Mawakili wa Mpina walivyoijibu Serikali kesi aliyomfungulia Spika, Waziri wa Kilimo

Mawakili wa Mpina walivyoijibu Serikali kesi aliyomfungulia Spika, Waziri wa Kilimo

Shakari

Senior Member
Joined
Jul 6, 2022
Posts
188
Reaction score
570
Mawakili wa Mbunge wa Kisesa (CCM), Luhaga Mpina wamejibu hoja za pingamizi la Serikali katika kesi ya Kikatiba aliyoifungua dhidi ya Spika wa Bunge la Tanzania na wenzake wawili, kuwa pingamizi hilo halina mashiko na wakaiomba Mahakama ilitupilie mbali.

Katika kesi hiyo ya Kikatiba, Mpina anapinga Bunge na utaratibu uliotumika kumpa adhabu ya kumsimamisha kuhudhuria vikao 15 vya Bunge hilo, kwa tuhuma za kusema uwongo dhidi ya Waziri wa Kilimo.Alipewa adhabu hiyo Juni 24, 2024, baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka kuwasilisha ripoti yake kuhusu tuhuma alizozitoa Mpina dhidi ya Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kukiuka sheria katika utoaji wa vibali na uagizaji sukari nje ya nchi.

Kamati hiyo iliyopewa jukumu la kupitia ushahidi wa Mpina katika ripoti yake ilidai tuhuma za Mpina dhidi ya Waziri wa Kilimo hazikuwa na ukweli, ndipo Bunge chini ya uongozi wa Spika baada ya kujadili likapitisha adhabu hiyo dhidi ya Mpina.Hata hivyo, Mpina hakukubaliana na uamuzi huo, ndipo akafungua kesi ya Kikatiba dhidi ya Spika wa Bunge, Waziri wa Kilimo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.Katika kesi hiyo Mpina anapinga utaratibu uliotumika kumpa adhabu hiyo, akidai uligubikwa na kasoro mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutopewa haki ya kusikilizwa kabla ya kupitishwa uamuzi huo.

Pamoja na nafuu nyingine, pia anaiomba Mahakama hiyo iamuru alipwe stahiki zake kwa kipindi chote atakachokuwa nje ya Bunge.

Hata hivyo, Serikali imemwekea pingamizi la awali dhidi ya kesi hiyo ikiiomba Mahakama isiikilize.Katika pingamizi hilo lililosikilizwa jana Jumanne, Septemba 24, 2024, na Jaji Awamu Mbagwa, anayeiwakilisha kesi hiyo, kuanzia saa 4:40 asubuhi mpaka sasa 2:30 usiku, Serikali imetoa sababu tatu kupinga kesi hiyo kusikilizwa.Katika sababu ya kwanza Serikali ikidai Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo kwa kuwa Bunge chini ya kanuni zake za kudumu lina mamlaka ya kumsimamisha mbunge, hivyo lilifanya kilicho ndani ya mamlaka yake.

Sababu ya pili Serikali ikidai alikuwa na nafuu mbadala alizopaswa kuzitumia kwanza kabla ya kufungua kesi ya Kikatiba ambazo ni kuwasilisha kwa Spika malalamiko yake kwa maandishi, au kufungua shauri la mapitio ya Mahakama.Sababu ya tatu ili Mpina amemuunganisha mdaawa asiyehusika, Waziri wa Kilimo kwani katika kesi hiyo hakuna sababu za madai dhidi wala nafuu ambazo Mpina anaziomba dhidi yake na ikaiomba Mahakama aondolewe katika kesi hiyo.

Wakati wa usikilizwaji huo jopo la mawakili wa Serikali lililoongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Hangi Chang'a akishirikiana na Wakili wa Serikali Mkuu, Obadia Kameya na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Edwin Webiro.Mawakili hao wa Serikali wametoa ufafanuzi wa kina wa sababu hizo za pingamizi lao, huku wakirejea vifungu mbalimbali vya sheria, kanuni za Bunge, Katiba na kesi zilizowahi kuamuriwa na Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani.




View: https://youtu.be/F6uQKTlMFsY?si=DrydNHA9IN2pqPfo
 
Back
Top Bottom