATAMPATA WAPI??MAKONDA KASHAMPA LISHOGA LIMOJA HILO JAMAA. SASA HIVI LIPO LODGE LINATAWANYA MATOPE KWA KWENDA MBELE
 
Hii kesi watu waliitazama kwa hasira zao kwa makonda,nilisema toka mwanzo haina mashiko,jitu zima la miaka 30+ linatapeliwa gari kweli !!
Hata wale walioambiwa walipe mamilioni kwenye plea bargain mliwaita mazuzu na mafisadi hivyo hivyo, baada ya kauli ya mama mmekuja kivingine...
 
Hata wale walioambiwa walipe mamilioni kwenye plea bargain mliwaita mazuzu na mafisadi hivyo hivyo, baada ya kauli ya mama mmekuja kivingine...
Mkuu ikoko, hivi ninaweza kuja hapo nyumbani kwako nikuombe gari yako (hatufahamiani ila unanisikiaga tu) ukubali kunipa gari yako hiyo ya thamani bila hata uwepo wa wanasheria kweli ?
 
Back
Top Bottom